Chenge kumtetea Mramba kesi ya ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge kumtetea Mramba kesi ya ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by armanisankara, Aug 23, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  Mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, kesho itaanza kusikiliza utetezi wa kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni 11.7, inayomkabili mawaziri wa zamani, Basil Mramba, Daniel Yona na Katibu mkuu wa Hazina, Gray Mgonja baada ya kukutwa wana kesi ya kujibu.

  Utetezi huo utasikilizwa mbele ya jopo la mahakimu watatu wakiongozwa na Jaji John Utamwa na Sam Rumanyika wa Mahakama Kuu waliopewa kibali na Jaji Mkuu kuendelea kusikiliza kesi hiyo wakisaidiana na Saul Kinemela.

  Upande wa Mashtaka unaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Osward Tibabyekomya akisaidiana na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kupambana na Kuzia Rushwa (Takukuru), Ben Linkolin.

  Upande wa utetezi unawakilishwa na mawakili, Herbat Nyange, Cathbert Tenga na Elisa Msuya.

  Mapema mahakama hapo bila kuacha shaka iliwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.

  Awali mahakamani hiyo, upande wa mashtaka ulifunga ushahidi wake baada ya kuita mashahidi 13 na kuwasilisha vielelezo 26 mahakamani.

  Katika kesi ya msingi, washitakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.

  Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) Government Business Corporation waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na Tausi Ally | 22 August 2012

  WAZIRI wa zamani wa Fedha, Basil Mramba ameanza kujitetea katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni huku akiwataja mashahidi sita akiwamo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge kuwa mashahidi wake.

  Mashahidi wengine watakaomtetea Mramba katika kesi hiyo, ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mwakilishi wa Kampuni ya M/S Alex Stewart Government Business Assayers, Erwine Florence, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo na Mtaalamu wa Ushauri wa Masuala ya Kodi, Florian Msigala.

  Baada ya kutaja idadi hiyo ya mashahidi, Mramba aliliambia jopo linaloongozwa na Jaji John Utamwa akisaidiwa na Jaji Sam Rumanyika, Msajili Sauli Kinemela kuwa shahidi wa sita ambaye wanatarajia kumwita, bado hajathibitisha kama atakwenda kutoa ushahidi au la.

  Mramba alieleza kuwa kati ya mashahidi hao anaotarajia kuwaita kumtetea, watatu watawasilisha nyaraka na wengine watafika mahakamani.

  Licha ya kuwataja mashahidi hao, Mramba aliiambia Mahakama kuwa atatoa utetezi wake kwa njia ya kiapo.

  Mbali na Mramba, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja nao wameiambia Mahakama kuwa na wenyewe watajitetea kwa njia ya kiapo na pia watatetewa na mashahidi hao.

  Lakini Mgonja aliongeza shahidi mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Karisti.
  Baada ya kutoa taarifa hiyo, Mramba alianza kujitetea na Wakili wake Hurbert Nyange alimtaka aieleze Mahakama chimbuko la kesi inayomkabili.

  Mramba alisema ana umri wa miaka 71. Alidai kuwa chimbuko la kesi hiyo ni malalamiko yaliyokuwapo bungeni kwa wananchi na kwenye vyombo vya habari kuwa ingawa Tanzania ina migodi kadhaa ya dhahabu, haijafaidika kwa sababu migodi hiyo ilikuwa inaiibia Serikali na kuidanganya juu ya uzalishaji na uuzaji wa madini hayo nje ya nchi.

  Alidai kuwa kutokana na malalamiko hayo, Serikali ilibidi kuchukua hatua ya kujibu hoja hizo zilizojitokeza katika jamii. Hivyo iliileta kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers kukagua migodi hiyo ili Serikali ipate maelezo juu ya malalamiko ya wananchi.

  Mramba aliendelea kueleza kuwa Serikali iliiteua BoT ifanye kazi ya kutafuta kampuni inayoweza kufanya kazi hiyo kwa niaba yake na ikafanya hivyo kwa kuingia mkataba na kampuni iliyochaguliwa ya Alex Stewart Government Business Assayers.

  "Kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers ni kampuni ambayo ipo katika kundi la kampuni za Alex Group ambazo makao makuu yake yapo nchini Uingereza, lakini kampuni hiyo ya Alex Stewart Government Business Assayers makao makuu yake yapo nchini Marekani," alisema Mramba.

  Alidai kuwa aliyeagiza BoT kufanya kazi hiyo ya kumtafuta mkaguzi wa dhahabu ni Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na kwamba wakati huo yeye akiwa Waziri wa Fedha alipewa jukumu la kuhakikisha gharama za kumlipa mkaguzi huyo zinapatikana ndani ya Serikali, BoT au popote.

  Alidai kuwa kati yake na Gavana, hakuna aliyekuwa na mamlaka juu ya mwingine na kwamba Gavana alikuwa na wajibu wa kufanya mchakato wa kumtafuta mkaguzi wa dhahabu.

  Mramba alisisitiza kuwa yeye hakuhusika kwenye mchakato huo kwa kumtafuta wala kumleta hapa nchini wala kumtuma mwakilishi yeyote kumwakilisha kwenye kamati iliyoteuliwa kufanya mchakato huo, bali alipewa agizo la kumlipa.

  "Mimi kama waziri sikuwa na mtu wangu kwenye ile kamati lakini Wizara ilituma mwakilishi, ambaye alikuwa Mwanasheria Bethar Soka wakati wa kuhoji kampuni mbili ili wachague na kwenye kujadili vipengele vya mkataba," alisema Mramba wakati akitoa utetezi wake.

  Mramba alidai kuwa katika mchakato huo, Bethar aliwahi kuandika barua TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) akiomba ushauri juu ya kipengele kilichopo kwenye mkataba huo kinachotoa msamaha wa kodi.

  Baada ya Mramba kueleza hayo, Nyange aliiomba Mahakama imruhusu kuzungumza na mteja wake, Jaji Utamwa alimruhusu. Hata hivyo, mazungumzo yao yalikuwa ya kunong'ona kitendo ambacho kilimfanya Wakili Mkuu wa Serikali, Fredrick Manyanda kupinga akiomba wazungumze kwa sauti ili na wao wasikie.

  Manyanda baada ya kutoa pingamizi hilo, Nyange alisema kwa sauti kuwa alikuwa akimwambia mteja wake aache kuzungumza juu ya mambo aliyoyasikia na yale asiyoyajua, bali azungumze kile ambacho anakifahamu.

  Kutokana na hoja hiyo, Mramba alidai kuwa wakati Bethar akiwa kwenye kamati (timu) hiyo, yeye hakuwapo wala hakujua alichoagizwa na kwamba hakuwahi kumpa mfanyakazi wake maagizo yoyote kwenye kamati hiyo na hajui Wizara ya Fedha ilikuwa na mamlaka gani kwenye makubaliano.

  Mramba aliongeza kudai kuwa BoT katika kusimamia uchumi, ndiyo yenye wajibu wa kumshauri Waziri wa Fedha, lakini Waziri wa Fedha hawezi kuishauri BoT au Gavana.

  Alibainisha kuwa mkataba kati ya Kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers na Serikali, ulisainiwa na aliyekuwa Gavana wa BoT, hayati Daud Balali na Makamu wa Rais wa kampuni hiyo, Erwine Frorence.

  Alidai kuwa Gavana alisaini kutokana na mamlaka aliyokuwa nayo pamoja na agizo la Rais.
  Akimhoji Mramba Wakili Nyange alisema: "Inasemekana kama isingekuwa wewe Gavana asingesaini huo mkataba."

  Mramba alijibu: "Mimi sikumwambia Gavana asaini, nilimwambia afungue mkataba na siyo asaini mkataba."

  Mramba alidai kuwa tangu mwanzo, Gavana mwenyewe aliomba asaini, lakini yeye na Waziri wa Nishati na Madini baada ya kujadili na kukubaliana, walimtaka afungue mkataba ili baadhi ya vitu fulani vianze kushughulikiwa ili hatimaye asaini na utekelezwe... "Nilimwambia don't sign (usisaini) nikampa na sababu."

  Jaji Utamwa ameiahirisha kesi hiyo hadi leo saa 7:00 mchana Mramba atakapoendelea kutoa utetezi wake.

  Mramba, Yona na Mgonja walifikishwa mahakamani mwaka 2008. Inadaiwa kuwa, kati ya Agosti, 2002 na Juni 14, 2004, Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa watumishi wa umma, walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

  Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao waliipatia msamaha wa kodi isivyo halali, Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hivi ni kweli Watanganyika Hawana Mind and Class? Ni kweli Tunaweza kuchezewa Akili na Viongozi Hao hao waliotuzulumu?

  Na Kujitetea wao kwa wao kunufaisha wizi wao wa Mali za Watanganyika?
   
 4. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  He's reached a new nadir.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,245
  Trophy Points: 280
  Chenge si ndio alikutwa akiwanga bungeni? Kina Mramba watashinda kwa nguvu ya pesa na uchawi wa Kinyantuzu
   
 6. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Nothing to add on there, birds of a feather flock together.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,792
  Likes Received: 83,169
  Trophy Points: 280
  Ndiyo matatizo ya kuwa na Serikali DHAIFU...fisadi anamtetea fisadi mwenzie!!! Wote hawa walihusika katika ufisadi dhidi ya rada...Kama mtakumbuka kauli ya Mramba, "Hata majani tutakula lakini lazima rada inunuliwe." Chenge alitakiwa awe lupango anachezea mvua nyingi.
   
 8. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wako timu moja wanacheza pamoja.
   
 9. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,528
  Trophy Points: 280
  Adai ndie aliye mwagiza kuitafuta kampuni ya ukaguzi nje ya nchi na ndie aliyemwagiza kutoitiza kodi kampuni hiyo
   
 10. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHANZO: GUMZO LA JIJI  WAZIRI wa zamani wa Fedha, Basil Mramba ameanza kujitetea katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni huku akiwataja mashahidi sita akiwamo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge kuwa mashahidi wake.

  Mashahidi wengine watakaomtetea Mramba katika kesi hiyo, ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mwakilishi wa Kampuni ya M/S Alex Stewart Government Business Assayers, Erwine Florence, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo na Mtaalamu wa Ushauri wa Masuala ya Kodi, Florian Msigala.
   
 11. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mramba kama kiongozi why he remained inept upon realization that Bethar was seeking to help in tax evasion?
   
 12. data

  data JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,793
  Likes Received: 6,571
  Trophy Points: 280

  umepotoka..
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  watanzania tusipumbazwe, kikwete alisha sema Mramba ni safi, Lowasa ni safi, Rostam ni safi, Chenge safi..sasa basi kama majaji wameteuliwa na kikwete na wanailinda serikali iliyoko madarakani subirini maajabu..
   
 14. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee baba yangu hawa jamaa wamechoka ile mbaya tatizo lao hao jamaaa hizo pesa hawakumpa jei kei afanyie kampeni ndio maana jei kei kawatosa
   
 15. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  hivi ukisikia kila siku watu wanaongelea pengo kati ya matabaka hamuwaelewi!?
  Hili ni tabaka lingine la Watanzania ambao upataji wao wa pesa ni kwa njia hizo hizo na hata wakiwa na kesi wanateteana wenyewe kwa wenyewe.
  Na hapo ndipo tutaijua kweli na hiyo kweli kututumbukiza zaidi kwenye utumwa mamboleo!

   
 16. peri

  peri JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mafisadi kwa mafisadi wanateteana, tusubiri tuone ila binafsi nina imani na mahakama.
   
 17. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna zuri litakalofanya kulipiza ubaya! Wewe ngoja tu. Sisi masikini tuko mikoani vijijini tunateseka, wao wanakula mapesa yetu kwa kusema ooo.... Wakili, wakili. . .Utetezi. . . .Sijui nini. . . Lakini hiyo Darisalama kuna siku mafisadi wataina ndogo na yamoto kama thermos ya chai.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,792
  Likes Received: 83,169
  Trophy Points: 280
  ...Kama huna cha maana cha kuchangia ni bora ukae kimya badala ya kuandikia upuuzi....Vinginevyo utacheza na kibano.

   
 19. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Hii kali yaani fisadi atamtetea fisadi mwenzake ,+1 + -1 = 0
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,909
  Trophy Points: 280
  chenge anawajua mahakimu wote huyu allikiwa mwanasheria wa serikali mtamuambia nini? Kila upenyo anaujua tena sana tu kwa hiyo nyie andikeni kuwa mmeumia
   
Loading...