Mzingo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 4,766
- 10,611
Siku moja nimeenda kibanda cha chips
MIMI:Mtaalam nifanyie chips kavu
MPISHI:Subiri kidogo ziko jikoni
MIMI:si unipe hizo za kwenye kabati hapo? Nataka kuwahi.
MPISHI:Hio zimepoa,subiri hizi fresh . Zipo kidogo kwenye chombo kwa hiyo zitawahi kuiva
MIMI:Unazingua,zijae zisijae zote zinatumia muda mmoja{hapa nikamchokoza ili afunguke zaidi}
MPISHI:Kiongozi nina uzoefu katika hilo,zikijaa zinachukua muda sana,kama vipi nikupe hizo za kabatini.
MIMI😛otezea ,nitazisubiri
Kuna chemsha bongo isemayo:-
Kuna majiko mawili,sufuria mbili zenye kiasi sawa cha maji na majiko yote yamewashwa kwa viwango sawa. Sufuria ya kwanza ina yai moja,sufuria nyingine ina mayai 15. Majiko yamewashwa muda mmoja. Ni yai moja au mayai 15 ndio yatawahi kuiva?
Ili yai liive linahitaji lifyonze Joto(heat energy) kutoka kwenye maji/mafuta na mafuta/maji yatafyonza joto hiyo kutoka kwenye jiko. Wingi wa mayai utafanya mahitaji ya joto yawe makubwa hivyo yatagawana joto dogo lililopo kwenye mafuta na mafuta/maji yatakuwa yanachukua joto jikoni mpaka ifikie hatua kiasi cha joto kinachohitajika kwa mayai yote kuiva kimepelekwa kwenye mayai.
Inafanana kidogo na wazazi wawili wenye vipato sawa kwa mwezi ila wanasomesha idadi tofauti ya watoto kwenye shule moja,itamchukuwa miezi mingi yule mwenye watoto wengi kukamilisha ada(chukulia kuwa majukumu yao ni kusomesha tu)
Jibu ni yai moja,muda utakaotumika na mayai 15 ni mwingi zaidi ingawaje sio mara kumi na tano ya ule wa yai moja.
Watu hukaririshwa kuwa muda utakuwa sawa.
NB:Niko tayari kwa changamoto