niko macho ndio maana naweza kuchati na wewe nakuuliza kwani ndege hazitui au wewe mpaka uone majengo mazuri ndio utajua umefika airport.
sio kwa serekali hii yenye surakali na serakali
yaani sirikali nyingine ikiingia madarakani sijui itaanzia wapi maana elimu ccm wamekwishaimaliza madini wametuachia maandaki afya ndio ukiwa na kitambi unaonekana una afya bora, kilimo ndio hicho kimekuwa kwanza, twiga wanapandishwa ndege, maji tunalipia lakini ukifungua bomba zinatoa hewa na sisi hatujalipia hewa, umeme nao tunalipia ukitoka kununu vocha ya luku ukifika nyumbani huwei kuweka maana umeme hakuna.
wewe unataka tukajenge majengo mazuri airport wakati watu hali zao ni mbaya hospitali watu wanalala chini hakuna vitanda wla madawa wala vifaa tiba mashule walimu wamechoka wanajinunulia chalk na kuuza vitumbua hatuna hata mtaala wa elimu walimu hawana nyumba za kuishi baadhi ya shule hazina hata matundu ya choo au wewe hujasikia kuna shule inafugwa kwakukosa chakula? wewe unataka majengo ya kurushia twiga? usafi wenyewe kwenye miji umekuwa kwa hisani ya watu wa marekani
We have a long way to go and we don't know where are we heading to