CHEMSHA AKILI yako utoe jibu.

mkuu ukinikopesha 10,000 halafu nikaahirisha na kusema nipe 7000 na kurudisha elfu tatu deni si linakuwa 7000. sasa we umerudisha mia mbili deni si linakuwa 9800, mia yako plus 9700 ya nguo. yaani deni ni ile hela uliyoenda kutumia sio miambili uliyo rudisha. NB ukimlipa mtu hela aliyo kukopesha bila kuitumia ni sawasawa na haukukopa
 
we vp unajumlishaje hiyo mia iliyobaki tena badala ya kutoa kwenye 9800 ili ibaki 9700 sawa na bei ya bidhaa, Bongo yako mbovu mwone kwanza?!!
 
Hiyo 100 iliyobaki utampa dada 50 na kaka 50,hivyo kiusahihi mgawo wa dada ni 4950 na kaka 4950 na wewe ,00.
 
Nguo inauzwa sh. 10,000.00 wewe huna pesa ukaamua kukopa kwa dada sh. 5,000.00 na kwa kaka sh. 5,000.00 ukapata sh. 10,000.00. Ukanunua ile nguo kwa sh. 9,700.00 na ukarudishiwa sh. 300.00, Ukaamua kupunguza deni, ukatoa sh. 100.00 kwa dada na sh. 100.00 kwa kaka. ukabaki na sh. 100.00. Hivyo ukawa na deni la sh. 4,900.00 kwa dada na sh. 4,900.00 kwa kaka, jumla sh 9,800.00, ukiongeza na ile sh. 100.00 yako, inakuwa sh. 9,900.00. Je sh. 100.00 imekwenda wapi?Nawasilisha.

Dreamliner naona umewachanganya wana jamvi wengine wanajibu kwa hasira, ila jibu langu ni hili:
Ulikopa 10,000
matumizi 9,700
Umerudisha deni 200
Umebakiwa na 100
Ili kujua deni lako kamili unapaswa kuangalia thamani uliyonayo jumlisha pesa mkononi halafu
9700 + 100 = 9800 na wala sio 9800 + 100, ili kutumia njia uliyopitia weweyapasa kuwa hivi
9800 + 200 na sio 100

nawasilisha
 
Kimsingi deni lako ni sh 9,800 tu (9,700 ya manunuzi na sh 100 ya matumizi yako) na sio sh 10,000 kama unavyolazimisha ili utupumbaze. Hizo sh 200 haziwezi kuwa deni maana ulipewa ukazirudisha.
 
Dreamliner naona umewachanganya wana jamvi wengine wanajibu kwa hasira, ila jibu langu ni hili:
Ulikopa 10,000
matumizi 9,700
Umerudisha deni 200
Umebakiwa na 100
Ili kujua deni lako kamili unapaswa kuangalia thamani uliyonayo jumlisha pesa mkononi halafu
9700 + 100 = 9800 na wala sio 9800 + 100, ili kutumia njia uliyopitia weweyapasa kuwa hivi
9800 + 200 na sio 100

nawasilisha

Nimecheka sana Kaka Lol. jamaa wananionea bure.
 
Nimekuja mbio nikadhani mambo ya migomo. Kumbe MATHEMATICS BANA DUUUH!!!
Hiyo mia we itafutetafute tu. Usikate tamaa utaiona.
 
angalia kwenye kile kimfuko kidogo(ganja pocket) kwenye suruali ya jeans, huwa sh mia zinapoteleaga huko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom