Chemsha bongo, chemsha bongo. Karibu uweke jibu lako

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,197
2,025
Habari watu wote wa hili jukwaa la elimu.

Leo kuna mtoto wa kaka angu amekuja na hii chemsha bongo na kusema ukweli naona kuna kila dalili ya mimi kuchemsha.

Iko hivi" Nguo dukani inauzwa Sh.10000/= Na wewe hauna pesa ila hiyo nguo unaitaka, ukaamuwa kwenda kukopa kwa kaka ako Sh.5000/= na Dada ako Sh.5000/= na wote wakakupa.Ukapata jumla ya Sh.10000/=.

Ulipoenda dukani muuza nguo alikuuzia hiyo nguo kwa Sh.9700/= ukabakiwa na Sh.300/=.

Baada ya kubakiwa na Sh.300/= ukaona ni bora upunguze deni lako kwa kaka na dada ako.Hivyo kaka ako ukampa Sh.100/= na Dada ako Sh.100/= We ukabakiwa na Sh.100/=.

Sasa ulipoweka sawa mahesabu ukagundua dada atakudai Sh.4900 na kaka sh.4900 ambayo jumla itafanya Sh.9800/=Ukijumlisha na Sh.100/= uliyobaki nayo itafanya jumla ya Sh.9900/=.
Je,Shilingi 100/= imeenda wapi
 
shlng 100 ulibakia nayo n den pia so jumlishia na hiyo ulouziwa nguo so jumla unadaiwa 9800 hamna ilopotea hapo
 
Na hivyo ndio wengi hupata hasara Kwenye biashara Kwa kudhani hela aliyojichukulia dukani au Kwenye biashara zao haina shida. Wanaipotezea
 
shlng 100 ulibakia nayo n den pia so jumlishia na hiyo ulouziwa nguo so jumla unadaiwa 9800 hamna ilopotea hapo
sijakuelewa mkuu, Hapo anadaiwa sh 9,700 kwakuwa amelipa jumla sh 300 kwenye deni la sh 10,000.
 
Back
Top Bottom