Chemistry ya wanawake inanichanganya sana jamani

Chemistry ya wanawake inanichanganya sana jamani

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
12,072
Reaction score
16,624
Mambo vip wanaume wenzangu?

Ebu tupeane mawazo kidogo hapa kuhusu tabia{chemistry}za wadada.

Kuna visa viwili kuwahusu wadada wawili ambao nliwatongoza kwa nyakati mbili tofauti,wa kwanza nlipomtokea alikua ndo ana kama miezi mitatu tangu atoke kuachana na mpenzi wake wa awali kwa mujibu wa maelezo yake.

Nikampiga voko zangu akazielewa but akaniambia atanijbu, sasa kila nlvokua namkumbushia ombi langu akawa kama ananikwepa.

Basi siku flani nikamkomalia mwishowe akaniambia tuwe marafiki wa kawaida tu, me nikamwambia nina marafki wengi tu so kama ndo jibu alilopanga kunipa hilo basi me ngoja nijiweke kando nae.

Akawa ananiambia kuwa nisije nikamchunia coz bado anahitaji close r'ship na mimi ila me nkashkilia msimamo wangu maana nilijua labda lengo lake ni kunichuna tu kama ilivyo kawaida ya mabinti wa mjini.

Me sikuangalia nyuma tena nikasepa zangu wala sikumtafutaga tangu wakati ule.

Manzi wa pili alikua ni mtoto wa mkurugenzi wa shirika flani la umma hapa nchini, huyu tulikutana kwenye zile venue maarufu pale udsm za yombo 4 na 5.

Mazingira yaliyotufanya tukajuana ni tulikuwa tunapigana chabo paper ya accounts, hapo ndo ukawa mwanzo wa kujuana.

Basi kama kawa nikampiga sound ye akanambia ana mtu wake,but cha ajabu nkimuomba tutoke out anakubali, nikimbusu anasema asante.

But nikimkumbushia ombi langu anasema tuwe marafiki tu, basi me nikaona nisiendelee kupoteza muda kwake.

Nikamwambia tupotezeane akakubali.

Sasa tangu nipotezeane na hawa viumbe hatukuwah kutafutana, ila siku za hvi karibuni nlipatwa na kiherehere flani cha kuwatafuta kila mmoja kwa wakati wake.

Nikaanza wa kwanza akanambia kwa nilichomfanyia kipindi kile hataki hata kunisikia tena katika maisha yake.

Nikasema poa mama isiwe kesi ya hadi kupelekana the hague nikamchunia, nikamtafuta wa pili nae huyu ndo balaa.

Akaniambia me sijui ni mwanaume wa aina gani mwenye maamuzi ya haraka haraka, mara sijui nilicorrupt her minds then nikamuacha akiwa anahang tu, hivyo nae hataki kunisikia tena katika maisha yake.

Sasa najiuliza, hawa watu wote maombi yangu waliyakataa, me nikaona nisiendelee kupoteza nao muda bora niangalie opportunities zingine.

Leo tena me ndo naonekana mmbaya kwao, au nyie wenzangu situation ya wanawake wa namna hii huaga mnaisolve vipi?

Maana me science ya hawa viumbe inanitoa knock out kabisa?
 
kwanza mm nilijua ww ni she, id yako imekaa ki she she hv!
 
ulikosea kitu kimoja w.ke design km hyo hutakiwi kusisitiza upewe jibu kinachotakiwa ni kuishi nao hvyo wanavyotaka mwisho wa siku unakula pweza gizani...unajua w.ke wengine hawawezi kusema wamekubali lkn actions zao zinaonesha kwmba washakubali ss ww ulikosea kufanya maamuzi ya haraka
 
kwa mazingira hayo waliyokuwa wakikuonyesha maana yake walikuwa wamekubali. wanawake wengi huwa hawakubali kwa kusema ndio, ni wewe tu kujijumlisha na kutoa kupata jibu.
 
vipi,nawe yalishakukuta nini?

Ndio ndugu yangu tena nina story kama ya kwako
Sema nachokielewa huwaga wana wengine wanaokua nao in fact sio mbaya sema ukiwa ----- utalea sana huku akikuona mjinga
Cha maana we tafuta tuu usikate tamaa hawa viumbe hawaelewekagi

Tena usiwe na maamuzi ya haraka wee nenda nao taratibu ukiona ni chenga wee jitoe kiroho safi na usahau kabisaa na namba futa kabisaa
 
umezingua ww..we unatongoza kama uko primary...demu akishakwambia ngoja nikafikirie ntakujibu,jua una asilimia kubwa za kumpata..kinachotakiwa baada ya hapo ni kumuonyesha kile ulichomwambia ili naye ajiridhishe kabla ya kukupa jibu..sasa ww unaendelea kutongoza tu na kudai majibu deile kama vile ulimkopesha
 
Una umri gani tang'ana?

Naomba wamiliki wa JF tukimalizana na uchaguzi watuwekee jukwaa la wavulana na mabinti.

Ingekuwa vizuri tukawa na MMU- boys and girls na MMU originale (kwa wahitimu na wastaafu kama Babu)...Lol!!

cc Invisible
 
Last edited by a moderator:
umezingua ww..we unatongoza kama uko primary...demu akishakwambia ngoja nikafikirie ntakujibu,jua una asilimia kubwa za kumpata..kinachotakiwa baada ya hapo ni kumuonyesha kile ulichomwambia ili naye ajiridhishe kabla ya kukupa jibu..sasa ww unaendelea kutongoza tu na kudai majibu deile kama vile ulimkopesha

Nenda mdogo mdogo na wadogo zenu... watafikia huko mlipo siku moja.
 
inaonekana nkifungua darasa la mtongozo humu ndani sitalala njaa... kama ni kutokea watoto mkuu una F nene kabisa
 
inaonekana nkifungua darasa la mtongozo humu ndani sitalala njaa... kama ni kutokea watoto mkuu una F nene kabisa


Kwa nini unamfelisha mtoto wa mwenzio? Umesahau kwamba na wewe umepita huko huko?

Toeni bure kama mlivyopewa bure......Wadogo zenu wamekwama, wasaidie watoke kwenye tope zito!
 
teh teh..nimekuelewa mkuu


Kuna ombwe kubwa sana kwenye haya mambo ambalo linaendelea na kukutana na lile la vijana kutofikia viwango vya kazi.

Kuna ombwe kubwa kwenye hili eneo kama ilivyo kwa utawala wa li nchi letu.

Msaada wa dharura unahitajika haraka sana!!
 
Back
Top Bottom