Makubaliano haya yamedhaminiwa na mashabiki wa Chelsea fc, Mungu ibariki chelsea, pole Eli79
Ila Wakuu msije mkawa mnakimbilia BAN ili kukimbia aibu ya kipigo, naona kama mnaogopana vile? Wekeni ngawira bana ili mtu awepo kujitetea hapa baada ya kibano
Ntuzu na mwenzako elie Invisible kasha-like hii post yako. Mnakumbuka ya Salamander na mwenzie Roots?Mkuu ata Mimi naomba Ban kubwa mpk msimu huu uishe iwapo Chelsea atafungwa na Arsenal hiyo tarehe 26..
Tena sitanii kabisa Invisible ktk hili. Nipigwe ban mpk mei tarehe 20. Naomba kabisa tafadhali
Hawa Gunners wanataka kutuchezea!
Ntuzu na mwenzako elie Invisible kasha-like hii post yako. Mnakumbuka ya Salamander na mwenzie Roots?
Kwenye football hivi vitu vipo kaka, siku ile niliusoma mchezo kisaikolojia ya timu zote mbili, nikaona wakatalani lazima waondoke. Kama nilivyotegemea, Los blancos walitawala mchezo, lakini kulikuwa kuna vijimambo tu ndio vilibadilisha matokeo. Lakini ndio soccer ndani ya JF, ukiamini chama lako omba ban.
Hata hivyo Chelsea huu mwaka wao!
Mourinho kamanda b5-click nimekuja..b5-click ukuye ukuye pande hii
Ntuzu na mwenzako elie Invisible kasha-like hii post yako. Mnakumbuka ya Salamander na mwenzie Roots?
Mentor mbona umeni-ignore kwenye hii comment though mimi ndio nimeanza kuwaomba hawa mabwana wasikimbie jukwaa kwa kujificha nyuma ya BAN baada ya mkong'oto, acha hizo bana😜Wakuu b5-click Ntuzu Eli79 na mheshimiwa Invisible,
Naomba mbadilishe bet yenu kwani;
- b5-click na Ntuzu na Eli79 tutakosa michango yenu kwa michezo iliyobaki. Jukwaa hili si kwa ajili ya mechi ya Arsenal vs Chelsea peke yake. tuna mchezo na liverpool baada ya hapo na kushangilia ushindi wa kombe. Jambo hilo halitafana bila uwepo wenu!
- kwako mheshimiwa sana Invisible, kufana kwa jukwaa hili kunamtegemea kila member mmoja mmoja. Kumpiga ban member yeyote kunapunguza lengo letu hilo.
Baada ya kusema hayo ningependelea kutoa solution ambayo itawanufaisha wote: Kila mmoja kwa makubaliano yenu wenyewe atume pesa kwa invisble ambapo kwa ambaye timu yake itashinda basi ile pesa ya mwenzake iwekwe kama mchango wa membership (bronze, gold, ...) na pesa yake (yule aliyeshinda) atarudishiwa.
Hivyo basi, kwa mfano, kama b5-click na Eli79 kila mmoja akituma 30,000/- basi mwisho wa siku timu itakayoshinda mmojawapo atarejeshewa pesa yake na hiyo ya aliyeshindwa itaenda kama membership ya mwenzake.
Hapo vipi?
Kama mkuu Invisible akikubali mimi nitaomba kubet na BAK tafadhali.
Ntuzu tafuta wa kwako...