Hili gari nimelisikia tangu mwaka jana na nina hamu nalo kweli ilia angalau nami niweze kujinunulia na kutekenya gari jipya! Bahati mbaya sijawahi kuliona hapa Bongo, sijui kwa nini. Naamini kuna Watanzania wengi ambao hatujawahi kumiliki magari mapya zaidi ya mitumba ya Kijapan, ni \vema watuletee hapa kwetu.
Nyumbu ilitelekezwaga baada ya Nyerere kung'atuka na hata yale magari yao yaliyokuwa yakiendesha Jeshini nadhani hayapo tena. Si wajua kununua magari mapya kutoka nje ya nchi kuna kamisheni? Jamaa wa Nyumbu wamebakia kubuni mashine rahisi kama za SIDO, imebidi wafanye hivyo maana Serkali ni kama imeshawaacha.