Chato yatangazwa kuwa kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ziarani Mkoani Geita ametangaza rasmi kuwa Chato ndio kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa

Amesema wamefikia uamuzi huo kwasababu kuna Utalii wa aina mbalimbali katika Wilaya hiyo ikiwemo wa Misitu, Maji, Hifadhi za Taifa na Uwindaji. Pia, Uwanja wa Ndege wa Chato utawezesha Watalii kusafiri kwa uhakika na urahisi

Vilevile, Waziri Ndumbaro ameielezea Chato kuwa eneo tulivu, hali ambayo inapendwa na Watalii.

 
Sijui huyu Ndumbaro ana PhD ya ushuzi? Kwani hata kama Magufuli alikupa ubunge wa bure na uwazirí wa utalii lazima alipe fadhila kwa kujipendekeza kizembe namna hiyo?

Zote alizotoa kama sababu za Chato kuwa kanda ya Utalii ni pumba tupu. Hamna hata moja inayozidi maeneo mengine kwenye kanda ya ziwa.

Hawa akina Ndumbaro baada ya utawala huu wa Magufuli ni moja kati ya mambo tutaomba vyuo vilivyowapa hizo PhD wazi NULLIFY, yaani WAZIFUTE
 
Hana akili kabisa.

Hii nchi zaidi 85% ya watalii huwa wanakuja kwa ajili ya mbuga ya Serengeti tu, kisha Ngorongoro 5% na mbuga nyingine zote combined ndio wanachangia 10% halafu leo uje kuweka Chato kitovu cha utalii?

Sasa naona kwa kuwa Chato ndio kila kitu sasa, naomba tuwasaidie kupendekeza ni vitu gani vipelekwe Chato.

UDSM, IFM, UDOM, UN, World Bank, IMF, na taasisi zote kubwa naomba zihamie Chato ili tuifanye Chato kua "Calafonia" ya Afrika.

Chato kujengwe kituo kikubwa cha kijeshi, Chato waweke deport kubwa ya magari, Chato kujengwe viwanda vikubwa vya ndege, Boeing wajenge kiwanda Chato, Toyota ijenge kiwanda kikubwa cha magari. Muhimbili wahamie Chato.

Nashauri Dunia iitazame Chato kwa jicho la pekee sana.
 
eti chato kuna vivutio vingi vya utalii ikiwepo utalii wa maji na utalii wa mashamba ya miti pia Chato kuna amani na utulivu sana kitu ambacho kinawavutia sana watalii
Yaani siamini nachokisoma, sijui tulilogwa na nani, mtu mzima na akili zake anasema kuna utalii wa maji! Mbona yapo dunia nzima?

Huyo alietuloga sasa hivi amekaa mahali anatucheka kweli.
 
Back
Top Bottom