Rais Samia amteua Dkt. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi, alisema Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa naye, amewateua wajumbe sita wa bodi hiyo.

Aliwataja wajumbe hao niJacqueline Woiso, ambaye ni Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Tindi Mndolwa Mkuu wa Itifaki, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kitengo cha Diplomasia
na Said Kamugisha, ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya uhamiaji naMwanasheria.

Wajumbe wengine ni Omar Mohammed, ambaye ni Mkurugenzi wa Utaratibu na Usimamizi wa Utalii, kutoka Tume ya Utalii Zanzibar na Mdau wa Utalii Zanzibar, Mozza Salim Mauly ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utali, inayojulikana kama Mauly Tours and Safari na Mdau wa Utalii Bara pamoja na Dk. Tereza Mugobi, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii na Mtaalamu wa Utalii.

Pia, alisema Damas Mfugale atakuwa Katibu wa Bodi hiyo ya Utalii, atakuwa na jukumu kubwa la kuwasimamia
wajumbe hao, kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

Wakati huohuo, Waziri Mchengerwa alimthibitisha Dk. Tereza Mugobi, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii nchini, awali alikuwa anakaimu nafasi hiyo.

Waziri Mchengerwa ameteua wajumbe hao, kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha Sheria ya Bodi ya Utalii, Sura ya 364 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali namba 4 ya mwaka 2019. Pia, alisema mchakato wa kuwapata wajumbe hao umefanywa ndani ya miaka mitatu.
 
Halipo ktk list ya mashirika yasio na tija
 
Back
Top Bottom