Shaka: Rais Samia ameipaisha Sekta ya Utalii nchini

MTANZANIA620

Member
Jun 20, 2023
34
30
Na Shaka Hamdu Shaka

MAFANIKIO KUMI YA RAIS SAMIA KATIKA SEKTA YA UTALII

1. Kupungua kwa ujangili kulikotokana na kuimarika kwa uhifadhi ikiwemo kuundwa kwa jeshi usu la wanyamapori na misitu. Hali hii imepelekea kuongezeka kwa wanyama maradufu wakiwemo tembo, faru, simba, mbwa mwitu, na kustawi kwa misitu kwa kiasi kikubwa.

2. Kuridhia mpango wa chanjo dhidi ya UVIKO19 kuliifanya Tanzania kuondolewa katika Nchi zenye hatari kutembelewa mpaka kuwa katika nchi salama kutembelewa hali iliyowafanya wageni kupanga safari za kuja kwa mapumziko na kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii nchini pamoja na masuala ya kiuwekezaji na biashara.

3. Kuonesha kwa vitendo kuwa yeye ndiye balozi namba moja katika kuitangaza Tanzania na kukuza chapa yake kwa kucheza filamu ya Tanzania The Royal Tour ambayo imetazamwa na mamilioni ya watu duniani.

Kwa sasa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amerekodi filamu na Muigizaji maarufu wa filamu nchini China Jin Dong katika hifadhi ya Arusha iitwayo 'Karibu Kijiji cha Milele' filamu ambayo itaoneshwa kwenye televisheni na mitandao ya kijamii nchini China lengo likiwa ni kuendelea kuwavutia watalii.

Aidha serikali inatumia ndege za kampuni ya Emirates kutangaza vivutio vya utalii mpango ambao umesaidia kuongeza idadi ya watalii

Pia serikali inatumia timu za mpira wa miguu ikiwamo Atletico Madrid, Getafe na Real Valladolid kutoka Laliga Uhispania na timu za mpira za Ajax na PSV kutoka Uholanzi kutangaza vivutio vya Utalii katika viwanja vya timu hizo kwa kuweka matangazo hayo katika mbao za viwanja hivyo. Lengo ni kuendelea kuongeza idadi ya watalii kwa kuwa ni timu zenye wafuasi wengi pia.

4. Katika kipindi cha miaka yake takribani mitatu sasa na kwa kuzingatia hatua alizozichukua hapo juu nchi yetu imeshudia ongezeko kubwa la watalii kutembelea maeneo ya hifadhi au yaliyohifadhiwa kutoka watalii 562,549 mwaka 2020 hadi zaidi ya watalii 958,953 Juni, 2023 kwa watalii wa ndani na kuiwezesha serikali kuongeza mapato yake kutoka shilingi bilioni 9.7 mwaka 2020 hadi shilingi bilioni 15.25 kwa kipindi cha Juni, 2023

Vilevile idadi ya watalii kutoka Nje ya Nchi waliongezeka kutoka watalii 620,000 mwaka 2020 hadi watalii 1,210,692 katika kipindi cha Juni, 2023 ambapo waliipatia Nchi yetu dola za Marekani bilioni 1.525 kutoka dola za Marekani milioni 754.59 mwaka 2020.

5. Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara na madaraja ndani ya maeneo ya hifadhi na misitu kumeboresha usafiri wa watalii wawapo maeneo hayo.

6. Amehuisha demokrasia, anatekeleza utawala wa sheria unaohakikisha haki na usawa kwa kila mwananchi, uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari hali ambayo imeimarisha umoja wa kitaifa na kuifanya Nchi yetu kuendeleza utulivu wa kisiasa, amani na usalama vilivyodumu miaka 60 ya uhuru wetu. Hii ni misingi muhimu katika kukuza utalii, biashara na uwekezaji popote duniani.

7. Minada ya vitalu vya uwindaji inafanyika kwa uwazi na usawa bila urasimu wala rushwa kupitia njia ya kielektroniki hali inayochochea uwekezaji mahiri katika sekta hii ya uwindaji wa kitalii.

8. Utalii wa mikutano ambayo ni matokeo ya kuimarika kwa mahusiano na diplomasia yetu na mataifa ya ulimwengu pamoja na mashirika na taasisi za kimataifa hususani diplomasia ya kiuchumi, kiutamaduni na kimichezo.

Tanzania imekuwa Mwenyeji wa mkutano wa chama cha mpira wa miguu Africa (CAF) Agosti, 2022

Tanzania imekuwa Mwenyeji wa Baraza la Utalii Afrika (Africa Tourism Council-ATC) uliofanyika Zanzibar mnamo mwezi Septemba 2022;

Tanzania imekuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 65 wa Utalii wa UNWTO kamisheni ya Afrika, Oktoba 2022.

Tanzania imekuwa Mwenyeji wa mkutano wa Jukwaa la mifumo ya chakula Afrika Septemba, 2023

9. Tanzania kwa kushirikiana na Nchi za Uganda na Kenya zimefanya maombi ya kuwa wenyeji wa mashindano ya mpira wa miguu kwa mataifa huru ya Afrika (AFCON) mnamo mwaka 2026

10. Kupitia uhifadhi wa misitu serikali inahamasisha na kuwezesha ufugaji wa nyuki na urinaji wa asali kwa njia za kisasa kupitia mfuko wa wajasiriamali wa mazao ya misitu (TaFF) pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya kuongeza thamani mazao ya misitu na kutengeneza bidhaa zitokanazo na mazao ya misitu hapahapa nchini.

Pia serikali imeanzisha Programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki (BEVAC – Support to Beekeeping Value Chain Programme) utakaonufaisha wananchi wa mikoa saba ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa jitihada hizi Tanzania inashika nafasi ya 14 duniani na nafasi ya 2 Afrika kwa uzalishaji wa asali. Hata hivyo bado tuna uwezo wa kuongeza uzalishaji wa asali na tukafikia namba moja Afrika na nafasi tatu za juu duniani.

Tanzania imechaguliwa pia kuwa mwenyeji wa mkutano wa Dunia wa Ufugaji Nyuki (APIMONDIA) mwaka 2027 utakaowaleta wageni 6,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.

#RaisNiSamia #T2025SSH
 
Mungu awasaidie sana watoto wangu na uzao wao, wasije wakawa na tabia za upambe skuizi mnaita uchawa....
Amen...🙏
 
Anampigia chapuo Mzanzibari mwenzie ili ateuliwe ubunge kisha uwaziri kwenda utalii akakamilishe vyema uporaji wa rasilimali za Tanganyika. Haridhiki na UDC wa mchongo huko Kilosa ambapo inawezekana amepora ardhi za wananchi.
 
Back
Top Bottom