Kwako Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (Mb),
Hatua za haraka zinahitajika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere/Selous. Mgogoro mkubwa unaanza kuibuka kati ya waendesha utalii (tour operator) na watalii wanaoenda kwenye hifadhi hii. Kitendo cha Maaskari wa Mbuga kuwatoa kwa nguvu watalii kwenye ndege hakikubaliki, ni ukosefu wa maadili, akili (commonsense), na nidhamu ya kazi. Tusisubiri hadi watalii wakapigwa, tutaua utalii kwa kukosa maarifa.
Jana Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Mbuga za Taifa wa kanda ya kusini alifanya kikao na wadau wa utalii katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere kilichofanyika kijiji cha Mloka na kutoa maagizo ya ghafla kwa kila muendesha utalii (tour operator) kulipa tozo ya dola za kimarekani 82.6 kwa kila mgeni (non-residents) na tozo muhsusi kwa wageni wengine ambao atatumia kiwanja kidogo cha ndege cha Mtemere (Selous Mtemere Airstrip).
Tozo hii haijalishi kwamba mgeni alipatikana kabla au baada ya utekelezaji wa amri hii, hivyo kumlazimisha muendesha utalii kulipa hata bila kujali kwamba malipo haya hayakujumuishwa kwenye malipo ya mgeni. Kwa mfano kwa muendesha utalii mwenye wageni 10 atapaswa kuwalipia dola za kimarekani 826. Pamoja na waendesha utalii (tour operators) kuomba muda (grace period) kumekuwa kukitumika nguvu, lugha chafu ambazo zinahatarisha utoaji wa hudua kwenye mbuga hii.
Pamoja na kwamba mbuga hii bado ni changa na kukosa miundombinu ya kutosha kwa watalii, pamoja na kutopata matangazo ya kutosha hivyo kuwa na wageni wachache, katika hali isiyo ya kawaida maaskari wa hifadhi (Rangers) wameanza kutekeleza agizo hili ndani ya masaa 24 kwa kuwatoa kwa nguvu kwenye ndege watalii waliotoka kwenye kiwanja hiki kwenda Zanzibar/Dar es Salaam.
Hali hii imesababisha mgogoro mkubwa kati ya waendesha utalii (tour operators), wenye mahoteli na wageni hivyo kuhatarisha uhai wa kampuni zao, ustawi wa mbuga hii, ajira za watu, na fursa mbalimbali za kiuchumi.
Hatua za haraka zinahitajika. Pascal Mayalla