Chapa za mifugo ni ukatili kwa wanyama

dafity

JF-Expert Member
Aug 16, 2008
1,849
2,036
Chuma kinawekwa katika moto mpaka kinaiva kisha anabandikwa mnyama kwenye ngozi. Mifugo ingeweza kutamka maneno nadhani matusi yake yasingevumilika.

Watu wa haki za wanyama-TSPCA mpo wapi?
Hakuna njia nyingine ya kuwawekea alama ambayo haiumizi mwili na kuharibu ubora wa ngozi?

Tuwatendee haki wanyama!
 
Zipo kama wanazotumia mataifa mengi "Cow tag earrings"
Ni bora zaidi na haiumizi wala kuharibu ngozi, tatizo bado tuna mifumo ya miaka mia iliyopita.
Tubadilikee
0350e13b7541f228206dbde82af8e91a.jpg
 
Hapo hapo tunahimizwa kujifunza kuuza nje mazao yatokanayo na mifugo.
Nani atanunua ngozi iliyounguzwa na chapa? Lakini ni kweli lazima kuunguza ngozi ya ng'ombe karne hii? Me nilishawahi kusikia ngozi ya ng'ombe iliyopigwa chapa haina ubora tena inahesabiwa kama ngozi dhoofu.
 
Chuma kinawekwa katika moto mpaka kinaiva kisha anabandikwa mnyama kwenye ngozi. Mifugo ingeweza kutamka maneno nadhani matusi yake yasingevumilika.

Watu wa haki za wanyama-TSPCA mpo wapi?
Hakuna njia nyingine ya kuwawekea alama ambayo haiumizi mwili na kuharibu ubora wa ngozi?

Tuwatendee haki wanyama!
Je kuwachinja na kuwala hilo mbona hujaliona kua nalo ni ukatili na hujawahi lipigia kelele?
 
Naona hata bora wangewatoga masikio waweekee ile tag..
 
Nishaendaga nchi fulani nkakuta ngombe wamewekwa tag alafu ina kitu kama deal Hivi

Ova
 
Je kuwachinja na kuwala hilo mbona hujaliona kua nalo ni ukatili na hujawahi lipigia kelele?
Kula wanyama sio ukatili bali ni agizo la Mungu.

Mwanzo 1:30
"Na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo."
 
Hiyo ndio njia rahisi na nafuu, kumbuka sisi ni Waswahili ni mpaka Wazungu wapate njia mbadala ndio tuone tufanye, other wise watatandikwa hiyo tu.

Kuna inayoitwa Freeze branding, Ngombe hapati maumivu ila ni aghali kweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom