Chanzo cha umasikini Afrika sio viongozi ila ukosefu wa ujuzi wa sayansi na teknolojia

Sikiliza kijana, mie sikutoa mada hii kujadili rais yeyote ila sie wote waafrika na ujinga wetu wa sayansi na tachnolojia tunaoukimbia kwa kuwatupia lawama viongozi wetu na kucheza siasa, siasa haitajenga madaraja na reli ila mchina kama sio siye. Ukileta hoja ya Magufuli sikujibu wala sisomi kama nilivyodharau jibu lako refu baada ya sentensi ya kwanza, sina muda huo wa kuongelea hayo.
 
Sawa mzee, ila mie nazungumzia mashine za viwanda, engine za magari, ndege, meli, Drones, hata mashine za kutengenezea nguo, dawa hata za mashambani. Pia uwezo wa kutengeneza barabara, madaraja, reli n.k.
Nakuelewa sana mkuu.
Ili twende kwa kasi, tunahitaji technology (ndiyo machine unazosema) na know-how kwenye yote hayo.
Bila investment financing kwa ajili ya kutengeneza products za pamba kama nyuzi, pamba za hospitali, vitambaa, nguo, animal feeds; yote haya hayatatokea.

Hivyo basi, tungeanza na investment financing kwenye vitu vinavyozalisha kwa vingi ikuwamo agro-inputs (mbolea na viwatilifu) na kuongeza ongeza thamani kwenye output.
Then kodi inayopatikana inakuwa kubwa. Na kwenye majenzi ya miradi mikubwa kama reli, meli na barabara nako pia tunaweza kuingia ili ku-service usafirishaji wa bidhaa za kilimo na output ya madini tunayochimba na kuyachakata kwenye ubora.
 
Ni kweli tunahitaji investment, lakini technology kwanza kabla hujapata capital, hivi ndivyo wanavyofanya wenzetu, wanatoa au present idea zao baada ya kuzifanyia kazi za kisanyansi, kisha wanaomba pesa za kuendesha mradi.
 
Ni kweli tunahitaji investment, lakini technology kwanza kabla hujapata capital, hivi ndivyo wanavyofanya wenzetu, wanatoa au present idea zao baada ya kuzifanyia kazi za kisanyansi, kisha wanaomba pesa za kuendesha mradi.
Kama kuna good feasibility study ya uhakika wa soko; kwa mfano Tanzania sukari inatengenezwa yote inauzika na bado tuna uhitaji wa zaidi ya tani 50,000

Kwa lugha rahisi ukipata dhamana ya bank ya kilimo au BoT kununua technology kwa ajili ya kununua kulima miwa au sugar beet kwa ajili ya kiwanda cha sukari; baada ya mauzo unakuwa na nafasi ya kurejesha mkopo kupitia mauzo ya sukari.

Katika uchumi wa soko, uhakika wa soko unaweza kumfanya mwekezaje apate mkopo wa uwekezaji
 
Sawa, lakini tunazungumzia teknolojia ya viwanda, ujenzi na kutengeneza vyombo vya usafiri na mawasiliano etc.
 
Tatizo kelele zote huwa zinaishia humu Jukwaani Wala hata nje hazifiki....
Kuna wanaojadiliana nje ya JF, hilo nalo litasaidia kuamsha watu, kwani utajiri wa mmoja mmoja ndiyo utajiri wa taifa kutokana na kodi, na ujuzi na utaalamu unaleta utajiri, na ujuzi huu ni sisi wananchi kuujua siyo viongozi sababu wao ni wanasiasa sio wataalamu.
 
Sayansi gani unaongelea mkuu. Afrika tuna sayansi na techno ya hali juu kupambana na upinzani kuhakikisha hawapumui, nje na ndani ya bunge
Pia sayansi ya kuiba kura
Mtu anachaguliwa tu, kitu cha kwanza anaapa kuua upinzani.
Hizo ndo sayansi zetu
 
Tatizo kelele zote huwa zinaishia humu Jukwaani Wala hata nje hazifiki....
Jukwaa hili ukiandika upuuzi, kudhalilisha au kutukana wakubwa; haichukui muda unakamatwa hasa kama ID ya jina lako linafahamika.

Ni heri hata mambo ya maana kwa mustakabali wa nchi yetu kusema. Huenda anaweza kutokea mtu mwenye nia njema na fikra mbadala akashikiana nasi kwenye kuijenga Tanzania kwa kuwekeza kwa kuanza na wazawa.
 
Umesema yote mkuu.. viongozi wengi ni wapumbafu.. yaani hawafaham umuhim wa R&D.. hawajui kuwa hata hizo SGR na Rufiji zinahitaji R&D.. ili uendelvu uwepo.. utaona kuwa TZ imefeli katika projects nyingi kwa kukosa hiyo element. Unakuta kila kitu kinaongozwa kwa mihemko bila kufuata matokeo ya utafiti.. hata serikaliiliyopo ipo ipo tu. Yaani ni shida tupu na hatuwezi kuendelea kwa mtindo huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…