Dhamira au haja ya binadamu kua na kuvutiwa katika mapenzi ya jinsia yake ama ya tofauti hutegemea sana mabadiliko ya akili katika kujitambua na kujitambulisha 'Kijisia'. Mabadiliko hayo ya akili 'Kiasili' hutokea na kuathiriwa na Umri 'baadae mazingira yanafuatia'. Kila binadamu katika mabadiliko hayo ya utambuzi kijinsia katika vipindi tofauti vya ukuaji wake. Kiuchunguzi katika akili ya Ubongo wa mtoto, huanza kuhisi na kujitambua kijisia (kama yeye ni Me au Ke) akiwa na umri wa miaka 2.5-3,hapa mtoto huanza kubagua kazi na jinsia tofauti na yake,kama ni wa kiume basi atachezea 'toys' kama magari,tairi ,mipira na kuigiza kazi za akina baba, kuzibagua kazi za akina mama na watu wa jinsia tofauti na yake,Vivo hivo na mtoto wa kike nae atapenda kuchezea toys za kike,kuvaa mavazi ya kike,nk.
Mtoto akifikisha umri wa miaka 4-10,akili katika ubongo wake huanza kua na haja za kuvutiwa na watu wa jinsia ya tofauti na kuwabagua wale wa jinsia yake- hii ni asili kabla ya kipindi cha kupevuka. Endapo itatokea hitilafu yeyote katika kipindi hiki( Hitirafu za mabadiliko kiakili katika kujitambua na kujitambulisha kijinsia) basi athali zake huweza kujidhihirisha katika kipindi cha mtu kupevuka (miaka 11 na kuendelea),ambapo hua ni wakati wa kutambulisha haja au Dhamira za Mapenzi kimwili kwa jinsia ya tofauti au ile ya muhusika.
Wapo watu, mfano wanaume, asili ya akili zao kimapenzi imejengwa kuvutiwa na wanawake (Heterosexual),Wapo wanaovutiwa na wanawake pamoja wanaume ( Bisexual),Wapo ambao hawavutiwi na wa jinsia yeyote (Asexual). Tofauti hizi haja huwepo kiasili, mazingira huja kuhalisha saikolojia ya muhusika.
Bahati mbaya tathmini zote za mapenzi ya jinsia moja,hayako katika kuangalia asili ya haja kwa muhusika,bali yapo katika hoja ya uhalali na uhalisia katika utumizi wa sehemu za siri. 'Unaweza ukawa huna sehemu za Siri lakini ukawa na haja za kua na mpenzi-mpenzi wa jinsia yako au ya tofauti'. Jamii inatambua utaratibu wa mahusiano,kwa hitilafu hizi chache tunazoziita har/lau** ziangaliwe katika utaratibu maalumu,kitaalam zaidi (watu hao huitaji tiba za mmoja mmoja kisaikojia),ndio maana suala la maadili litabaki kuchukua nafasi ndogo.