Chanzo cha mabasi ya "No Challenge" kuitwa "Tashriff"

Chanzo cha mabasi ya "No Challenge" kuitwa "Tashriff"

Tanga wenda leo warudi leo

Enzi naenda Tanga kusabahi ndugu na jamaa tulikuwa tunaondoka na gari Moshi Stesheni, tunapika chakula (wali, pilau, maandazi) ya kula njiani.
Ila sasa tunajikuta chakula chote tunakula hapo stesheni kabla ya kuanza safari.

Mnaambiwa safari ni saa 12 jioni kisha mnatangaziwa imesogezwa hadi saa 2 usiku kisha saa 6 usiku kisha asubuhi alfajiri mnakuja kuondoka saa kumi jioni....😪😪😪

Na ikibidi kupanda mabasi enzi zile ilikuwa tunaondoka usiku tunashuka Muheza saa 8 hadi 10 alfajiri.....
Tunakaa kituoni hadi pakuche tunaanza kuchanja mbuga hadi kijijini.....

Enzi hizo moja ya mabasi ilikuwa Zafanana....

Kasinde Matata.
Kumbe dada wewe ni mtu wa Tanga?

Basi ndo maaaana.
 
AJALI NYINGI NI USHIRIKINA , KAFARA ZA WENYE MA BUS YAO.
kuna nyingine haikuua watu ila basi liliteketeketea lenyewe kwa moto wiki iliyopita. Assumption za kishirikina lazima ziwepo kunakotokea ajali za mabasi haya ya matajiri. Huenda wanatoa kafara kwa miungu yao inayowapa utajiri
 
Damu yangu ni mchanganyiko wa asili ya Mahabat na inakorinwa asali....😋😋😋

aka chotara wa Pwani na Bara...😊.
Mungu wangu, niozeshe basi hata binti yako na mie nipate hio radha. atakuwa mke wa pili lakini
 
Ally’s Singida juzi pia malaika Singida
huko huko singida kuna ajali mbaya sana ilitokea miaka ya nyuma, basi lilipinduka na kuwaka moto abiria wengi walipoteza maisha kiasi cha kutojulikana sura zao, walizikwa pamoja kando ya barabara ilikotokea ajali. Eneo hilo sasa hivi linaitwa kona ya mohamed kutokana na jina la basi hilo.
 
Unakuta kampuni ina mabasi mengi, moja linakuja kupata ajali mbaya, ama liteketeze watu au liteketee lenyewe. Abiria wawe wanafanya maombi kwa Mungu kuvunja nguvu za kishirikina wafike salama. Kuzembea kuomba na kuvunja nguvu za kishirikina kunapelekea kutamalaki nguvu za kishirikina na kushinda
 
Tanga wenda leo warudi leo

Enzi naenda Tanga kusabahi ndugu na jamaa tulikuwa tunaondoka na gari Moshi Stesheni, tunapika chakula (wali, pilau, maandazi) ya kula njiani.
Ila sasa tunajikuta chakula chote tunakula hapo stesheni kabla ya kuanza safari.

Mnaambiwa safari ni saa 12 jioni kisha mnatangaziwa imesogezwa hadi saa 2 usiku kisha saa 6 usiku kisha asubuhi alfajiri mnakuja kuondoka saa kumi jioni....😪😪😪

Na ikibidi kupanda mabasi enzi zile ilikuwa tunaondoka usiku tunashuka Muheza saa 8 hadi 10 alfajiri.....
Tunakaa kituoni hadi pakuche tunaanza kuchanja mbuga hadi kijijini.....

Enzi hizo moja ya mabasi ilikuwa Zafanana....

Kasinde Matata.
acheni tabia ya uongo mnapotosha vijana wenu walozaliwa baada ya huo usafiri kusitishwa. Treni ya Moshi-Dar ilikuwa inaondoka saa 04.15 jioni haijawahi kuongeza muda wala kupunguza. Treni kutoka Tanga ilikuwa inafika Korogwe, inasubiri ya kutokea Dar-Moshi, wanabadilisha mabehewa pale, tunaondokaga saa 8 hivi usiku Tanga tunafikaga alfajir saa 06.00am bila kuchelewa. Treni zilikuwa smart sana acha kupotosha watu. Nna wasiwasi we hujawahi kutumia huo usafiri.
 
Kampuni ya mabasi air shengena ilibadili jina mara 3, baada ya kupata ajali kubwa mara kwa mara zilizo sababishwa kufungiwa kwa kampuni ,. 1 air shengena ilipata ajali kwa kugongana na treni Kilimanjaro wilaya ya mwanga ,ikabadilishwa jina kuwa NO CHALLENGE, nayo ikapata ajali kubwa sana ,ikabadilishwa jina na kutumia tashiriff,Nina amini hii ndio kampuni ilio pata ajali nyingi kubwa na zisizo sahaulika tena kwa mfurulizo chini ya miaka 7.
 
Anaandika mzee Joseph Jandwa

Leo 3/5/2023 imetimia miaka 25 tangu ajali ya basi iliyosababisha vifo vya abiria 96 na majeruhi 9, ilipotokea jioni ya tar 3/5/1998. Kihistoria haijawahi kutokea ajali mbaya ya basi iliyoua watu wengi kama hiyo.

Mimi ni miongoni mwa wale 9 walionusurika kwa neema ya Mungu. Ajali hii ilihusisha basi la kampuni ya NO CHALLENGE ambayo baada ya ajali ile ilibadili jina na kujiita TASHRIFF. Ajali ilitokea Mkoani Tanga, Wilaya Muheza, kijiji cha Kibanda. Bus lililokua na namba za Usajili TZK 960 lilikuwa likitoka Tanga kuelekea DSM.

Kipindi hicho kulikuwa na mvua nyingi zilizobatizwa jina Mvua za El-Nino. Tulipofika kijijini hapo tulikuta mabasi mengi yamesimama kutokana na kujaa maji kwenye mto Msangazi. Kuanzia mabasi makubwa hadi madogo kama Coaster na Hiace. Pia zilikuwepo gari binafsi.

Kwenye kijiji cha Kibanda kuna mto uitwao Msangazi. Ulikua umejaa maji. Basi tulilopanda lilijaribu kuvuka ng'ambo ya pili ili kuendelea na safari. Baadhi ya abiria wa mabasi mengine walidandia basi letu ili wavuke kuendelea na ratiba zao. Lakini halikuweza kufika ng'ambo. Lilisombwa na maji. Likasukumwa mtoni na kuzama kabisa.

Watu 96 wakapoteza maisha, wakiwemo wale waliodandia. Sehemu kubwa ya abiria walifia ndani ya basi kwa kushindwa kutoka. Wachache walioweza kutokea madirishani walikufa kutokana na kusombwa na maji yenye kasi ya mto huo. Ilikua simanzi kubwa.

Pamejengwa mnara wa kumbukumbu ya wafu na majina yao. Lakini naambiwa vijana wa vyuma chakavu walishakwanyua kibao kilichokuwa kimeorodhesha majina ya wafu 72 waliotambulika na wengine 24 ambao hawakutambuliwa.

Katika wale 9 tuliosalimika, mmoja wao ni Mzee Ramadhani Kimbunga aliyekuwa Dereva wa basi hilo. Bahati mbaya pamoja na kuokoka kwenye ajali hiyo alikuja kufa miezi michache baadae kwa kifo cha kawaida. Manusura wengine wawili nao walishafariki kwa nyakati tofauti, na tuliosalia hai mpaka sasa ni 6 tu.

Baada ya ajali hiyo kampuni ya NO CHALLENGE ikabadili jina na kujiita TASHRIFF kwa sababu Challenge imeshatokea. Nimeona niwakumbushe maana wengi wamesahau. Na tuliosalimika ili kusimulia tumebaki 6 tu. Tujifunze kupitia kisa hiki ili kuepusha ajali nyingine za aina hii.

View attachment 2608991
Asante sana pole na hongera kwa kusalimika ajali ile na kuwa hai hata leo.. Wazungu wana usemi wao LEFT TO TELL
Kinachoniumiza kila nikipita pale mahali ni wizi wa lile bango lililokuwa limeandikwa majina yote 96 ya marehemu na serikali kushindwa kutengeneza lingine
Pale mahali pana simulizi nyingi za kutisha kama
Kuona watu wengi wakiogelea
Kuona watu wakizama
Kuna boat imefurika watu nknk
 
Mama yangu Mkubwa alikuwepo na alinusurika na hadi leo yupo,yeye kilichomukoa aliung'ang'ania mnazi juu kabisa karibia na matawi yake
Mkuu unataka kusema bus lililazimisha kupita maji yakiwa mengi kimo cha mnazi au??
 
Back
Top Bottom