Chanzo cha mabasi ya "No Challenge" kuitwa "Tashriff"

Chanzo cha mabasi ya "No Challenge" kuitwa "Tashriff"

Heb

Pole Dana mzee.hebu tukumbushie na air msae mpaka kubadilishwa kuwa Kilimanjaro bus nasikia nayo ilizama mtoni 1998 Enzo za elnino.anaejua hii taarifa atupe mkanda mzma
Air Msae zilikuwa zinamilikiwa na Wilbard Mtenga alibadilisha jina na kuziita Metro Coach, hazijawahi kuitwa Kilimanjaro
 
Shusheni ajali hasa za mohamed trans aa ile basi zilikuwa zinauwa nyie
 
Wewe umekuta maji yamekatiza barabara pressure ya hatari wenye akili wamepaki wanasubiri wewe unapeleka pua yako unaua watu 96 kwenye maji alafu unarudi kisema ni kafara....Ujinga ni mzigo
Mkuu anayesema kafara sio dereva aliyepeleka gari au mmiliki wa gari. Wanaosema hivyo ni mashuhuda wa ajali hiyo au watu waliopata taarifa za ajali. Wanashangaa inakuwaje mtu mwenye akili alipeleke gari kwenye maji ilhali amekuta wenzake wamepark kusubiri maji yapungue?? Ndio hapo linakuja jibu kuwa alitaka kwa makusudi kutoa watu kafara
 
huko huko singida kuna ajali mbaya sana ilitokea miaka ya nyuma, basi lilipinduka na kuwaka moto abiria wengi walipoteza maisha kiasi cha kutojulikana sura zao, walizikwa pamoja kando ya barabara ilikotokea ajali. Eneo hilo sasa hivi linaitwa kona ya mohamed kutokana na jina la basi hilo.
Yap nakumbuka hii kama siyo 2006 ni 2007, alifariki pia rafiki yake dada yangu aliitwa Restuta alikuwa anatokea Arusha kwenda kwao Singida[emoji854]
 
Mkuu anayesema kafara sio dereva aliyepeleka gari au mmiliki wa gari. Wanaosema hivyo ni mashuhuda wa ajali hiyo au watu waliopata taarifa za ajali. Wanashangaa inakuwaje mtu mwenye akili alipeleke gari kwenye maji ilhali amekuta wenzake wamepark kusubiri maji yapungue?? Ndio hapo linakuja jibu kuwa alitaka kwa makusudi kutoa watu kafara
Uzembe barabarani ndio chanzo cha ajali nyingi, haya makafara ni mitazamo tu ya watu wavivu wa kufikiri. Mfano mwaka huu tu pekee kuna magari kibao yamesombwa na maji na kuua watu sababu ya madereva kupuuza nguvu ya maji.

Ajali zitapungua sana kama uzembe utapungua na umakini kuongezeka, otherwise tutegemee madereva wapuuzi wakimaliza vyombo na watu huku uma ukihangaika na tuhuma za kafala.
 
Mkuu, kama ulivyosema, ni mitazamo ya watu. Kila mtu ana uhuru wa kukiona kitu kwa mtazamo autakao. Wewe unayeamini kuwa sababu ya vifo ni uzembe upo sawa kwa mtazamo wako na wanaoamini kuwa sababu ni kutoa kafara wapo sawa kwa mtazamo wao.
 
Anaandika mzee Joseph Jandwa

Leo 3/5/2023 imetimia miaka 25 tangu ajali ya basi iliyosababisha vifo vya abiria 96 na majeruhi 9, ilipotokea jioni ya tar 3/5/1998. Kihistoria haijawahi kutokea ajali mbaya ya basi iliyoua watu wengi kama hiyo.

Mimi ni miongoni mwa wale 9 walionusurika kwa neema ya Mungu. Ajali hii ilihusisha basi la kampuni ya NO CHALLENGE ambayo baada ya ajali ile ilibadili jina na kujiita TASHRIFF. Ajali ilitokea Mkoani Tanga, Wilaya Muheza, kijiji cha Kibanda. Bus lililokua na namba za Usajili TZK 960 lilikuwa likitoka Tanga kuelekea DSM.

Kipindi hicho kulikuwa na mvua nyingi zilizobatizwa jina Mvua za El-Nino. Tulipofika kijijini hapo tulikuta mabasi mengi yamesimama kutokana na kujaa maji kwenye mto Msangazi. Kuanzia mabasi makubwa hadi madogo kama Coaster na Hiace. Pia zilikuwepo gari binafsi.

Kwenye kijiji cha Kibanda kuna mto uitwao Msangazi. Ulikua umejaa maji. Basi tulilopanda lilijaribu kuvuka ng'ambo ya pili ili kuendelea na safari. Baadhi ya abiria wa mabasi mengine walidandia basi letu ili wavuke kuendelea na ratiba zao. Lakini halikuweza kufika ng'ambo. Lilisombwa na maji. Likasukumwa mtoni na kuzama kabisa.

Watu 96 wakapoteza maisha, wakiwemo wale waliodandia. Sehemu kubwa ya abiria walifia ndani ya basi kwa kushindwa kutoka. Wachache walioweza kutokea madirishani walikufa kutokana na kusombwa na maji yenye kasi ya mto huo. Ilikua simanzi kubwa.

Pamejengwa mnara wa kumbukumbu ya wafu na majina yao. Lakini naambiwa vijana wa vyuma chakavu walishakwanyua kibao kilichokuwa kimeorodhesha majina ya wafu 72 waliotambulika na wengine 24 ambao hawakutambuliwa.

Katika wale 9 tuliosalimika, mmoja wao ni Mzee Ramadhani Kimbunga aliyekuwa Dereva wa basi hilo. Bahati mbaya pamoja na kuokoka kwenye ajali hiyo alikuja kufa miezi michache baadae kwa kifo cha kawaida. Manusura wengine wawili nao walishafariki kwa nyakati tofauti, na tuliosalia hai mpaka sasa ni 6 tu.

Baada ya ajali hiyo kampuni ya NO CHALLENGE ikabadili jina na kujiita TASHRIFF kwa sababu Challenge imeshatokea. Nimeona niwakumbushe maana wengi wamesahau. Na tuliosalimika ili kusimulia tumebaki 6 tu. Tujifunze kupitia kisa hiki ili kuepusha ajali nyingine za aina hii.

View attachment 2608991
Mkuu unaweza kutuelezea ulijinusuru vipi? Maana umesema maji yalikuwa na kasi, na mto umejaa sana.

Na je, wakati bus linajaribu kuvuka, hakuna abiria waliojaribu kuzuia?
 
kuna nyingine haikuua watu ila basi liliteketeketea lenyewe kwa moto wiki iliyopita. Assumption za kishirikina lazima ziwepo kunakotokea ajali za mabasi haya ya matajiri. Huenda wanatoa kafara kwa miungu yao inayowapa utajiri
Sio kila kitu ushirikina kwani hajari duniani hakuna?
 
Unakuta kampuni ina mabasi mengi, moja linakuja kupata ajali mbaya, ama liteketeze watu au liteketee lenyewe. Abiria wawe wanafanya maombi kwa Mungu kuvunja nguvu za kishirikina wafike salama. Kuzembea kuomba na kuvunja nguvu za kishirikina kunapelekea kutamalaki nguvu za kishirikina na kushinda
Hajari zipo na ushirikina hupo kazi kutambua hajari ya ushirikina
 
Mkuu, kama ulivyosema, ni mitazamo ya watu. Kila mtu ana uhuru wa kukiona kitu kwa mtazamo autakao. Wewe unayeamini kuwa sababu ya vifo ni uzembe upo sawa kwa mtazamo wako na wanaoamini kuwa sababu ni kutoa kafara wapo sawa kwa mtazamo wao.
NO CAP
 
Kuna ile waligonga gari ya nguzo za Tanesco na zile nguzo zinakapita kweny kioo kwa mbele usawa wa siti kama walovyojipanga kweny column walikufa vibaya watu walikatwa vichwa..
Bus gani mkuu?
 
Naam, na Ile ndio ikawafanya wabadili Jina
Actually haya Magari Zamani yalikuwa yanaitwa Air Shengena
Kwa hiyo ni kusema buses za Tashrif zina matukio mawili makubwa yaliyosababisha vifo hadi kubadili majina ili wasikimbiwe na abiria?
 
Back
Top Bottom