Chanzo cha mabasi ya "No Challenge" kuitwa "Tashriff"

Chanzo cha mabasi ya "No Challenge" kuitwa "Tashriff"

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
828
Reaction score
2,110
Anaandika mzee Joseph Jandwa

Leo 3/5/2023 imetimia miaka 25 tangu ajali ya basi iliyosababisha vifo vya abiria 96 na majeruhi 9, ilipotokea jioni ya tar 3/5/1998. Kihistoria haijawahi kutokea ajali mbaya ya basi iliyoua watu wengi kama hiyo.

Mimi ni miongoni mwa wale 9 walionusurika kwa neema ya Mungu. Ajali hii ilihusisha basi la kampuni ya NO CHALLENGE ambayo baada ya ajali ile ilibadili jina na kujiita TASHRIFF. Ajali ilitokea Mkoani Tanga, Wilaya Muheza, kijiji cha Kibanda. Bus lililokua na namba za Usajili TZK 960 lilikuwa likitoka Tanga kuelekea DSM.

Kipindi hicho kulikuwa na mvua nyingi zilizobatizwa jina Mvua za El-Nino. Tulipofika kijijini hapo tulikuta mabasi mengi yamesimama kutokana na kujaa maji kwenye mto Msangazi. Kuanzia mabasi makubwa hadi madogo kama Coaster na Hiace. Pia zilikuwepo gari binafsi.

Kwenye kijiji cha Kibanda kuna mto uitwao Msangazi. Ulikua umejaa maji. Basi tulilopanda lilijaribu kuvuka ng'ambo ya pili ili kuendelea na safari. Baadhi ya abiria wa mabasi mengine walidandia basi letu ili wavuke kuendelea na ratiba zao. Lakini halikuweza kufika ng'ambo. Lilisombwa na maji. Likasukumwa mtoni na kuzama kabisa.

Watu 96 wakapoteza maisha, wakiwemo wale waliodandia. Sehemu kubwa ya abiria walifia ndani ya basi kwa kushindwa kutoka. Wachache walioweza kutokea madirishani walikufa kutokana na kusombwa na maji yenye kasi ya mto huo. Ilikua simanzi kubwa.

Pamejengwa mnara wa kumbukumbu ya wafu na majina yao. Lakini naambiwa vijana wa vyuma chakavu walishakwanyua kibao kilichokuwa kimeorodhesha majina ya wafu 72 waliotambulika na wengine 24 ambao hawakutambuliwa.

Katika wale 9 tuliosalimika, mmoja wao ni Mzee Ramadhani Kimbunga aliyekuwa Dereva wa basi hilo. Bahati mbaya pamoja na kuokoka kwenye ajali hiyo alikuja kufa miezi michache baadae kwa kifo cha kawaida. Manusura wengine wawili nao walishafariki kwa nyakati tofauti, na tuliosalia hai mpaka sasa ni 6 tu.

Baada ya ajali hiyo kampuni ya NO CHALLENGE ikabadili jina na kujiita TASHRIFF kwa sababu Challenge imeshatokea. Nimeona niwakumbushe maana wengi wamesahau. Na tuliosalimika ili kusimulia tumebaki 6 tu. Tujifunze kupitia kisa hiki ili kuepusha ajali nyingine za aina hii.

FB_IMG_1683147475471.jpg
 
Anaandika mzee Joseph Jandwa

Leo 3/5/2023 imetimia miaka 25 tangu ajali ya basi iliyosababisha vifo vya abiria 96 na majeruhi 9, ilipotokea jioni ya tar 3/5/1998. Kihistoria haijawahi kutokea ajali mbaya ya basi iliyoua watu wengi kama hiyo.

Mimi ni miongoni mwa wale 9 walionusurika kwa neema ya Mungu. Ajali hii ilihusisha basi la kampuni ya NO CHALLENGE ambayo baada ya ajali ile ilibadili jina na kujiita TASHRIFF. Ajali ilitokea Mkoani Tanga, Wilaya Muheza, kijiji cha Kibanda. Bus lililokua na namba za Usajili TZK 960 lilikuwa likitoka Tanga kuelekea DSM.

Kipindi hicho kulikuwa na mvua nyingi zilizobatizwa jina Mvua za El-Nino. Tulipofika kijijini hapo tulikuta mabasi mengi
Asante sana mkuu
 
Eeeeh kumbe..!!
Asante kwa taarifa
Nakumbuka hii ajari ilikuwa mbaya sana, Nakumbuka kuna mama alikuwa kabeba mtoto mgongoni gari ilivyo kuwa inazama alijitahidi kun'ga n'gania mnazi ulikuwa karibu lakini mnazi ulianguka na mama na mtoto walitumbukia mtoni ...[emoji24] inasikitisha sana....watu wengi sana walipoteza maisha.....
 
Na Ile Ajali nyingine ya kuparamiwa na nguzo za Tanesco, watu kutobolewa kama mishkak
Walibadili Jina Kwa sababu za Kishirikina ilisemekana
Kuna ile waligonga gari ya nguzo za Tanesco na zile nguzo zinakapita kweny kioo kwa mbele usawa wa siti kama walovyojipanga kweny column walikufa vibaya watu walikatwa vichwa..
 
Tanga wenda leo warudi leo

Enzi naenda Tanga kusabahi ndugu na jamaa tulikuwa tunaondoka na gari Moshi Stesheni, tunapika chakula (wali, pilau, maandazi) ya kula njiani.
Ila sasa tunajikuta chakula chote tunakula hapo stesheni kabla ya kuanza safari.

Mnaambiwa safari ni saa 12 jioni kisha mnatangaziwa imesogezwa hadi saa 2 usiku kisha saa 6 usiku kisha asubuhi alfajiri mnakuja kuondoka saa kumi jioni....😪😪😪

Na ikibidi kupanda mabasi enzi zile ilikuwa tunaondoka usiku tunashuka Muheza saa 8 hadi 10 alfajiri.....
Tunakaa kituoni hadi pakuche tunaanza kuchanja mbuga hadi kijijini.....

Enzi hizo moja ya mabasi ilikuwa Zafanana....

Kasinde Matata.
 
Tanga wenda leo warudi leo

Enzi naenda Tanga kusabahi ndugu na jamaa tulikuwa tunaondoka na gari Moshi Stesheni, tunapika chakula (wali, pilau, maandazi) ya kula njiani.
Ila sasa tunajikuta chakula chote tunakula hapo stesheni kabla ya kuanza safari.

Mnaambiwa safari ni saa 12 jioni kisha mnatangaziwa imesogezwa hadi saa 2 usiku kisha saa 6 usiku kisha asubuhi alfajiri mnakuja kuondoka saa kumi jioni....[emoji25][emoji25][emoji25]

Na ikibidi kupanda mabasi enzi zile ilikuwa tunaondoka usiku tunashuka Muheza saa 8 hadi 10 alfajiri.....
Tunakaa kituoni hadi pakuche tunaanza kuchanja mbuga hadi kijijini.....

Enzi hizo moja ya mabasi ilikuwa Zafanana....

Kasinde Matata.
Mauzauza hayajaanza sasa Tz, na hayatakwisha! Mnakaa kituo cha garimoshi siku mbili?!!
 
Mauzauza hayajaanza sasa Tz, na hayatakwisha! Mnakaa kituo cha garimoshi siku mbili?!!

Na hiyo ilikuwa kawaida kabisa....

Na hakuna abiria kupewa mablanketi mjifunike usiku, wala maji ya kunywa...

Unaambiwa ukiondoka kurudi nyumbani hjku nyuma gari Moshi ikitengemaa ikaondoka imekula kwako....

Ukiwaza hiyo hela ya nauli kuipata tena unakuwa mpole tuu unasugua gaga Stesheni hadi safari iive.....🙁.
 
Back
Top Bottom