#COVID19 Chanjo za Corona ni salama na thabiti kiasi gani kutumika na binadamu?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,681
46,362
Yapo mengi yamesemwa kuhusu usalama Chanjo za Corona, tunaendela kushuhudia hata watu wasio na ujuzi wowote wa tiba na sayansi ya madawa wakiwa mstari wa mbele kuonyesha madhara ya chanjo. Lakini ni vyema tufahamu.

1. Chanjo za COVID-19 ni SALAMA na zimefanyiwa majaribio ya kutosha ya usalama wake.

2.Chanjo za Covid zote za Marekani, Ulaya, Russia na China HAZIGUSI DNA kabisa, zote ni kwa ajili ya mRNA. Hizi chanjo hazitabadilisha DNA yako kwa namna yoyote.

3.Chanjo za COVID-19 zimewahi kutengezewa kwa sababu ya maendeleo makubwa ya teknolojia ya tiba na madawa katika karne ya 21 na ufadhili mkubwa wa haraka wa kifedha.

4.Sio kweli kwamba hata Chanjo nyingine amabazo zilifanyiwa majaribio ya muda mrefu ziliwahi kuleta madhara makubwa.

5.Mashirika yanayohusika na udhibiti wa chanjo yamezipa kibali cha haraka baada ya kuridhika ni salama kabisa.

6.Wapinga chanjo(Anti vaxxers) wamekuwepo katika chanjo zozote zilizowahi kutengenezwa, hawa wa sasa wana faida kubwa ya maendeleo ya teknolojia ya habari kueneza uvumi wao.

7. Ukiumwa unakimbilia hospitali kucheki afya yako na unamuamini daktari anajua au atajua tatizo lako. Hauendi kwa Gwajima, padri au wanasiasa, fanya hivyo kwa Covid pia. Sikiliza na fuata madaktari na wataalamu wa virusi wanachosema.

 
ASANTE KWA TAARIFA NZURI MKUU NIMEPENDA HAPO MBONA MTU AKIUMWA ANAKWENDA KUMEZA DAWA ZILIZOLETWA NA WAZUNGU NA SIO KWENDA KWA GWAJIMA
 
Back
Top Bottom