Chanjo au majaribio ya dawa ya COVID-19 (Clinical Trial )

Chanjo au majaribio ya dawa ya COVID-19 (Clinical Trial )

Ni nani PFizer .
Mwaka 1996 katika Jimbo la Kano nchini Nigeria ulizuka ugonjwa wa "Menengetics" haraka kampuni ya PFizer ikatengeneza dawa na Kisha hatua ya majaribio ya dawa hio(Clinical Trials) wakaenda kuifanya kwa watoto nchini Nigeria huko Kano.
Jambo hili lilipelekea watoto kadhaa kupoteza maisha na kesi hii kupelekwa mahakamani.
Ni Mwaka 2009 PFizer ikaomba kesi ifanyike nje ya Mahakama na kulipa Jimbo la Kano dola za kimarekani milioni 75 na familia za watoto waliopoteza maisha(watoto 4) dola za marekani 175,000.
Naam na huo ndio uzuri wa Kampuni kama hizi ambazo zipo accountable, zikifanya kosa zinabanwa na sheria na zinatoa pesa; tofauti na wengine hilo likitokea malipo hampati na data zinakuwa cooked.

Unategemea mrusi (taifa) au mchina (taifa) litakubali kwamba kuna makosa / uzembe ulifanyika?

Big companies are after profit na bad publicity inaweza kuua kampuni (thus they try to be careful uzembe haufanyiki)
 
Mkuu,

Hiyo chanjo ya Pfizer mimi nimechanjwa pamoja na raia wa Marekani wengi sana.

Kituo nilichopiga chanjo mimi walikuwa wanachanjwa watu takriban 14,000 kwa siku. Unafanya appointment online, unaenda kuchanjwa.

Wakati mimi nachanjwa, takriban watu wa Marekani milioni mbili kwa siku nchi nzima walikuwa wanachanjwa.

Kuna states karibu robo ya watu washapata chanjo.

Soma hapa kwa habari zaidi

Rais Biden kasema anataka kila mtu aliye Marekani anayetaka kuchanjwa awe amechanjwa by May.

Unataka kusema nini?

Marekani inataka kuua watu wake pia?
Kajazwa ujinga na bosi wake.

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
 
Ulaya kundi la kwanza kupata chanjo ni madaktari na wauguzi, chanjo ni moderna ná Pfizer. Kweli wazungu wanania ya kuua wauguzi na madaktari wao? Kundi la pili ni wazee wan wenye magonjwa sugu. Kati yao wabunge na maofisa wa serikali wamo.
Mim nataka niseme hivi yawezekana mashaka haya yawepo aulaa ila kwa nnavyojua mim dawa ya marekani inautofauti mkubwa sana katk ubora ukiachia mbali hii itakayosemwa inatolewa kwa Africa, vitu vya America ni special kwa. Waamerika
 
Naam na huo ndio uzuri wa Kampuni kama hizi ambazo zipo accountable..., zikifanya kosa zinabanwa na sheria na zinatoa pesa; tofauti na wengine hilo likitokea malipo hampati na data zinakuwa cooked....

Unategemea mrusi (taifa) au mchina (taifa) litakubali kwamba kuna makosa / uzembe ulifanyika ?

Big companies are after profit na bad publicity inaweza kuua kampuni (thus they try to be careful uzembe haufanyiki)
Anakwambia watoto waliopoteza maisha ni wanne, lakini hakwambii waliochanjwa ni wangapi. Na kati ya hao waliochanjwa, wangapi maisha yao yameokolewa kutokana na chanjo.

Ridiculous.
 
Ulipo muhusisha jiwe kwenye huu uzi ndipo nilipogundua uwezo wako wa kufikiri. Naweza sema mko sawa yani wew na Jiwe
Shukurani mkuu kwa kunipaisha sikujua kama nipo level ya jiwe
 
Naam na huo ndio uzuri wa Kampuni kama hizi ambazo zipo accountable..., zikifanya kosa zinabanwa na sheria na zinatoa pesa; tofauti na wengine hilo likitokea malipo hampati na data zinakuwa cooked....

Unategemea mrusi (taifa) au mchina (taifa) litakubali kwamba kuna makosa / uzembe ulifanyika ?

Big companies are after profit na bad publicity inaweza kuua kampuni (thus they try to be careful uzembe haufanyiki)
kweli mkuu
 
Mkuu,

Hiyo chanjo ya Pfizer mimi nimechanjwa pamoja na raia wa Marekani wengi sana.

Kituo nilichopiga chanjo mimi walikuwa wanachanjwa watu takriban 14,000 kwa siku. Unafanya appointment online, unaenda kuchanjwa.

Wakati mimi nachanjwa, takriban watu wa Marekani milioni mbili kwa siku nchi nzima walikuwa wanachanjwa.

Kuna states karibu robo ya watu washapata chanjo.

Soma hapa kwa habari zaidi

Rais Biden kasema anataka kila mtu aliye Marekani anayetaka kuchanjwa awe amechanjwa by May.

Unataka kusema nini?

Marekani inataka kuua watu wake pia?
Noma kweli mkuu
Wewe si level yetu
 
Hujui kwamba hiyo chanjo imetolewa kwa matumizi ya dharura, an experimental vaccine approved for emergency use. Kwa hiyo wewe na hao vilaza wa kimarekani mmekubali kuwa panya wa majaribio..
 
Ogopa USA ni taifa linaishi kwa siri nyingi.unaweza ukawa ulichanjwa pamoja na wamarekani ,lakini ukawa umechanjwa chanjo tofauti na wao,japo mlikuwa site moja ya uchanjaji,na pengine foleni moja.kwanza uliomba chanjo online,hivyo hapo kirahisi wanakujua wewe ni Nani,na detail zako zingine,hivyo kirahiiiisi wanakuandalia mzigo wako binafsi mapemaaa wa chanjo.hongera mkuu kwa kuchanja Ila next time u have to take extra care.hizi chanjo zina confusion nyingi ambazo hata wao(makampuni yanayotengeneza+WHO) Wamepiga kimya kutolea majibu.
 
Noma kweli
 
Ulaya kundi la kwanza kupata chanjo ni madaktari na wauguzi, chanjo ni moderna ná Pfizer. Kweli wazungu wanania ya kuua wauguzi na madaktari wao? Kundi la pili ni wazee wan wenye magonjwa sugu. Kati yao wabunge na maofisa wa serikali wamo.
Shida iliyopo wanaweza kuleta chanjo isiyokuwa hiyo (moderna & pfizer)--- Mzungu akiwa mwema huwa mwema hasa na akiwa shetani huwa shetani hasa, tufikirie pia inawezekana ukawepo mpango wa kishetani wa kuangamiza watu weusi ili tutakapo malizika baadaye waje ku take over Africa, wazungu walianza kulipenda bara letu kitambo sana.

Kifupi ni kwamba kuna mpango wa kuangamiza au kutufanya Guinea pigs waafrika kupitia njia mbalimbali ikiwemo njia ya vaccination, jambo kama hilo limewahi kutokea Nigeria, Sieraleone na India.

Sipingi chanjo lakini lazima tuwewaangalifu na hizo chanjo kutoka America, Chanjo zisizokuwa na mashaka ni Sputnik na Sinovac za Russia na China.
 
Hatari mzee
 
Ogopa USA ni taifa linaishi kwa siri nyingi.unaweza ukawa ulichanjwa pamoja na wamarekani ,lakini ukawa umechanjwa chanjo tofauti na wao,japo mlikuwa site moja ya uchanjaji,na pengine foleni moja.kwanza uliomba chanjo online,hivyo hapo kirahisi wanakujua wewe ni Nani,na detail zako zingine,hivyo kirahiiiisi wanakuandalia mzigo wako binafsi mapemaaa wa chanjo.hongera mkuu kwa kuchanja Ila next time u have to take extra care.hizi chanjo zina confusion nyingi ambazo hata wao(makampuni yanayotengeneza+WHO) Wamepiga kimya kutolea majibu.
100000% Very true---- you have spoken the truth.
 
Wewe huna chanjo yoyote?

Hii ni conspiracy theory ambayo haina msingi wowote.

Halafu sitashangaa kusikia mtu anayepinga chanjo hivyo, anavaa mitumba moaka chupi, dawa za kuafisha maji, madawa, chakula etc anategemea za kutoka nje.

Weka ushahidi wa fact hapa kwamba Wamarekani wanawachanja vibaya watu, usipige hadithi za uharo wa conspiracy theory tu.
 
SAYANSI YA CHANJO KWA LUGHA RAHISI NA MASHAKA YAKE:-

Nitajaribu kuieleza sayansi hii kwa njia na lugha nyepesi ili jamii ipate mwanga suala hili ambalo kisayansi ni complex. Lengo ni kuelimishana ili kupunguza mihemuko na mivurugano tunayoishuhudia kwa sasa hasa kwa baadhi ya wanasiasa na viongozi mbali mbali wa kijamii na wenye taaluma ya habari.
Atakayeweza kusoma nakala hii ndefu anakaribishwa.

1. Nitaanza na vinasaba (genes):
Miili ya viumbe hai ina undwa na chembe chembe ndogo sana zinazoitwa seli (cells). Binadamu ana matrillion ya seli. Seli hizi zinafanya kazi mbali mbali za kuwesha kuishi (metabolism). Kila seli ina nukleasi iliyozungukwa na saitoplasm. Kwenye nukleas kuna molecules za Deoxyriboncleic acid - kifupi chake DNA. Kila seli ya binadamu ina DNA zipatazo billion 3 zilizobebwa kwenye mikufu (chromosomes) 46 ndani ya nukleas.

Taarifa zote za jinsi miili yetu inavyojengeka na kufanya kazi inabebwa kwenye hizo DNA. Kazi zote za miili yetu inafanyika kwenye saitoplasm ya seli zetu. Yaani kwenye saitoplasm ndiko kwenye viwanda mbali mbali vya kuiwezesha miili yetu iishi na kufanya kazi zote vizuri.
Kazi zote zinazofanyika kwenye kwenye saitoplasm zinafanyika kwa maelekezo na usimamizi wa DNA. Ili DNA iweze kusimamia kazi inayofanyika kwenye saitoplasm huwa inatengeneza molecule ya Ribonucleic acid - kwa kifupi RNA na kuituma huko kwenye saitoplasm kwenda kusimamia kazi husika. Hivyo inaitwa messenger RNA - kwa ufupi mRNA.

DNA ilivyumbuliwa mwaka 1953. Huu ulikuwa ni uvumbuzi wa siri ya maisha kwani siri zote za uhai na jinsi kila seli ya mwili inavyofanya kazi zimebebwa kwenye DNA. Baada ya sayansi mpya ya uhandisi wa vinasaba (genetical engineering) kuendelea (advance), kwa kipindi cha miaka 13 kuanzia mwaka 1990 hadi 2003 wanasayansi toka sehemu mbali mbali duniani walifanikiwa kuzing'amua (decode) siri zote za DNA zote billion tatu zilizoko kwenye seli za mwili wa binadamu. The entire human genetic code was decoded/ revealed. Ziko kwenye ving'amuzi vya maabara mbali mbali za uhandisi wa vinasaba.

Kuanzia hapo wanasayansi wameendelea kucheza na hizo vinasaba vya DNA ili kuweza kuangamiza baadhi ya magonjwa kwenye seli za binadamu hususani ya saratani kama ya kongosho (pancreas cancer) na ya baadhi ya virusi kama virusi vya Zika vilivyogundulika huko Uganda mwaka 1947 kwenye msitu wa Zita vikienezwa na mbu Aedes.
Pamoja na kuonesha matokeo mazuri sana katika tiba za maradhi haya, hadi sasa kwa kipindi cha mwongo mmoja mamlaka za FDAs zilishindwa kuzipa kibali tafiti hizi kuendelea na phase 2 ya clinical trials za watu wengi zaidi. Wasi wasi ukiwa ni athari ya muda mrefu ambayo inaweza kutokea kwenye vinasaba (DNA) ya seli ya binadamu.

2. Virusi ni vitu gani:
Virusi ni vimifuko ya vipande vidogo sana ya vinasaba (genes). Kuna virusi ambavyo genetic material yake ni DNA tupu na zingine ambazo ni za RNA tupu. Kirusi cha ukimwi ni cha RNA chenye genetic code 9 tu. Kirusi cha coronavirus nacho ni cha RNA na kina genetic codes 56.

Seli ya kirusi haina saitoplasm. Yaani hizo RNA au DNA zake zimehifadhiwa kwenye gamba (envelope) la protein. Kwa coronavirus gamba hili la protein ni la duara lenye miiba midogo midogo mingi (spike protein). Maji ya sabuni (soapy water) huweza kulisambaratisha (denature) gamba hili kwa urahisi na kukiua kirusi hiki. Ndiyo sababu ya kuwashauri watu kunawa mikono yao kwa sabuni mara kwa mara. Pia joto la nyuzi 45 hadi 56 C kwenye mazingira ya unyevunyevu huweza kulisarambaratisha gamba hili. Hii nayo ndiyo sababu ya tafiti mbali mbali duniani ambazo zimeweza kuonesha faida ya steam inhalation therapy ambao kwetu tunaita kujifukuzia.

Kwa kuwa virusi havina saitoplasm ili viweze kuzaliana zinahitaji kuingia kwenye seli za kiumbe kingine chenye saitoplasm. Hivyo zinaingia kwenye seli ya binadamu kwa lengo la kwenda kuzaliana. Kikishaingia kwenye seli ya binadamu genes ya virusi hivi huchukua kamandi ya maelekezo na usimamizi wa viwanda vya saitoplasm. Vinaamurishwa kufanya kazi ya kuzalisha virusi tu. Kazi zingine zinasitishwa. Hivyo seli zizovamiwa na virusi hivi zinageuzwa kuwa viwanda vya kufyatua virusi tu na vikishafyatuliwa vinavyamia seli zingine. Seli za askari wa mwili (immune cells - B lymhocytes, T lymphocytes, macrophages, Killer cells, cd4 cells etc) zinaingia vitani ambayo matokeo yake ni kifo au kupona.

3. Chimbuko la chanjo za SARS-CoV-2
Baada ya mlipuko mkubwa wa SARS (kiswahili chake Changamoto la Upumuaji) wa kirusi cha CoV-2 au coronavirus wa pili huko Wuhen, China mwezi Nov 2019 wahandisi mahiri wa vinasaba waliingia kazini kumchakata huyu kirusi. Hadi March 2020 wakawa wameweza ku decode the entire genetic code ya kiumbe hiki kidogo ambacho hadi wakati huo hakuna aliyekuwa anazijua hapa duniani. Mchina angeweza kukaa na king'amuzi hicho kwa siri peke yake maana ilikuwa ni uvumbuzi mkubwa wa siri ya maisha ya kirusi hiki. Lakini kwa upendo wa kipekee aliamua kuwasambazia bure maabara zote kubwa za genetic engineering ulimwenguni. Maabara hizi zilipokea kwa furaha ving'amuzi hivi na mara moja kuanza kucheza na vinasaba za kirusi hiki ili kupata dawa au chanjo ya kumwangamiza. Bahati mbaya au nzuri zilijielekeza zaidi kwenye genetic code ya gamba la mdudu huyu - the spike protein genome. Ziliona hapo ndipo rahisi kummaliza mdudu huyu. Clinical trials zikafanyika haraka haraka. Ilikuwa ni fursa kwa tafiti zao za tiba kwa njia ya vinasaba zilizokuwa zimekwamishwa na FDAs zao kwa miaka mingi sasa kupewa ruhusa angalao ya dharura. Hadi kufikia December 2020 zikawa zimepata hiyo emergency approval na kuanza mass vaccination ya watu wote duniani kama phase IV clinical trial.

Cha kushangaza Mchina ambaye ugunduzi wake wa vinasaba ndiyo ulipelekea utengenezaji wa hizo chanjo, yeye chanjo yake haikutumia teknolojia hiyo. Yeye chanjo yake inatumia kirusi chote (the whole virus with its entire structure including the entire genome intact) kilichopunguzwa makali kama ambavyo zilivyo chanjo za magonjwa mengine tulizozizoea.

Chanjo hizi za wengine ni kama ifuatavyo:

- Pfizer na Modern: Hizi saitoplasma ya seli za binadamu inaingiziwa mRNA kuiamuru izalishe magamba (spike proteins) ya virus vya corona. Unapata kinga dhidi ya magamba yake na hivyo hataweza kuingia tena mwilini mwako kama ataendelea kubaki na gamba lile lile. Ndani ya muda mfupi imeonekana kwamba gamba la kirusi hiki ni kama la kinyonga. Hujibadilisha mara kwa mara kutegemea na mazingira. Kwa muda mfupi zaidi ya aina 7 ya magamba haya yamegundulika - kuna South Africa variant, UK variant, Brazil variant, na majuzi Kenya variant na kadhalika.
Chanjo hizi za mRNA ni ngumu kuzitunza kwani zinahitaji ubaridi wa -20 C kwa Moderna na -70 C kwa Pfizer.

- Johnson & Johson, AstraZeneca na Gamaleya (Spunik V from Russia):
Ili kutatua tatizo la uhifadhi, chanjo hizi zinatumia DNA adenoviruses zilizofanyiwa engineering kubeba ndani yake gene ya spike protein ya CoV-2. Tofauti kati yake ni aina za hizo adenovirus zilizotumika kama kibebeo. Ile ya Astra Zeneca inatumia kirusi cha mafua ya sokwe (chimpanzee flue virus). Ile ya Urusi ina viral vector mbili (Ad26 na Ad5). Ile ya J & J ina viral vector Ad26.

- Efficacy ya chanjo hizi kwa matokeo ya phase III clinical trials: Moderna 94%, Pfizer 95%, Gamaleya 91.4%, AstraZeneca 62%, Johnson & Johnson 62%.

4. Coverage ya chanjo huko ughaibuni:
Zoezi la chanjo huko ughaibuni na america lilianza mwanzoni mwa mwezi December 2020. Lilienga kuanza kwa wale waliokwenye hatari zaidi ya kupoteza maisha kwa gonjwa hili ambao ni wanaohudumia wagonjwa hawa mahospitalini, wazee wenye umri zaidi ya miaka 70 na wenye magonjwa hatarishi km kisukari, magonjwa ya moyo au figo au maini, saratani na ukimwi.

Hadi kufikia tarehe 4 March ni wastani wa asilimia 5 tu ndiyo walioweza kuchanjwa ndani ya muda huo wote wa miezi mitatu pamoja na hamasa kubwa iliyofanyika na inayoendelea kufanyika. Sababu kubwa ni wasi wasi walionao wananchi pamoja na baadhi ya wanasayansi wao kuhusu chanjo hizo zinazocheza na vinasaba za genes zao. Bado kuna vitu vingi havijajulikana kisayansi. Kwa mfano unaambiwa hata ukichanja lockdown, kuvaa barakoa na mambo mengine unaendelea nayo kama awali. Yaani hata hiyo efficacy yake hawaiamini.
Halafu wanaona kabisa licha ya kuchanja gonjwa hili badala ya kupungua huko kwao limekuwa likiongezeka. Kwa nini?
Vaccination coverage kwa baadhi ya nchi zao ni kama ifuatavyo:
USA 7.7%, Belgium 7.2%, Italy 7.8%, France 7.1%, Netherland 5.9%, Russia 3.7%, Bulgaria 3.5%, Sweden 8.1%, Germany 8.1%, Spain 8.6%, Portugal 8.8%, Greece 9.5%,

5. Huu upendo kwa nchi za Afrika umetokea wapi?:
Wakati kasi ya coverage ya chanjo kwenye nchi zao zimekuwa za kusuasua, sisi wametuandama tuchanjane haraka. Wametupa au kutuahidi kutupa chanjo bure zinazotosheleza kuchanja watu laki 5 kila nchi ya Afrika. Masharti ya chanjo hizi za bure ni kwamba zichanje watu wenye afya nzuri walio na umri wa miaka 18 hadi 45. Wasiwe na magonjwa mengine ye yote including morbid obesity. Wamediliki hata kutuamuru kuwa watu hawa wawe ni walimu na polisi wetu.

Kwa nini wanataka watu wa aina hii ndiyo tuwachanje wakati watu wa aina hii miili yao iko imara kukabili virusi vya corona kwa asilimia 99.9%?
Kwa mjanja atagundua kuwa wanataka kuwafanyia a phase IV clinical trial watu hawa ambayo matokeo yake yanaweza kuondoa wasi wasi walionao watu wao huko ughaibuni kuhusu hizi chanjo.

Wanatusubiri sisi tuchanjane. Hadi sasa nchi 10 za Afrika zimekubali 'msaada' huu na faster faster zimepelekewa hizo chanjo na wameanza kuchanjana.
Nchi inayokataa au kusuasua kupokea 'msaada' huu inaandamwa kinoma na inachukuliwa kama adui. Sisi hatujaukataa bali tumewaambia watupe muda wa wanasayansi wetu kufanya uchambuzi na utafiti. Loo ona mashinikizo tunayoyapata hadi kutoka kwa watu tunaowaheshimu sana. Tupeni muda kidogo. Uamuzi tutatoa bila kushinikizwa tuzitoe wapi na tumchanje nani.

6. Ushauri wangu: Tuangalie zaidi chanjo ya Sinopharm ambayo imeiwezesha China kuudhibiti viziri sana ugonjwa huu.
 
Kuna gazeti linasema imeua kakakuona🤣
Kuna gazeti linasema imeua kakakuona🤣
View attachment 1718553

Kila mtu sikuhizi ni mchambuzi iwe soka au sayansi. Nguchiro alikufa /walikufa katika hatua gani za utafiti.

Ni wangapi walikufa na kwa wakati huo ni nini kilikuwa kinaangaliwa? Kama ni highest level dose toxicity?

Ni adjustment gani ilifanyika baada ya hapo ili kutoleta madhara?

Wanakurupuka bila taarifa rasmi na za kutosheleza team wazalendo paranoid.
 
Chanjo Au Majaribio Ya Dawa Ya Korona( Clinical Trial ) ?

PFizer ni kampuni kubwa na maarufu ya tafiti ya madawa nchini Marekani na maarufu pia kufanya majaribio ya Dawa zake barani Afrika.Katika kutafuta Chanjo ya Korona 2020 wameshirikiana na Kampuni ya Ujerumani BioNTech(Pengine katika Kujikosha) huku wakidai Chanjo yao ina ufanisi wa 95%
Na 11/12/2020 walipewa ruksa na FDA(USA) kutumika rasmi kama Chanjo.
Ni nani PFizer .
Mwaka 1996 katika Jimbo la Kano nchini Nigeria ulizuka ugonjwa wa "Menengetics" haraka kampuni ya PFizer ikatengeneza dawa na Kisha hatua ya majaribio ya dawa hio(Clinical Trials) wakaenda kuifanya kwa watoto nchini Nigeria huko Kano.
Jambo hili lilipelekea watoto kadhaa kupoteza maisha na kesi hii kupelekwa mahakamani.
Ni Mwaka 2009 PFizer ikaomba kesi ifanyike nje ya Mahakama na kulipa Jimbo la Kano dola za kimarekani milioni 75 na familia za watoto waliopoteza maisha(watoto 4) dola za marekani 175,000.

Kwa nini wanapenda kuja Kujaribu Afrika ?
Swali hili analijibu Mwandishi Joseph Conrad katika kitabu chake Cha " Heart of Darkness " 1989 .
Mwandishi anasema wazungu wanaamini sisi sio watu kamili(tuko tofauti Sana na wao)na tunafaa sana kufanyiwa majaribio ya dawa na hasa Chanjo na mengine Kama hayao(kwa maneno yangu)
Kabla ya leseni ya chanjo(Approval and licence) Kuna hatua muhimu tatu ile ya maabara(Exploratory Stage) ambayo huchukua muda mrefu sana(miaka 2 mpaka 3).
Sijui hawa kwa nini wamewahi wakati Chanjo za HIV,Malaria nk zina miaka bado watu wako mahabara.
Halafu huja hatua ya majaribio kwa wanyama(Pre clinical stages) na mwisho hatua ya majaribio kwa mwanadamu (Vacine Trial) hapa hufanyika kwa hatua kuu tatu,Kwanza huanza kwa watu wachache(20-80),Kisha hujaribiwa kwa watu mamia na baadae kwa watu maelfu.
Kimsingi kampuni zote za dawa na chanjo hupenda hizi hatua za mwisho kufanyia Afrika na wapo tayari kutoa mamilioni kama fidia kutokana na maafa yatakayotokea.
Na kutokana na kukithiri kwa rushwa na utawala wa Ovyo katika nchi nyingi Duniani Jambo hili hukubaliwa.

Na wanapotokea watawala wenye kujielewa Kama JPM mambo huwa magumu na wakati mwengine nguvu na hila hutumika.
Mwaka 2014 wakati walipiko wa Ebola Afrika Magharibi zaidi ya sampuli za damu 250,000 zilikusanywa toka kwa wagonjwa na makampuni makubwa ya dawa ya ulaya ili kufanya tafiti za dawa na chanjo.
Mpaka leo USA na Ufaransa wanashindwa kutoa majibu ni wapi zilipo hizo sampuli.
Ukweli ni kwamba zimetumika kuwapatia mamilioni ya pesa katika tafiti zilizopelekea kutengenezwa kinachoitwa Tiba ya Ebola.
Wanadai kutokana na sababu za kiusalama hawawezi kuzirejesha sampuli hizi.

Mwaka 1994 majaribio Kama haya yalifanyika nchini Zimbambwe na Kampuni ya madawa ya USA AZT mradi uliofadhiliwa na CDC na NIH za marekani na kuacha athari kubwa na vifo.
Namibia mwanzoni mwa Miaka ya 1900 madakatari wa kijerumani waliwafanyiaTiba bandia na kuwatia utasa maelfu ya wanawake katika kile kilichokuja kujulikana baadae kama njia za kuzuia mchanganyiko wa kuzaliana Kati ya wazungu na waafrika.
Mwaka 2011 CIA kwa kupitia mlango wa uani(undercover) kukusanya maelfu ya sampuli ya damu nchini Pakistani katika kilichoitwa kampeni feki ya kuandaa Chanjo baadae ikagundulika ulikuwa mkakati wa kuwasaka watuhumiwa wa ugaidi wa muda mrefu waliokuwa kwenye orodha ya CIA jambo lililoleta mgogoro mkubwa wa kidiplomasia baina ya nchi hizi.

Ndio kusema makampuni yote yaliyotengeneza Chanjo ya Korona Kwanza yana agenda ya biashara na pili wana ajenda lukuki za siri wanazojua wao.
Tujifunze kwa Afrika ya kusini walikimbilia kununua Chanjo ambayo sasa wanatafuta wa kumuuzia baada ya tafiti kuonyesha ufanisi wa Chanjo hii kwa aina yao ya virusi ni 22%
Miongoni mwa chanzo zilizopewa ruksa kuuzwa na sasa zinatafuta wateja na ufanisi wake kwa baadhi kwenye mabano ni
Oxford/Astrazaneca ya Uingereza(70%),Johnson/Johnson Janseen USA(72),Moderna/Niaid USA 94.4%,SinoPharm/Beijing Ist.Biogical product CHINA(79%),Consino CHINA,Coronovac CHINA,Bharat Biotech(India),Sputkin Rusia.

Swali kwa nini hakuna chanjo toka Afrika hata moja ?
Ni wakati muafaka sasa kwa nchi za Afrika hasa Tanzania kuwekeza kikamilifu katika tafiti za afya na dawa maana Korona ni mwanzo tunataraji siku za usoni kuwe na mapambano mengi ya kibaiolojia.
Tafiti hizi zisimamiwe kwa ukaribu na taasisi za ulinzi na usalama Kama wafanyavyo wenzetu kusimamiwa na wataalamu bobezi wa maeneo husika hasa vyuo vikuu maana hii ni vita mpya ya kibaiolojia Duniani .
👏👏👏👏

Tuache spinning na kuunganisha vipande vya taarifa zisizohusika.

Kama kuna mtu ana taarifa husika za majaribio ya chanjo husika/clinical trial na alete full report tuchambue na jinsi ilivyoingizwa kwenye emergency permit ili kuanza kutumika. Vigezo na masharti vilizingatiwa zaidi ya hapo ni upuuzi kuunganisha vimaelezo na kufanya kama taarifa rasmi ya kisayansi.

Tuna TMDA, kama chombo chenye mamlaka ya kupata na kupitia taarifa ya DAWA YOYOTE NA VIFAA TIBA kabla havijaingizwa nchini. Hii huusisha kwenda kuangalia kupitia mnyororo mzima wa molecules discovery, development, whole trials na eneo, jinsi uzalishaji wa dawa husika unavyofanyika.

Hawa ndio wenye nguvu ya ufukunyuzi halisi na wasemaji wetu kwa waliyoyapata kutokana na kazi zao, kama ilivyo kwa data zote za wagonjwa chini ya wizara ya afya.

Mengine yote ni mambo ya kusikia tu.
Tumeacha kupambana na Corona kisayansi na tumeamua kutengeneza taifa lenye wasiwasi bila fact (PARANOID). Baada ya Corona tuna kazi ya kutafuta dawa ya hii hali pia na kwa kasi na nguvu mnayotumia wengi wataambukizwa na matokeo yake tutayabeba.

Mfano: Hatujui ni kwa kiasi gani coverage ya chanjo zingine zitaenda kuathirika. Under five na pregnant women.

Hivi mbona ARV tu, hatujasema hayo yote? Madawa mengine na vifaa tiba? Tulienda lini binafsi kuangalia trials zake individually?
Je kwa nini wasipitie huko?
Hizo toothpick tunazoimport?
Simu?
Magari?
Pombe?
Vyakula/juisi?
Nguo?
Viatu?
LETENI SCIENTIFICALLY PROVEN FACTS AND STOP BEING PARANOID.
 
Asante kwa ushauri wako mzuri
 
Back
Top Bottom