Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,027
- 20,414
PFizer ni kampuni kubwa na maarufu ya tafiti ya madawa nchini Marekani na maarufu pia kufanya majaribio ya Dawa zake barani Afrika. Katika kutafuta Chanjo ya Korona 2020 wameshirikiana na Kampuni ya Ujerumani BioNTech (Pengine katika Kujikosha) huku wakidai Chanjo yao ina ufanisi wa 95%
Na 11/12/2020 walipewa ruksa na FDA(USA) kutumika rasmi kama Chanjo.
Ni nani PFizer
Mwaka 1996 katika Jimbo la Kano nchini Nigeria ulizuka ugonjwa wa "Menengetics" haraka kampuni ya PFizer ikatengeneza dawa na Kisha hatua ya majaribio ya dawa hio (Clinical Trials) wakaenda kuifanya kwa watoto nchini Nigeria huko Kano.
Jambo hili lilipelekea watoto kadhaa kupoteza maisha na kesi hii kupelekwa mahakamani.
Ni Mwaka 2009 PFizer ikaomba kesi ifanyike nje ya Mahakama na kulipa Jimbo la Kano dola za Kimarekani milioni 75 na familia za watoto waliopoteza maisha (watoto 4) dola za Marekani 175,000.
Kwa nini wanapenda kuja Kujaribu Afrika?
Swali hili analijibu Mwandishi Joseph Conrad katika kitabu chake Cha "Heart of Darkness" 1989
Mwandishi anasema wazungu wanaamini sisi sio watu kamili(tuko tofauti Sana na wao)na tunafaa sana kufanyiwa majaribio ya dawa na hasa Chanjo na mengine Kama hayao(kwa maneno yangu)
Kabla ya leseni ya chanjo (Approval and licence) kuna hatua muhimu tatu ile ya maabara(Exploratory Stage) ambayo huchukua muda mrefu sana(miaka 2 mpaka 3).
Sijui hawa kwanini wamewahi wakati Chanjo za HIV, Malaria nk zina miaka bado watu wako mahabara.
Halafu huja hatua ya majaribio kwa wanyama (Pre clinical stages) na mwisho hatua ya majaribio kwa mwanadamu (Vacine Trial) hapa hufanyika kwa hatua kuu tatu,Kwanza huanza kwa watu wachache(20-80), kisha hujaribiwa kwa watu mamia na baadae kwa watu maelfu.
Kimsingi kampuni zote za dawa na chanjo hupenda hizi hatua za mwisho kufanyia Afrika na wapo tayari kutoa mamilioni kama fidia kutokana na maafa yatakayotokea.
Na kutokana na kukithiri kwa rushwa na utawala wa Ovyo katika nchi nyingi Duniani Jambo hili hukubaliwa.
Na wanapotokea watawala wenye kujielewa Kama JPM mambo huwa magumu na wakati mwengine nguvu na hila hutumika.
Mwaka 2014 wakati walipiko wa Ebola Afrika Magharibi zaidi ya sampuli za damu 250,000 zilikusanywa toka kwa wagonjwa na makampuni makubwa ya dawa ya ulaya ili kufanya tafiti za dawa na chanjo.
Mpaka leo USA na Ufaransa wanashindwa kutoa majibu ni wapi zilipo hizo sampuli.
Ukweli ni kwamba zimetumika kuwapatia mamilioni ya pesa katika tafiti zilizopelekea kutengenezwa kinachoitwa Tiba ya Ebola.
Wanadai kutokana na sababu za kiusalama hawawezi kuzirejesha sampuli hizi.
Mwaka 1994 majaribio Kama haya yalifanyika nchini Zimbambwe na Kampuni ya madawa ya USA AZT mradi uliofadhiliwa na CDC na NIH za marekani na kuacha athari kubwa na vifo.
Namibia mwanzoni mwa Miaka ya 1900 madakatari wa kijerumani waliwafanyiaTiba bandia na kuwatia utasa maelfu ya wanawake katika kile kilichokuja kujulikana baadae kama njia za kuzuia mchanganyiko wa kuzaliana Kati ya wazungu na waafrika.
Mwaka 2011 CIA kwa kupitia mlango wa uani(undercover) kukusanya maelfu ya sampuli ya damu nchini Pakistani katika kilichoitwa kampeni feki ya kuandaa Chanjo baadae ikagundulika ulikuwa mkakati wa kuwasaka watuhumiwa wa ugaidi wa muda mrefu waliokuwa kwenye orodha ya CIA jambo lililoleta mgogoro mkubwa wa kidiplomasia baina ya nchi hizi.
Ndio kusema makampuni yote yaliyotengeneza Chanjo ya Korona Kwanza yana agenda ya biashara na pili wana ajenda lukuki za siri wanazojua wao.
Tujifunze kwa Afrika ya kusini walikimbilia kununua Chanjo ambayo sasa wanatafuta wa kumuuzia baada ya tafiti kuonyesha ufanisi wa Chanjo hii kwa aina yao ya virusi ni 22%
Miongoni mwa chanzo zilizopewa ruksa kuuzwa na sasa zinatafuta wateja na ufanisi wake kwa baadhi kwenye mabano ni
Oxford/Astrazaneca ya Uingereza(70%),Johnson/Johnson Janseen USA(72),Moderna/Niaid USA 94.4%,SinoPharm/Beijing Ist.Biogical product CHINA(79%),Consino CHINA,Coronovac CHINA,Bharat Biotech(India), Sputkin Rusia.
Swali kwa nini hakuna chanjo toka Afrika hata moja?
Ni wakati muafaka sasa kwa nchi za Afrika hasa Tanzania kuwekeza kikamilifu katika tafiti za afya na dawa maana Korona ni mwanzo tunataraji siku za usoni kuwe na mapambano mengi ya kibaiolojia.
Tafiti hizi zisimamiwe kwa ukaribu na taasisi za ulinzi na usalama kama wafanyavyo wenzetu kusimamiwa na wataalamu bobezi wa maeneo husika hasa vyuo vikuu maana hii ni vita mpya ya kibaiolojia Duniani.
👏👏👏👏