Changamoto za watoto wa nje ya ndoa

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Wanajukwaa wasalaam, mkitaka kujua khali yangu Mimi ni bukheri wa afya, namshukuru Mola wetu kutuzidishia urijali kwa ustawi wa familia zetu

Leo napenda niulize hasa kwa wanaume wenzangu wenye watoto nje ya ndoa, ni Changamoto gani mnazopotia, na mnazitatua vipi, na je watoto hao wana namna ya baraka au heri katika ndoa? Je, wanatambulishwa ndani ya ndoa?

Uzi udumu muda mrefu, na wakati mwingine ni suluhu kwa matatizo yanayojiri, hivyo tuujadiliane kwa unyenyekevu.
 
Mbona kawaida tu mkuu? watoto wa nje ya ndoa wapo wa aina mbili,,wapo uliowapata kabla hujaoa na ambao umewapata baada ya kuwa ndani ya ndoa tayari....wale uliowapata baada ya ndoa ndy shida kuwatambulisha,,na sio wale waliokuwa kabla ya ndoa...ukitokea umepata mtoto nje ya ndoa kinachomuumiza zaidi mke wa ndoa,,ni mahusiano ya kuendelea na yule mama wa mtoto na sio yule mtoto uliyezaa nje...,,lakini kama ukijieleza vzr,,na kuhakikisha umekata MAHUSIANO na hyo uliyezaa nae sidhani kama kutakuwa na shida... Inaeleweka kuwa kuteleza ktk ndoa kupo,,,na ieleweke kuwa mwanamme hana uwezo wa kuzuia mimba,,Bali mwanamke mwenyewe,,, sometimes mwanamke huamua kuzaa na Fulani,, huwezi kukwepa kwa hilo....atakuelewa tu mkuu..
 
Kumtambulisha na kuishi nae mtoto wako wa nje ndani ya ndoa uliyo nayo ni njia ya kupunguza changamoto,mshawishi mwanamke amkubali mtoto wako na muongoze mtoto wako awe mfano wa kuigwa.
 
Aiseee Mimi ninaye Ila nilichojifunza ni kuwa na msimamo sababu ukiwa mpole sana kisa mkeo ata atakasirika anaweza kukuwekea mipaka Kwa mwanao kitu ambacho ni ujinga mkubwa sana chapili beba majukumu ya wanao fanya wakutane na wanao wengine ili kuweka umoja kati Yao wape huduma za kufanana siyo uyu anasoma uyu hasomi achana na dhana ya mtoto wa nje si wanao tambua ndugu yako halisi ni mwanao na si vinginevyo
 
Wanajukwaa wasalaam, mkitaka kujua khali yangu Mimi ni bukheri wa afya, namshukuru Mola wetu kutuzidishia urijali kwa ustawi wa familia zetu

Leo napenda niulize hasa kwa wanaume wenzangu wenye watoto nje ya ndoa, ni Changamoto gani mnazopotia, na mnazitatua vipi, na je watoto hao wana namna ya baraka au heri katika ndoa? Je, wanatambulishwa ndani ya ndoa?

Uzi udumu muda mrefu, na wakati mwingine ni suluhu kwa matatizo yanayojiri, hivyo tuujadiliane kwa unyenyekevu.
Watoto wa nje ya ndoa ni ishara ya wazi kuwa mkeo asikuamini tena. Hili huifunua zaidi Tania ya mwanamume na hivyo ndivyo ilivyo
 
Wanajukwaa wasalaam, mkitaka kujua khali yangu Mimi ni bukheri wa afya, namshukuru Mola wetu kutuzidishia urijali kwa ustawi wa familia zetu

Leo napenda niulize hasa kwa wanaume wenzangu wenye watoto nje ya ndoa, ni Changamoto gani mnazopotia, na mnazitatua vipi, na je watoto hao wana namna ya baraka au heri katika ndoa? Je, wanatambulishwa ndani ya ndoa?

Uzi udumu muda mrefu, na wakati mwingine ni suluhu kwa matatizo yanayojiri, hivyo tuujadiliane kwa unyenyekevu.
Kulea mtoto wa kambo ni kipaji na karama ambayo wanawake wengi hawana
Mwanamke atampenda sana mwanao mkiwa mko kwenye mahusiano ya awali kabla ya ndoa... Lakini anapoingia ndani utaanza kuona tofauti.. Sauti atakayoitumia kwa mtoto ni tofauti kabisa na sauti atakayoitumia kwako

Kuna wakati utatokea mgogoro wa kugombea nafasi ya upendo na kujaliwa kwenye moyo wako hasa kama mwanao alishazoea kuwa nawe beneti.. Hapa ni pagumu sana kwakuwa sasa asali wako wa moyo naye ataihitaji hiyo nafasi... Unatakiwa kubalance sana hapa....

Jr
 
Hiyo rahisi ukimleta mtoto wa nje hakikisha na yeye ana mimba au kashakuzalia katoto
 
Kama ninao watoto wa nje ya ndoa kamwe na katu sintoweza kuwatenga wanangu mke akiwakataa Bora aondoke yye aniache na damu yangu
Unaweza ukawa na upendo sana na wanao, lakini kumbuka muda mwingi anayeshinda na watoto ni mwanamke, hutajua kirahisi manyanyaso wanayopata wanao lkn athari bado watakuwa wanazipata!!

Msingi hapo ni kukataa uwezekano wa kuwa na watoto wa nje ya ndoa maana mwenye maamuzi wa hili ni wewe!!!
 
Back
Top Bottom