Changamoto za kimaisha zinataka kunifanya nichukue maamuzi magumu na ya kishetani

The king mswati

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
787
820
Habari zenu wakuu.

Bila kuwachosha nina mada ya ku-share na ninyi ingawa sijui kama hili jukwaa ni sahihi ama laa mtanisamehe bure.

Kiufupi mimi ni kijana wa 26 years na sijaoa bado ila kuna changamoto kadhaa za maisha zinanitia wazimu sana kiasi cha kunifanya nianze kufikiri nje box tena kwenye mambo yanayohusiana na ushetani kabisa (Freemasons & Illuminati societies).

Nilibahatika kusoma (Level ya degree moja) na nilihitimu mwaka 2018 lakini mpaka sasa ajira ya uhakika sijaipata,

Kuna mahali tu nimejiegesha napata Tsh 380,000/= per month.

Tatizo ni kwamba matumizi ni mengi kuliko kipato changu natakiwa nilipie chumba, nilipie umeme, nilipie maji, ninunue vitu vya kula ndani na kinachonigharimu zaidi ni kuwa na wategemezi wengi hasa wazazi na wadogo zangu.

Kwa hiyo huwa najikuta kipato changu cha mwezi siyo kitu (hakitoshi hata robo ya matatizo yangu) na kibaya zaidi kinachonitia stress ni kwamba kila mwisho wa mwezi unapofika matatizo huanza kujizalisha kwa fujo kama mvua.

Sasa nimekuja kujitafakari na kuona kwamba nitaishi kwenye maisha ya umaskini na fedheha hadi lini?

Ni lini mimi nitafanikiwa na kuwa na maisha yangu na kuonekana kwamba niliishi Duniani? Nikiangalia familia yangu Baba, Mama na wadogo zangu maisha wanayoishi inaniuma sana kwa sababu ni umaskini unaofedhehesha.

Kutokana na kulemewa na mawazo ya umaskini na katika kufikiri namna ya kuanza kujikomboa kwenye umaskini, ndipo nilipokutana na jamaa mmoja Mmarekani wa huko Los Angeles.

Huyu jamaa ni mzungu na alinitumia Email akisema yeye ni Agent wa Illuminat (Devil worshiper Master) na akasema huko kuna Utajiri, umaaarufu, Nguvu n.k

Akanipa namba ya WhatsApp tukaanza kuchati.

Nikachati nae mambo mengi sana kuhusu jamii ya Illuminati ila key point niliyomuuliza ni kwamba "Is there any blood or human sacrifices in this society ?"

Yeye akanijibu "NO" na nikaona kama hakuna kafara ya damu wacha nijaribu nimechoka kufedheheshwa na Umaskini.

Tukaanza process zote za kujiunga akanipa form ya kujaza nikajaza na masharti kama 15 hivi nikayasoma ila sharti nililoliona gumu lilisema "Nisioe Wala kufanya mapenzi mpaka pale nitakapopata ruhusa kutoka kwa Master wao".

Lakini bado sikukata tamaa kutokana na hilo sharti maana katika masharti yote 15 ilikuwa hakuna hata sharti moja linalosema kuwa nitatakiwa kutoa kafara ya damu.

Nikamwambia tuendelee mbele kwa ajili ya initiation process.

Nilikuja kushindwana nae aliponiomba USA dollar 200, nikamuuliza kama nyie ni matajiri na mnatoa pesa Je dollar 200 kwangu unaitaka ya nini?

Akanijibu kuwa "It is a sacrifice for Lucifer to help you "

Nikaona huyu jamaa nitapeli nikam-block muda huo huo.

Sasa picha lingine limekuja juzi, kuna jamaa mmoja hivi kani follow Instagram anaitwa Illuminati 666, baada ya kuni- folllow nili agree request alafu baadae akanitumia ujumbe mrefu sana DM.

Akasema yeye ni Devil Worshiper na anawaleta watu kwenye ulimwengu wa mafanikio na pia akasema watu wanaotozwa pesa kama ada ya kujiunga ni uwongo kwani kujiunga na Illuminati ni free ili mradi tu uwe umekidhi vigezo.

Huyu jamaa nilimuuliza maswali mengi sana lakini badae nilijiridhisha kuwa siyo tapeli wa kuomba hela kama yule wa kwanza.
Na akanambia in Iluminatti - no bloodshed

- no registration fee

- no human sacrifice

Nikaona imekaa poa.tukaanza process zote ila tu alinipa angalizo kwamba kifo huja pale mwanachama anapotoa siri kwa watu wasiohusika (ambao si wanachama)

Aisee niwe mkweli kwamba nimeshafanya process zote hadi kitambulisho cha NIDA nishamtumia na picha yangu moja kwa ajili ya kunitengenezea Identity card ya Illuminati.

Sasa process iliyopo kwa sasa ameniambia nimtumie video ya dakika 2 ya kuomba kwamba nataka Mungu wao (wao wanamwita BAPHOMET) anifanyie nini.

Na kilichonipa wakati mgumu niandike hapa ni kwamba kuna maneno ambayo amenipa nianze nayo na kumalizia nayo na ni kama kiapo hivi ila ni maneno makali sana hadi nafsi inatetemeka ninapoyataja tu.

Yanasema hivi "Hail the Lucifer, The leader of this world who created Men and Women, Hail the light and open the gate of Hell to come and hug me your brother, Hail our Lord BAPHOMET"

Mengine sijayataja maana ni sala ndefu kidogo amenambia kuwa hayo maneno hapo juu ni very spiritual kuwa nitakachokisema ndicho kitakachokuwa.

Sasa wakuu mimi kichonipa wakati mgumu ni kurekodi video nikiyasema hayo maneno hapo maana ni makali mno mpaka natetemeka mwenyewe ingawa umaskini nauchukia pia.

Na lengo mimi la kuingia huko ni niwe tu maisha mazuri na kusaidia wengine wenye uhitaji na wasiojiweza wala mengine sina mda nayo.

Ahadi alizoniahidi ni kwamba iwapo nitakidhi vigezo vya kukubaliwa basi nitapewa USA dollar elfu 60 kama zawadi ya kuanza maisha mapya.

Halafu baada ya hapo siku ya kwenda kula kiapo nitakutana na illuminati wa nchini kwetu ambao watanifanyia ceremony na kunipa zawadi kama nyumba, magari ama kunipa job offer kwenye kampuni zao ama kunifanyia promosheni yeyote ile.

Na pia kabla ya kuwa full member watakuwa wanatoa mshahara wa dollar laki moja kwa mwezi kwa mwanaume na dolla laki moja na nusu kwa mwezi kwa mwanamke kama njia ya kuwa full membership ambao hapo inaweza kuchukua miaka kadhaa pia.

Mimi nimeona kwamba haya ndiyo maisha ninayoyataka maana umaskini ushanifedhehesha sana.

NB: You will not success by any means if you will not sell your soul to the Lucifer, and money is something to some people but is nothing to those who made it"

Haya ndiyo maneno aliyoniachia.
 
Tutafanyaje mkuu ..ndo ushaamua kuuza nafsi yako.
Unajua huyu jamaa kwa kauli yake anasema Mungu na Lucifer wote ni wema na wanafanya kazi pamoja

Hata katika kujiunga lazima uwe na dini na unaapa kwa imani yako kama ni mkristo biblia inatumika na kama ni mkristo Quran inatumika, kwa imani zingine hivo hivo unaapa kwa imani yako.

Anasema Mungu aliumba watu ili wawe matajiri na siyo maskini ila Umaskini wanaitaka wao na walioamua kuondokana na umasikini ndiyo wapo huko.
 
Ishi kulingana na kipato chako.

Hapo usikute umepanga nyumba ya 150,000/= kwa mwezi wakati kipato chako ni 380,000/= tu.

Ukitaka uishi kichuo chuo nakuhakikishia hutoboi kijana.

Huko unakotaka kwenda ndio utapotea kabisaaaa, maaana kuna mambo ya kafara, hao ndugu zako unaowasaidia kwa sasa utaanza kuambiwa uwatoe kafara kitu ambacho kitaku-hunt your whole life.

Live a real life not virtual one.
Unforgetable
 
mkuu kama unataka kujiunga freemasons si uende pale kitegauchumi kwa nyuma kanisa lao liko wazi muda wote kwanini uhangaike na vishoka wa mitandaoni au kama unataka hela za magumashi nenda kule Temeke Buza kanisani pale muulize bodaboda kwa Mwandulame wapi watakuonesha na utakua tajili overnight sema kuna masharti kama kuua mb
*noo unakua na hela kinoma wengi wanafanikiwa
 
Ukisharecord wanakuwa wanatumia video zako kushawishi wengine kuwa vijana wapo kibao wanaojiunga. Au atatumia hiyo video kuku blackmail ili umlipe asikuchafue kwenye mitandao. Utakuja kushangaa dunia nzima video zako zipo.
Duuh...aisee mbona kama umenifungua kitu mkuu

Wazo lako ni kama linanifungua akili hivi..ebu ngoja nilitafakari kwa kina
 
Degree? Uko bize kusambaza infos zako to a total stranger? Nida umeweza ila video ndiyo unashindwa? Soon utaambiwa tuma namba ya akaunti yako ya benki ili utumiwe hela.

As long as maamuzi magumu siyo kujiua mi sikushauri kitu.

Tumia degree yako kujiona unapoelekea katika hiyo deal.
 
Ishi kulingana na kipato chako.

Hapo usikute umepanga nyumba ya 150,000/= kwa mwezi wakati kipato chako ni 380,000/= tuu...
Mkuu kwenye suala la kafara bora tu waniue mm ila sipo tayari kitoa damu ya mtu na pia kama nilivyosema amenihakikishia kuwa hamna kafara ya damu bali kuna ya items ambazo item zenyewe alinitumia ni manidhaa tu yenye nembo zao

Sasa kama wataenda kunigeuka kuwa nitoe kafara ya damu hapo itakuwa wametumia uwongo wa kunidanganya niingie alafu wanibadilikie, ingawa amenambia kuwa kafara huja pale unapotoa siri kwa wasiohusika hapo ndiyo unaweza kufa wewe mwenyewe

Na pia suala la kuishi room kweli nalipa laki na nusu kila baada ya miezi mitatu ( yani elfu 50 kila mwezi) na siyo kwamba napenda kulipa hiyo gharama bali mazingira ya kazi yenyewe maana ni maeneo flani ya utalii maisha ni ghali sana nanasi tu unanunua elf 5, embe buku 2 yani kwa kifupi maisha ni ghali hadi kero
 
mkuu kama unataka kujiunga freemasons si uende pale kitegauchumi kwa nyuma kanisa lao liko wazi muda wote kwanini uangaike na vishoka wa mitandaoni au kama unataka hela za magumashi nenda kule temeke buza kanisani pale muulize bodaboda kwa mwandulame wapi watakuonesha na utakua tajili overnight sema kuna masharti kama kuua mb
*noo unakua na hela kinoma wengi wanafanikiwa
Mimi pesa za kumwaga damu ndiyo naziepuka na pia kusema niende sijui wapi wapo sidhani kama ni kweli kwa sababu jamii hizi hujiendesha kisiri mno ndiyo maana huwa ni nadra watu kujua kuwa hawa jamaa hufanya nini hasa kuwapa watu utajiri
 
mkuu mpigie huyu jamaa fundi 0714 022 953 kama unatafuta kazi mahali anaweza fanya mambo ukafanikiwa we muelezee shida zako atajua jinsi gani akusaidie only kama uko serious
Hawa waganga wa kienyeji wa kwenda kunambia niende nikaoge usiku njia panda ama kupasua nazi ama uje na jogoo mweusi sijui...hawa siwawezi

Maana kama ni hao hata hapa ninapoishi kuna mabango hadi bara barani kuwa tunaunganisha watu freemason sijui tunatajirisha watu..naonaga uzushi tu maana anae anaesema anakuunganisha yeye mwenyewe maskini tu
 
Iko hivi, baada ya kula hicho kiapo atakuambia umefuzu na shetani amekukubali sana, atasema anaanza process ya kukutumia dola elfu 60, na ili kufanikisha inabidi uwe na account ya nje ambapo utaambwa utume dola 200 ili wakusaide kufungua akaunti hiyo.

ukishawatumia dola 200 inakua imeisha hiyo anakutia block.
 
Back
Top Bottom