Changamoto za kifedha baina ya wenza zinazidi kuongezeka

Kabisa!mtu aliyeoa au kuolewa sio sahihi kuishi kisela na haitakiwi,lazma ujielewe na ueleweke kwa kuzingatia heshima na maadili mema....
kama hauko tayari kwa haya ni mtihani
Tatizo la watu wengi wanaitamani ndoa, lakini kiukhalisia hawapo tayari kuiishi hiyo ndoa, si wanaume wala wanawake.!! Kama ulivyosema wengi bado wanaishi kisela sababu maana khalisi ya ndoa imepotea imebaki fashion ya kuingia kwenye ndoa.
 
Kuna mwanamke mmoja comment za juu hapo kasema wakati wa uchumba hajawa spoiled lakini anakula raha ndani ya ndoa.

Hatuwezi beba majukumu ya wazazi wakati wa uchumba, ndani ya ndoa wewe ni jukumu langu asilimia mia.
Wakati tayari una chembe chembe za ku spoil gold diggers, unadhani ukiingia kwenye ndoa utakuwa mtu tofauti wa kutoka sayari nyingine??
 
Tuseme kweli jamani, Uzi wa SweetieLee unafundisho na kweli nzuri sana, Uzi huu kila anaeusoma na kuuelewa, atajifunza kitu kikubwa sana kwenye mahusiano yake na kuwa na mahusiano bora daima.
Hongera SweetieLee! !!
 
Mimi ninaamini kuwa mwanaume ndiye kichwa cha familia na ni mtu wa kwanza kuchuua majukumu ya familia kikamilifu. Mwanaume anayejitambua atafanya kila kitu kwa ajili ya familia yake. Na mwanamke anayejitambua kama msaidizi wa mume wake inatakiwa kwa utashi wake (mwanamke) aone haja ya kumsaidia mume wake mambo madogomadogo (hata makubwa) baada ya kuona mume wake anafanya majukumu yake ipasavyo nyumbani. Ifikie hatua "a-apreciate" kwamba kweli my husband is doing a lot to this family let me help him on this/that, huyo ni mwanamke anayejitambua sana. Na ndio maana wanaume waliowengi huwa hawaulizi mshahara wa mke wake kaufanyia nini na hata kujua analipwa sh. ngapi labda mke wake amwambie. Na unaweza kuta mke anajua password ya ATM card ya mume wake lakini mume hajui yake (angalizo; hapa ni kwa mwamke anayejitambua ndo atapewa hiyo password kwa sababu is a good manager of the familly).

So, wanaume tutimize majukumu yetu ipasavyo ili wake zetu watuunge mkono kutokana na juhudi zetu tunazoonesha kutunza familia na sio kuwalazimisha kuchangia matumizi ya familia. Kila mtu atimize sehemu yake then mtajikuta mko kwenye Equilibrium, otherwise kufikia hiyo point itawachukua karne au msiifikifie kabisa.
 
Nasubiri jibu kwa kweli maana hili ni janga lengine kwenye jamii yetu,unakuta mme hatunzi familia hususani mkewe ila gold diggers anawagharamia!...Huwa haniingii akilini kwanini upoteze pesa na mda kwa vitu visivyo add value in your life?
Wanawake wengi wanaishi maisha magumu mno, ukilinganisha na ukhalisia wa vipato vya wenzi wao, ukilinganisha maisha ya mke wa ndoa na maisha ya kimada ni mbingu na ardhi.!!
Mungu awahurumie wanaume tu hakuna namna!!
 
Cole Williams,
Umeongea ukweli mtupu Cole, maisha yamekuwa magumu mno katika mahusiano kwa sasa, 'Men Lie, Women Lie, no one is speaking truth'..!!

Watu wanaoana kwa upendo mkuu, ila humo ndani wanaenda kuishi kiuadui sana!!
 
Mkuu ila wewe si ndiye uliyesema huwa mnavimba mkiwa na maslay queen that means pesa inatumika kuwapata,sasa mbona wajipinga tena?

Yule dada ambaye yuko spoiled ndani ya ndoa anabahati sana maana huku kwetu wenzie wanachakaa ndani ya ndoa ila michepuko inanona
Shuhuda tunazokutana nazo za wanandoa zinakatisha tamaa na kusikitisha sana!!
Wanaume wajitafakari na kubadilika jamani!!
 
Umesema hawatachangia wamechangia, naona umekuja na nyingine ya wataharibu baadae.

Naona kama wewe ndo huna mpango mzuri na hii thread, unaitabiria mabaya.
Haha,
Hakuwa na nia mbaya bwaana Don C, kajaribu tu kutoa maoni yake kulingana na ukhalisia wa mambo ulivyo.!
 
Hii ipo sana n sielewi hua wanakua na maana gani ni kwamba mtu hajiamini au ndo vile hataki kuishi uhalisia wake

Wanaume wakiacha hii tabia bas hata malalamiko ya kusema girls wanapenda hela yatapungua. Napenda sana wanaume wasiopretend kuhusu financial status zao maana inakua rahisi pia kumuamin kuliko yule kila mkionana anataka kujimwambafy
Haha.!!
Eti kujimwambafay,
Kuna wanaume wanajua kufake bwaana, wanaishi maisha magumu kwa kujitakia wakati wapo wanawake wanaopenda reality na nawaambia kila siku, mwanamke anayekupenda kwa dhati ni ngumu mno kukufanya sponsor!!
 
Tuseme kweli jamani, Uzi wa SweetieLee unafundisho na kweli nzuri sana, Uzi huu kila anaeusoma na kuuelewa, atajifunza kitu kikubwa sana kwenye mahusiano yake na kuwa na mahusiano bora daima.
Hongera SweetieLee! !!
Ahsante sana mkuu yakobo11 usinisifie hivi sana nitaishia kuringa buree!!
Barikiwa mno!!
 
Back
Top Bottom