Changamoto za kifedha baina ya wenza zinazidi kuongezeka

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
7,398
24,680
Hello guys,

Kwa wale wenzangu na mimi tunasema TGIF..!!

Naomba kuzungumza na waliopo ndani ya ndoa na wale wanaotarajia kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Kwenye mahusiano hasa ya uchumba, kuna hii tabia ya ndugu zetu wa kiume kutumia nguvu kubwa mno kutu-impress ladies kwa mitoko ya gharama, zawadi za bei ghali, shoppings za hapa na pale bila kusahau adventures - wenyewe wanaita kutu 'spoil'.

Hell yeah! Tumeumbwa kuwa wapokeaji we can't say 'No' to such offers and, in a meantime, tutawakubali tutakuwa nanyi sababu hiyo ndiyo aina ya maisha mliyotuonyesha na kutuaminisha kuwa we can live that life happily ever after.

Haha, picha linaanza baada ya kuwa mwili mmoja, ukishakubali kuishi kwa shida na raha mpaka pale kifo kitakapowatenganisha, hapo ndo wakati pekee utaujua uhalisia wa maisha ya mwenza wako..!!

Unaanza kuona mwenza wako kabadilika; mbona hakujali kama alivyokuwa anafanya wakati wa uchumba? Kwanini kila unachomuomba anasema hana pesa..!?

Dear ladies, sikatai kweli wapo wanaobadilika ila pia asilimia kubwa ya wanaume wengi wanakuwa wana-fake uhalisia wa kipato chao, hivyo ukija jumlisha na majukumu ya familia za pande zote mbili ni lazima mambo upande wao yawe magumu mno..!

Dear brothers,
Tunapenda sana kuwa spoiled na ninyi, ila tafadhalini sana msiishi nje ya budget wala uwezo wenu, muoneshe mchumba wako uhalisia wa maisha yako kabla hajasema 'Yes I do'. Uwe na uhakika na amani moyoni kuwa amekubali kuwa na wewe kwa hali yoyote ile uliyokuwa nayo, hebu msitunishe misuli mpaka mkachana mashati..!

Na ni muhimu mfahamiane vizuri kabla ya kuishi pamoja. Lazima umjue mwenza wako vyema, is she a good saver? Are you an extremely spender? Do both of you believe in debts? Mna assets gani? Mna mipango gani kwenye maisha yenu na je, budget yenu itakidhi na kuyafikia malengo yenu mkianza kuishi pamoja kama familia? Wewe una mshahara na yeye ana mshahara that's good and okay, lakini ni lazima mliweke hili sawa kabla ya kuishi pamoja. 'Ni changu changu, chako chetu' ama '50 by 50'..!!

Na mliopo kwenye ndoa jitahidini sana kuliweka hili sawa baina yenu, jifunzeni kuwa 'open' and 'honest' kwa wenza wenu linapokuja suala la 'waleti' zenu, ukweli na uwazi wa kipato chenu ndiyo utakaojenga msingi bora wa kuimarisha muhimili wa maendeleo ya familia imara! And don't forget that 'marriage is forever..!!

Utachagua mwenyewe kuishi huru ama kuishi katika 'kifungo huru'..!

''Money is one of the biggest thing couples do always fight about'' - Cary Siegel..!!

Tafakarini hili na mchukue hatua stahiki, Blessed Weekend Dears..!!
 
SweetieLee, ]SweetieLee,
Umeleta Uzi mzuri sana wenye viwango vyote vya kuijenga ndoa (Agano) la mke na mume, Katika uhalisia na kweli tupu. Kusema kweli kwenye neno la MUNGU, Kitabu cha Efeso 5:22-24, imeandikwa, kwa maana " mume ni kichwa cha mkewe, kama KRISTO naye ni kichwa cha kanisa.

Ipo hivi, Mume ni kichwa cha mkewe ambaye ni kanisa. Kwahiyo mke ni kiwiliwili ambacho ndiyo kanisa. Sasa kama mke ni kiwiliwili basi ndiye mwenye mikono ya kupokelea na kufanya vita zidi ya maadui wa mume na familia yote.
Kwahiyo swala la uwazi wa mambo fedha ni muhimu kujenga mahusiano bora.
Naunga mkono Uzi SweetieLee!
 
50/50 kiuhalisia ni ngumu,mfano weekend mimi nategemea kurudi nyumbani asubuhi nimelewa na unifungulie mango,haitowezekana wewe urudi umelewa nikufungulie lazima ulale nje.
Nazungumzia suala la kipato zaidi mkuu,
Ila kama umekwishaoa na bado unarudi nyumbani asubuhi, ungemaliza kwanza hayo maisha kabla ya kuwa committed..!!
 
Nadhani umeongelea michepuko si wachumba! Hakuna mwanaume atakayefake kwa mchumba sana sana ataonesha hana kitu wakati anazo.
Wapo wanao fake sana tu mkuu, wanajitutumua kuliko uwezo wao, mfano mzuri ni pale mwanaume anaenda ukweni, baadhi yao wanaazima mpaka magari ya kifahari wakati kiuhalisia hata gari la mkopo muoaji hana.!!
 
77 Reactions
Reply
Back
Top Bottom