Changamoto za kifedha baina ya wenza zinazidi kuongezeka

Changamoto za kifedha baina ya wenza zinazidi kuongezeka

Latakiwa kuwa endelevu na kwa hili sipingani nawe, maana ni sehemu ya kudumisha intimacy...

Isipokuwa maisha huwa hayasimami, muda unapoenda kuna vipaumbele vingine vinatokea ikiwemo watoto n.k...

Wengi wa wanawake pia hujikuta tu baada tu kuolewa huwakataza wenzi wao kupunguza kutumia fedha katika minajili hii ya mitoko, zawadi zawadi za mara kwa mara n.k

Wanaondeleza maisha ya hivi mara nyingi utapata ni wale ambao wapo na mafanikio ya mali na fedha kiasi kwamba saving kwao si jambo ya kipaumbele...
Nimekuelewa vizuri mkuu..!
Jitahidi uwe unam spoil japo mara moja moja Mrs, hii itaongeza intimacy baina yenu.! Na wakati huo huo wengine wanajisahau na ku-spend too much kwa michepuko mpaka wanasahau wake zao nyumbani halafu wanakuja kusingizia ni majukumu.!!
Mungu anawaona wanaume.!!
 
Napenda vitu vizuri ila sipendi mwanaume wangu atumie hela hovyo.
Ni juzi tu nimetoka kumwambia sipendi anavyotumia hela zake kwa vitu visivyo na maana kama starehe.
Wewe ni mwanamke mzuri sana, kila mwanaume aombe apate mwanamke wa aina yako naamini atauaga umaskini kabisa.! Barikiwa mumie.!
 
Wewe ni mwanaume wa kwanza kuwa wa kitofauti, kuwa na different hobbies na zile ambazo nilizoea kila mmoja huwa anazo..

Uliishi na washkaji wenzio kabisa katika kukua kwako?? Uipitia changamoto gani maana najua lazima mlikuwa tofauti kila muda.!!

Wewe zichange change hizo pesa! Ukishazipata njoo kwangu we can talk business..!!

Woow'..!! Kupika? Naomba nikae nawe nikuwe nakutegea tegea kupika.!

And hell yeah, kuna thread moja ulisema unapenda sana kuchamba! Please add that to one of your hobbies..(joking)
Hapana kwakweli sijapata bahati ya kuishi na washkaji hata nilipokua shule boarding tunajikuta na marafiki tumekaa pamoja ila mara nyingi sinaga la kuchangia wanapokua wanaongelea vitu ambavyo wengi hupenda ku participate,najikuta too cool sina la kufanya.

changamoto kubwa asee ni ile kitu ambacho wanafunzi wenzangu tangu shule mpk vyuo kuwafanya wanione SPY na kwamba mimi ni mpeleka habari za mambo yao staff basi taratiibuu wakaanza kunitenga na kuwa mbali namimi,asee niliiishi maisha magumu sana,nadhani unapata picha "kutengwa" inakuaje unapokua kwenye sehemu mpo wengi.

Ghafla unaweza kwenda mahali watu walikua wamekaa wakikuona wanasambaratika wote,wasiposambaratka basi watageuka mabubu kimyaaaa,hiyo ndio changamoto yangu kubwa iliyotokana na kutoendana na wenzangu vitu vingi.

Acha nizichange nikizipata ntakuja sasa hapo kwenye kuzipata ndio sijuagi "inatakiwa umiliki kiasi gani" ndipo useme yes nimezipata,ungenisaida hapo kiduchu.

eeheee kutegewa kupika ni raha yani wewe just prepare for me mazaga zaga yote ntayokwambia yawepo then ukimaliza acha hapo mimi nikirudi ntakuja unganisha nitoe kitu inaitwa "msosi", ktk vitu wananishangaaa (kina nyie) ni linapokuja swala la hiyo sekta "usije nipikia ujinga aseee maana katka vitu simkwepesh mtu akikosea" ni apike chakula kibaya,tasteless asee nakuchana live kadhalika Ukipatia siwezi nyamaza lazima nikupe credit zako za kutosha sana.

hahaha kuchamba ooooh 🤭 🤭 hapana bana am not that much si wajua vile huku JF we do write n write some things are real while some are not,sema mimi nachamba bana😂😂 (staki ujinga kbsa)
 
Umeandika baada ya critical thinking, ni jambo zuri ila baadhi wataona tofauti. Lakini kupanga ni kuchagua na mtu huwezi kichagua matokeo ila unaweza kuchagua cha kufanya.
you're very right..!!
'Huwezi chagua matokeo ila unaweza chagua cha kufanya'..!!
Point well captured and noted.!
 
Mimi mchumba wangu ambaye ndo mke wangu leo miaka hiyo tukitoka hata kama mimi ndo nimesema twende akifika eneo la tukio bills tunachanga. Na hata sasa tukiwa home mishahara yetu ni ya familia siyo mtu anamiliki kila kitu. Kuna mahali ambapo na onyesha kama mimi ndo baba wa familia. Surprise [emoji44] za Hapa na pale lakini we enjoy life.

Shida watu wengi wanaishi maisha ya kucopy maisha ya watu.

Kuna watu eti wanasema mimi kama mwanaume naweza mkopa mke wangu hela. Wakati jukumu ninalo fanya ni la familia. Hapana hela ni ya familia ninapokuwa na jukumu namweleza mke wangu nini nataka kufanya tunasaidiana kutafuta hela kwaajili ya hiyo project. Sijawahi kujuta kumpata mke wangu.


Huyu kweli mimi nilipewa na Mungu. Na those days nilikuwa nasali sana rozari nipate mke mwenye feature kama zake. Mungu alinipa nilichotaka.
Hello guys,

Kwa wale wenzangu na mimi tunasema TGIF..!!

Naomba kuzungumza na waliopo ndani ya ndoa na wale wanaotarajia kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Kwenye mahusiano hasa ya uchumba, kuna hii tabia ya ndugu zetu wa kiume kutumia nguvu kubwa mno kutu-impress ladies kwa mitoko ya gharama, zawadi za bei ghali, shoppings za hapa na pale bila kusahau adventures - wenyewe wanaita kutu 'spoil'.

Hell yeah! Tumeumbwa kuwa wapokeaji we can't say 'No' to such offers and, in a meantime, tutawakubali tutakuwa nanyi sababu hiyo ndiyo aina ya maisha mliyotuonyesha na kutuaminisha kuwa we can live that life happily ever after.

Haha, picha linaanza baada ya kuwa mwili mmoja, ukishakubali kuishi kwa shida na raha mpaka pale kifo kitakapowatenganisha, hapo ndo wakati pekee utaujua uhalisia wa maisha ya mwenza wako..!!

Unaanza kuona mwenza wako kabadilika; mbona hakujali kama alivyokuwa anafanya wakati wa uchumba? Kwanini kila unachomuomba anasema hana pesa..!?

Dear ladies, sikatai kweli wapo wanaobadilika ila pia asilimia kubwa ya wanaume wengi wanakuwa wana-fake uhalisia wa kipato chao, hivyo ukija jumlisha na majukumu ya familia za pande zote mbili ni lazima mambo upande wao yawe magumu mno..!

Dear brothers,
Tunapenda sana kuwa spoiled na ninyi, ila tafadhalini sana msiishi nje ya budget wala uwezo wenu, muoneshe mchumba wako uhalisia wa maisha yako kabla hajasema 'Yes I do'. Uwe na uhakika na amani moyoni kuwa amekubali kuwa na wewe kwa hali yoyote ile uliyokuwa nayo, hebu msitunishe misuli mpaka mkachana mashati..!

Na ni muhimu mfahamiane vizuri kabla ya kuishi pamoja. Lazima umjue mwenza wako vyema, is she a good saver? Are you an extremely spender? Do both of you believe in debts? Mna assets gani? Mna mipango gani kwenye maisha yenu na je, budget yenu itakidhi na kuyafikia malengo yenu mkianza kuishi pamoja kama familia? Wewe una mshahara na yeye ana mshahara that's good and okay, lakini ni lazima mliweke hili sawa kabla ya kuishi pamoja. 'Ni changu changu, chako chetu' ama '50 by 50'..!!

Na mliopo kwenye ndoa jitahidini sana kuliweka hili sawa baina yenu, jifunzeni kuwa 'open' and 'honest' kwa wenza wenu linapokuja suala la 'waleti' zenu, ukweli na uwazi wa kipato chenu ndiyo utajaojenga msingi bora wa kuimarisha muhimili wa maendeleo ya familia imara! And don't forget that 'marriage is forever..!!

Utachagua mwenyewe kuishi huru ama kuishi katika 'kifungo huru'..!

''Money is one of the biggest thing couples do always fight about'' - Cary Siegel..!!

Tafakarini hili na mchukue hatua stahiki, Blessed Weekend Dears..!!
 
Mimi mchumba wangu ambaye ndo mke wangu leo miaka hiyo tukitoka hata kama mimi ndo nimesema twende akifika eneo la tukio bills tunachanga. Na hata sasa tukiwa home mishahara yetu ni ya familia siyo mtu anamiliki kila kitu. Kuna mahali ambapo na onyesha kama mimi ndo baba wa familia. Surprise [emoji44] za Hapa na pale lakini we enjoy life.

Shida watu wengi wanaishi maisha ya kucopy maisha ya watu.

Kuna watu eti wanasema mimi kama mwanaume naweza mkopa mke wangu hela. Wakati jukumu ninalo fanya ni la familia. Hapana hela ni ya familia ninapokuwa na jukumu namweleza mke wangu nini nataka kufanya tunasaidiana kutafuta hela kwaajili ya hiyo project. Sijawahi kujuta kumpata mke wangu.


Huyu kweli mimi nilipewa na Mungu. Na those days nilikuwa nasali sana rozari nipate mke mwenye feature kama zake. Mungu alinipa nilichotaka.
Lucky you..!!
Barikiwa sana mkuu.!!
Naomba hizi sifa zimfikie mkeo huko aliko.!
Zidi kumpenda, kumuheshimu na kumtunza, siku zote!!
 
Back
Top Bottom