Changamoto za kifedha baina ya wenza zinazidi kuongezeka

Changamoto za kifedha baina ya wenza zinazidi kuongezeka

Upo sahihi kwa upande ulioongelea haswa.

Nikuambie tu uhalisia kati ya wanawake 10 utawapata wawili usipofake kipato. Nitaenda mbali nikuambie ukishikilia misingi ya ukweli katika maisha idadi itapungua kati ya 10 utawapata wawili au mmoja.

Wanawake wanapenda maisha fulani (unayajua) usipowaonyesha wata compromise kwasababu fulani...hapa ndipo watakukubali.

Je, wataka tufe bila kamchezo?
 
Kinachotakiwa ni kuwa waaminifu mkiaminiana kwa asilimia 100%, na kwamba mume uwe wazi kwa kila jambo unalifanya kwa mkeo ikiwa ni pamoja na mkeo ajue mshahara wako ni kiasi gani.
Pia mke lazima mumeo ajua kila unalofanya na mume ajue mshahara wa mke wake pia. Na kinachotakiwa kufanyika hapo ni kwamba kila mume apatapo mshahara wake basi amkabidhi mkewe kwa mujibu wa neno Efeso 5:21-24 , na hapo kwa pamoja mtazipangia matumizi .
Au hata kama mume hatampa mkewe mshahara wake basi ahakikishe mkewe anajua ni kiasi gani mume amepokea au anapokea na hapo kwa pamoja mtapanga ni cha kufanya na kiasi gani cha kusave.
Hapo mke mwema atahakikisha hata mshahara wake anauingiza kwenye maendeleo ya familia vizuri tu na kufanya familia kuwa na lugha moja na amani iliyojaa furaha.
Mume ni kichwa, mke ni kiwiliwili, mke ndiyo amepewa mikono kwenye familia ili kwamba ndiyo msimamizi wa maendeleo yote ya familia kwa ujumla.
Ukisoma kitabu cha Yeremia 31:22, imeandikwa, Hata lini utatanga tanga ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani, " mwanamke atamlinda mwanamume".
Kwahiyo, ili wana ndoa wawe na ndoa bora yenye Upendo, furaha na amani sawa na 1Korintho 13:13.
Ni lazima wawe na mawasiliano mazuri muda wote kwenye kila jambo na hasa kuhusu fedha, kuwa wazi na mshahara wako kwa mwenzi wako , mthamini mwenzi wako kwanza kabla ya fedha. Kwa kufanya hivyo fedha haitavuruga ndoa yenu.
Pamoja na kwamba tunasema fedha ni jawabu la mambo yote lakini kwa yeyote anaye mcha MUNGU atamthamini mwenzi wake kwanza kabla ya yote.
Niwatakie jumapili njema.
Unfortunately, it doesnt work like that...

Ukutane na mtu muaminiane 100%?
 
Obviously watakuwa wana 1 na 2 so huo ugomvi umeenda tu kuongeza petrol kwenye moto! Hakuna kitu kigumu kama watu wawili wenye makuzi tofauti, misimamo tofauti, uwezo wa kufikiri tofauti, namna wana perceive mambo kwa utofauti uwaweke chumba kimoja halafu eti waishi kwa kuelewana, Ni ngumu mno!!
Vipi dogo
 
Upo sahihi kwa upande ulioongelea haswa.

Nikuambie tu uhalisia kati ya wanawake 10 utawapata wawili usipofake kipato. Nitaenda mbali nikuambie ukishikilia misingi ya ukweli katika maisha idadi itapungua kati ya 10 utawapata wawili au mmoja.

Wanawake wanapenda maisha fulani (unayajua) usipowaonyesha wata compromise kwasababu fulani...hapa ndipo watakukubali.

Je, wataka tufe bila kamchezo?
Hivyo unamaanisha Daby you gonna fake it till you make it,
Ukiamua kufake then jiandae ku face the consequences.!!

Kwahiyo ni bora upate 8 wasio sahihi kuliko 2 waliopo real??
 
Hello guys,

Kwa wale wenzangu na mimi tunasema TGIF..!!

Naomba kuzungumza na waliopo ndani ya ndoa na wale wanaotarajia kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Kwenye mahusiano hasa ya uchumba, kuna hii tabia ya ndugu zetu wa kiume kutumia nguvu kubwa mno kutu-impress ladies kwa mitoko ya gharama, zawadi za bei ghali, shoppings za hapa na pale bila kusahau adventures - wenyewe wanaita kutu 'spoil'.

Hell yeah! Tumeumbwa kuwa wapokeaji we can't say 'No' to such offers and, in a meantime, tutawakubali tutakuwa nanyi sababu hiyo ndiyo aina ya maisha mliyotuonyesha na kutuaminisha kuwa we can live that life happily ever after.

Haha, picha linaanza baada ya kuwa mwili mmoja, ukishakubali kuishi kwa shida na raha mpaka pale kifo kitakapowatenganisha, hapo ndo wakati pekee utaujua uhalisia wa maisha ya mwenza wako..!!

Unaanza kuona mwenza wako kabadilika; mbona hakujali kama alivyokuwa anafanya wakati wa uchumba? Kwanini kila unachomuomba anasema hana pesa..!?

Dear ladies, sikatai kweli wapo wanaobadilika ila pia asilimia kubwa ya wanaume wengi wanakuwa wana-fake uhalisia wa kipato chao, hivyo ukija jumlisha na majukumu ya familia za pande zote mbili ni lazima mambo upande wao yawe magumu mno..!

Dear brothers,
Tunapenda sana kuwa spoiled na ninyi, ila tafadhalini sana msiishi nje ya budget wala uwezo wenu, muoneshe mchumba wako uhalisia wa maisha yako kabla hajasema 'Yes I do'. Uwe na uhakika na amani moyoni kuwa amekubali kuwa na wewe kwa hali yoyote ile uliyokuwa nayo, hebu msitunishe misuli mpaka mkachana mashati..!

Na ni muhimu mfahamiane vizuri kabla ya kuishi pamoja. Lazima umjue mwenza wako vyema, is she a good saver? Are you an extremely spender? Do both of you believe in debts? Mna assets gani? Mna mipango gani kwenye maisha yenu na je, budget yenu itakidhi na kuyafikia malengo yenu mkianza kuishi pamoja kama familia? Wewe una mshahara na yeye ana mshahara that's good and okay, lakini ni lazima mliweke hili sawa kabla ya kuishi pamoja. 'Ni changu changu, chako chetu' ama '50 by 50'..!!

Na mliopo kwenye ndoa jitahidini sana kuliweka hili sawa baina yenu, jifunzeni kuwa 'open' and 'honest' kwa wenza wenu linapokuja suala la 'waleti' zenu, ukweli na uwazi wa kipato chenu ndiyo utajaojenga msingi bora wa kuimarisha muhimili wa maendeleo ya familia imara! And don't forget that 'marriage is forever..!!

Utachagua mwenyewe kuishi huru ama kuishi katika 'kifungo huru'..!

''Money is one of the biggest thing couples do always fight about'' - Cary Siegel..!!

Tafakarini hili na mchukue hatua stahiki, Blessed Weekend Dears..!!
Nyuzi bora ya mwaka
Ndo maana girlfriend wangu wakwanza alipenda sana out vitu vya kipekee
At that time sikua hata na Nazi
Nlimwambia ukwer kabsa siwezi ishi maisha ya watu wengine
Had ntakapomaliza malengo yangu
 
Na ndipo wengi wanapoingiaga mkenge.
Kwa wanawake na kwa wanaume.
Unahisi huyu ni wa kupita tuu, unaishi maisha ya kufake ukijua ni kwa muda mchache, siku zinaenda unajikuta umeshampenda.
Hapo umemzoesha kwamba wewe maisha kwako ni super na kila kitu.
Haha..!!
Hizo situation zipo sana, hasa kwa wanaume, wanajifanya huyu dada ni wa kupita tu, mwisho wa siku wanajikuta they've fallen on that trap!!
Inabaki 'hilo ni chaguo lako'..!! 😂 😂
 
Hatuwez kuwafahamisha maana tukifanya hvyo mtatukataa.......
N mwendo wa kufeki tu,Kama utaujua ukweli ukiwa ndoani n juu yako ukae au usepe but najua hutasepa
Kitu pekee kitajenga ndoa bora, ni 'Ukweli' na 'Uaminifu' pekee.!!
 
Kinachotakiwa ni kuwa waaminifu mkiaminiana kwa asilimia 100%, na kwamba mume uwe wazi kwa kila jambo unalifanya kwa mkeo ikiwa ni pamoja na mkeo ajue mshahara wako ni kiasi gani.
Pia mke lazima mumeo ajua kila unalofanya na mume ajue mshahara wa mke wake pia. Na kinachotakiwa kufanyika hapo ni kwamba kila mume apatapo mshahara wake basi amkabidhi mkewe kwa mujibu wa neno Efeso 5:21-24 , na hapo kwa pamoja mtazipangia matumizi .
Au hata kama mume hatampa mkewe mshahara wake basi ahakikishe mkewe anajua ni kiasi gani mume amepokea au anapokea na hapo kwa pamoja mtapanga ni cha kufanya na kiasi gani cha kusave.
Hapo mke mwema atahakikisha hata mshahara wake anauingiza kwenye maendeleo ya familia vizuri tu na kufanya familia kuwa na lugha moja na amani iliyojaa furaha.
Mume ni kichwa, mke ni kiwiliwili, mke ndiyo amepewa mikono kwenye familia ili kwamba ndiyo msimamizi wa maendeleo yote ya familia kwa ujumla.
Ukisoma kitabu cha Yeremia 31:22, imeandikwa, Hata lini utatanga tanga ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani, " mwanamke atamlinda mwanamume".
Kwahiyo, ili wana ndoa wawe na ndoa bora yenye Upendo, furaha na amani sawa na 1Korintho 13:13.
Ni lazima wawe na mawasiliano mazuri muda wote kwenye kila jambo na hasa kuhusu fedha, kuwa wazi na mshahara wako kwa mwenzi wako , mthamini mwenzi wako kwanza kabla ya fedha. Kwa kufanya hivyo fedha haitavuruga ndoa yenu.
Pamoja na kwamba tunasema fedha ni jawabu la mambo yote lakini kwa yeyote anaye mcha MUNGU atamthamini mwenzi wake kwanza kabla ya yote.
Niwatakie jumapili njema.
Umeongea ukweli mtupu mkuu,
Mungu akubariki sana!! Naamini wengi watakuwa wamejifunza katika ujumbe wako.!! 'Mwenye sikio na asikie'..!!
Blessed up yakobo11..!!
 
SweetieLee,
Nadhani umeongelea michepuko si wachumba! Hakuna mwanaume atakayefake kwa mchumba sana sana ataonesha hana kitu wakati anazo.
Njinjo, usiwe mbishi, mtoa Mada yuko sahihi kabisa, ni kweli wanaume wengi hupenda kujifanya wana uwezo wakati wanapovizia msichana wakati huu ataitwa mchumba, na kujitahidi kumuonesha kwamba wana maisha standard ili tu dada wa watu akubali, akishamuoa tu ndio sasa anaanza kuishi maisha yake halisi, wapo wengine huazima hata gari ili kumdanganyia mdada, mwingine anakopa pesa ili mdada amuone anazo kumbe kauzu na kapuku
Kwa mdada makini ni rahisi sana kugundua kwamba huyu mwanaume anaigiza,
Kwenu wadada,
Ukitaka kumjua mtu mwambie akupeleke kwao kabla hajakuoa, kwani maisha ya kwao yatakupa picha halisi ya hali yake,
Sio mnakutana huko mjini sijui Beach na wewe unajidanganya unadhani Beach ndio nyumbani kwake, ukimuona na gari angalia Kadi ya gari imeandikwa jina gani, mtu anaazima gari anakuja kukuzuga na wewe unakimbilia kupanda,mtu akikupeleka kwenye maeneo ya stareheo ya kataa, mwambie mimi sio mdori, mtakuwa mnalizwa kila siku, kaeni hapo sasa.
 
Back
Top Bottom