Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,273
Kila biashara ya rejareja Ina changamoto zake. Biashara ya nyumba za kupanga pia ina kero zake. Unapojenga nyumba ya vyumba sita na kuipangisha chumba kimoja kimoja ni rahisi kupata wateja. Ni bahati sana kukuta vyumba viko wazi unatafuta mteja kulinganisha na kupangisha nyumba nzima.
Katika kuboresha biashara, kama una uhakika wa maji, weka Indian toilet mbili, hii itasaidia foleni asubuhi. Unawafahamisha kabisa kuwa choo kikiziba kwa vitu kama tampons gharama za uzibuaji wanalipa wao. Maji unaweza kuvuna ya mvua pia kusaidia usafi wa chooni hasa Dawasa kukiwa na shida.
Changamoto, ni kuwa unakusanya watu wa aina tofauti, jiandae kuwa hakimu. Kuna kesi moja, mama wa watu anapika maharage kwenye jiko la mkaa, msela alikua ana mlima timing, mama ameingia ndani kwake msela amechota maharage ya watu. Kesi za uchawi usiombe na nyingine kuibiana mabwana.
Hii biashara haiumizi kichwa sana, vyumba sita kila kimoja 50,000. Una uhakika wa 300,000 kwa mwezi.