Changamoto wanazopitia wachawi wanapotaka kukuroga

Changamoto wanazopitia wachawi wanapotaka kukuroga

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,256
Uzi mfupi**

Wachawi wanapatia changamoto nying wanapotaka kukuroga, kwanza inabidi atafute pesa ya kununulia Vifaa Vya kazi
Kununua Vifaa Vya kazi ni gharama kubwa na Muda mwingine itamlazimu kusafiri ata nje ya Mkoa ili akanunua kifaa icho cha kukurogea

Kwa mfano Kuna uchawi mwingine ili ufanyike mchawi ataitaji maji ya maiti
upatikanaji wa maji ya maiti ni mgumu sana,

Yani inabidi uwe na koneksheni ya kufa mtu ili upate maji ya maiti na maana muda mwingine unaweza uziwa maji feki
Kwaiyo katika hali kama iyo mchawi inabidi atoe pesa ndefu ili kufanikiwa

Mchawi ni mtu mbishi sana yana hakubali kushindwa kabisa
Kitu ambacho kinamuumiza sana mchawi ni pale anapotumia nguvu nying kukuroga alafu ww unaleta dharau

Yani yeye anapokuroga anataka kuona matokeo yani anataka kukuona umepaniki
Mchawi Anaskia raha sana pale anapoona kwamba umepaniki alafu umekimbilia kwa mganga

Changamoto kubwa kwa mchawi ni kuona kwamba badala ya kupaniki lakini ww ukamua kufanya ibada yan ukasimama na MUNGU
Mda mwingine mchawi inabidi akijifunze teknolojia ambayo itamsaidia kukuroga

Hapa inabid aende kozi iyo maalumu na inabidi alipie pesa kwa ajili ya kupata utaalamu
Upatikanaji wa Vifaa Vya kurogea imekuwa changamoto kubwa kwa Wachawi

Maana katika maduka ya kawaida ya asili havipatikani
Madalali wanaouza Vifaa Vya kurogea wamekuwa wakiwauzia wachaw Vifaa ivyo kwa bei juu sana

Kwa mfano mchawi ili aingie kwako lazima awe na testa ili aone kama kuna mtego au hamna
Testa ya kichawi inauzwa bei juu sana maana bila ya testa unaweza jikuta unaingia mtegoni

Kama ulishawai ona mchawi Kanasa juu ya bati au ameanguka basi jua uyo ameingia bila testa
Wachawi wanatumia pesa nyingi sana kununua Vifaa Vya kurogea pande za mahospitali na makaburini

Mara nyingine mchawi anajikuta anamadeni mengi sababu anataka afanikiwe kukuroga
Akishakuroga itambidi afatilie mara kwa mara maendeleo yako ili aone kama uchawi unafanya kazi

Muda mwingine inabidi afanye update yani kama vile Ana update windows

Asanteni
IMG_20200702_184440.jpg
 
Kwa mfano mchawi ili aingie kwako lazima awe na testa ili aone kama kuna mtego au hamna
Testa ya kichawi inauzwa bei juu sana maana bila ya testa unaweza jikuta unaingia mtegoni

Kama ulishawai ona mchawi Kanasa juu ya bati au ameanguka basi jua uyo ameingia bila testa
Wachawi wanatumia pesa nyingi sana kununua Vifaa Vya kurogea pande za mahospitali na makaburini

Muda mwingine inabidi afanye update yani kama vile Ana update windows

AsanteniView attachment 1495584
Aisee nimecheka hapo anapo update windo zake
 
Afrika sisi yaani bado sana. Wenzetu walivuka hii steji zamani karne sijui ya ngapi huko na sasa wamebaki kufanya haya mambo kama hobby tu ya watu wachache wachache na vi society na vi cult vyao huko lakini sisi kabisa kabisa ndiyo mfumo unaoendesha maisha ya jamii. Bado saaana !!!
 
hata mimi nimecheka pale aliposema wachawi wanakwenda kupata training za kuji update kama watu wa IT/programming.
Na pia alinichekesha pale aliposema kuna vifaa vingine huwezi kuvipata hadi uwe na connection,na lazima uwe na tester kabla ya kwenda kuroga.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ila jamaa vitu alivyoviandika ni vya ukweli,kuna majirani zetu uswahilini ni wachawi wana hizo tabia zote jamaa alizozitaja
Aisee nimecheka hapo anapo update windo zake
 
Nasubiri ushuhuda kutoka kwa wenye fani zao hapa [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Kitu gani cha kuweza kujikinga na hawa wachawi maana naona maombi pekee hayatoshi. Japo siamini kama uchawi upo.
 
Mkuu acha kuingilia fani za watu,mchawi ni tasisi kubwa kama ilivyo kwa taasisi za serikali,

Eti akitaka kukuloga hadi akanunue vitu,are you sure?

Story za vijiweni mbaya sana

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Naelewa uchawi u po lkn waumini wake wananiudh san. Unakuta mtu anakufata eti umerogwa, nenda kwa mtaalamu. Maanina
 
Back
Top Bottom