Changamoto nilizokutana nazo jimboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changamoto nilizokutana nazo jimboni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge wa CCM, Mar 24, 2010.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za siku nyingi ndugu wanaJF

  Nimefanya safari nyingi sana ndani ya jimbo langu la uchaguzi ninalodhamiria kugombea na paoja na mambo mengine nilitangaza rasmi dhamira yangu hiyo. katika safari hizo nilijionea mengi sana yanayoashiria kuwa bado tuna kazi kubwa mbele yetu katika kufikia maendeleo ya kweli na endelevu. moja ya changamoto za wazi ni pamoja na:

  1. Umasikini
  2. Mipango mibovu ya maendeleo
  3. Ushiki duni wa wanachi
  4. Kukata tamaa
  5. Ukosefu wa fursa zana na mitaji ya kifedha
  6. Uharibifu wa mazingira
  7. Magonjwa
  8. Nk.

  Nafurahi kusema kuwa niliungwa mkono na wananchi kwa kiasi cha kunipa Uhakika wa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa bunge licha ya mbunge wa sasa naye kutangaza azma ya kutetea kiti chake.

  Bila kuficha, hali ya mambo ilivyo huko jimboni, ni wazi hakuna anyeweza kunipinga na kunishinda. Kwa upande wangu nimekwishaanzisha ushirikiano na wanachi katika kukabili changamoto mbalimbali za kujiletea maendeleo kama:


  1.
  Kuanzisha mifuko midogomidogo vijijini itakayotoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake

  2. Kuanzisha miradi ya maji vijijini kwa kuchinba visima vifupi na virefu vinavyotumia vifaa vya upepo na umeme-jua
  3. Kudhamini mikopo ya baiskeli kwa vijana wajasiriamali
  4. Kuanzisha vikundi vya ushirika wa kilimo, ufugaji na viwanda vidogovidogo
  5. Nk.

  Mipango yote hii iko katika hatua mbalimbali za maandalizi na mingine tayari imeanza kutekelezwa.

  Hakuna lisilowezekana, Licha ya sheria mpya ya gharama za uchaguzi na kanuni zake kutoeleweka vizuri kwa wengi, sisi tumeanza kupiga hatua kwa uangalifu mkubwa na bila kuvunja sheria mpya, wakati tukisubiri chama kizindue rasmi mchakato tuakamalize kazi.

  Nitafurahi pia kama nitapata michango ya mawazo ya nini cha kufanya au kuboresha zaidi kule jimboni kwa manufaa ya wananchi na taifa letu kwa ujumla.

  Bado kidogo tu, ushindi ni dhahiri
  KIDUMU CHAMA CHA MAPIMDUZI
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Jimbo gani? Mkoani Kilimanjaro?
   
 3. K

  Kijunjwe Senior Member

  #3
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ...Jina lako siri? Jina la Jimbo kapuni? Sasa tutakusaidia vipi?
  Tafadhali weka bayana japo tujue jimbo gani ili tukupe mikakati itakayo endana na jimbo lako Mfn. jimbo la wakulima au wafanya biashara, jimbo la wafugaji na vinginevyo.

  Labda pia ungesema kwa nini umeamua kutoa michango ya kimaendeleo katika jimbo lako kipindi hiki cha uchaguzi na sio kabla ya hapa.
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  .....ngoja tusikuharibie zaidi......ila ningekuwa mpiga kura wako......hungepata kura yangu ng'ooooo! u know why?
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Yaani...we acha tu! Siasa zinafurahisha sana kuzifuatilia.
   
 6. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Hilo jimbo linaweza kuwa la kufikirika hukoa Marekani.

  Kuna mama mmoja mheshimiwa sana wa kule mkoani Kilimanjaro ndio huwa anaongea mambo karibu na hayo. Huyu mkulu atakuwa na uhusiano naye tu.
   
 7. p

  pori Member

  #7
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bora kama umeona mbali ktk kunufaisha (kimaendeleo) jimbo lako usilopenda kulitaja. maendeleo ya jumuia ni sawa lakini angalia, wapiga kura wengi hutegemea wakichagua mbunge basi hudhani ana miujiza ya kutimiza kila shida binafsi k.v kulipia ada watoto,kutoa nauli za safari, n.k. nadhani hii inachangia kwa wabunge wengi kukwepa majimbo yao mpaka uchaguzi unapokaribia. wapiga kura tuangalie hilo, tusiwakimbize wabunge wetu.
   
 8. B

  Big Dady Member

  #8
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana, chama chenyewe unachogombea cha mafisadi, hata ukiwa na sera nzuri namna gani watakuziba tu. Utabaki kudumisha CCM na sio taifa lako. Ukombozi wa kweli hautapatikana kamwe kupitia CCM.
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kweli dhamira yako inaweza kuwa safi sana ila chama ulichopo sio kabisa ukitaka mabadiliko badili pia na mazingira mabovu yalokuzunguka kwanza ndio dhamira yako inaweza kuwa safi na kabla ya uchaguzi akikisha yote uloaidi umeyatekeleza hapo uitaji ata kampeni wakati mpinzani wako yupo bze kujinadi majukwaani ww tekeleza ahadi zako kwa wananchi yani watakupa jimbo milele
   
 10. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwanza nakupongeza sana kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge kwenye hilo jambo....ila mpaka sasa umeshakiuka kanuni za ccm kwa wagombea watarajiwa, kikanuni kama unataka kugombea unatakiwa ufike ofisi za chama na kutangaza nia yako kwa viongozi basi, huruhusiwi kupita jimboni kupiga kampeni na kuanza kutoa misaada na ahadi kwa wananchi.
  Hiyo ni rushwa na kishawishi, muache mbunge aliyeko afanye kazi zake na akamilishe muda wake wakuwatumikia wananchi....na kuhusu hii kanuni mpya ya gharama za uchaguzi...umeumia kabisaaaa.
  Kama unania ya kusaidia wananchi ngoja utakapochaguliwa ndio ujitolee hayo yote kupitia kanuni za chama....

  Kuwa muangalifu ndugu....ila pia ni bora ukaweka wazi jimbo na jina ili usaidiwe hapa, maana kuna watu wanataalifa za majimbo huwenda wakakusaidia....
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Back again?
  Tunashukuru kwa kuja kuleta MREJESHO!
  uLIPOTEA SANA mKUU!
   
 12. bht

  bht JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  HAHAA
  Cousin nilijua huku lazima nikukute, yaani huyu jamaa huyu dah basi tu.......
   
 13. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa ni pamoja na kusoma wakati. Ukishindwa hilo huwezi siasa.

  Nawashukuru jamani kwa shauku ya kulijua jimbo na mengineyo, wakati muafaka ukifika mtalijua tu.

  Asanteni kwa mawazo mazuri, mbarikiwe
   
 14. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu, hujaelewa bado?

  pamoja na matatizo tuliyonayo katika jamii yetu, wewe yale maandishi ndiyo yanayokutisha zaidi. kama umejiandikisha kupiga kura umefanya vyema sana. hamasisha na wengine.
   
 15. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu umeongea kitu kikubwa a muhimu sana. niliguswa sana na tabia mbaya ya wabunge wengi kusaidia majimboni kutoka mifukoni mwao, sasa mimi nimeanza kutayarisha mfumomsingi wa uchumi wa mtu mmojammoja na jamii kwa ujumla, naamini tutafanikiwa. hamasa iliyoonyeshwa pamoja na ushiriki vimenitia moyo san. ubarikiwe.
   
 16. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pori, bigdady na drphone, nawashukuru kwa maoni yenu. ccm si mbaya. imani, malengo na madhumuni yake ndiyo msingi wa falsafa zote za kisiasa kwa sasa hapa tanzania na zinaongoza zile za vyama vingine vyote. pia siasa ya ccm ndiyo siasa pekee hapa nchini mimibinafsi ninaweza kuitetea, siasa zingine wapo wanaozitetea na nakubali wanafanya vyema na vizuri.

  nakiri kuna matatizo katika ccm kama katika vyama vingine na hili haliepukiki kila palipo na mfumo unaosimamiwa na wanadamu. tiba yake si kukimbia, bali kukabili. mimi nimeamua kukabili. ni suala la wakati tu, na matunda yataonekana.

  ndugu yangu nikuhakikishie kuwa sijavunja kanuni wal taratibu zozote za kichama wala za kisheria ikiwemo hilo ulilogusia la rushwa. niko makini sana. siasa si kitu cha kukurupuka. umakini wa hali ya juu sana unahitajika. mimi na timu yangu tumejipanga vizuri na hatuna shaka na ushindi kwani tuna nguvu ya umma nyuma yetu
   
 17. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nami nashukuru kuwakuta mnaendeleza ulingo wa mijadala yenye manufaa makubwa. nitaonekana kwa kitambo na nitapotea tena. kwa sasa niko safarini na nitarejea tena jmboni kuendeleza mikakati ya ushindi.
   
 18. R

  Renegade JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Ndugu mwanasiasa, mimi siamini sana katika siasa kwa sababu najua ni utapelitapeli, nataka kujua kitu kimoja kutoka kwako kuwa wewe kama wewe nani anakufadhili?
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa kugombea kupitia hapa unawadanganya wapiga kura wako.
  Na wewe unataka ukavimbishe tumbo bungeni porojo tu huwezi leta mabadiliko jimboni kwako ndani ya chama cha mafisadi kama umedhamiria kuwakomboa wananchi wako hama chama utakuwa mzalendo wa kweli.
   
 20. R

  Renegade JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  We unagombea halafu usemi Jimbo gani? halafu unakataa kutaja jina lako!!, are you serious? ni kweli unataka kura zetu? Sisi ndio wapiga kura wako. Shauri yako.
   
Loading...