CHAN2021: Mchezo umemalizika kwa Taifa Stars kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zambia

Kocha hana uzoefu,wachezaji hawana uzoefu......kwa mechi ya leo tungekuwa na key players wa Tz,inawezekana tungeweza kufungwa ila siyo kijinga hivi hivi.

Timu yangu ambayo ingeleta ushindani leo

Kaseja/Manula Golini yeyote

Kapombe

Yassin

Nondo

Nyoni

Mkude(dunia nzima watukutu wapo)

Kaseke

Sure boy/Fei toto

Nchimbi

Mzamiru

Farid

Sub.Nado,Manyama,Lusajo,Kaseja,Muhilu,Tshabalala,Yondani (pressure ikizidi anaingia),Mudathiri,Boko,Nyoso,Dilunga

Hiyo timu angalau tungeleta upinzani

Tz wachezaji wa Simba,Azam na Yanga wanacheza mechi nyingi kuliko wachezaji wote WaTz,hawaepukiki
 
Taifa stars imeanza vibaya huko Cameroon dhidi ya Zambia kwa kulala 2-0.
Nadhani rais atatekeleza ahadi Yake ya kutumbua waziri wa michezo ingawa hakucheza.

===

#CHAN2021 Mchezo umemalizika kwa Taifa Stars kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zambia.

Zambia 2-0 Tanzania
Sikombe 64' (P)
Chabula 81'

View attachment 1681489
Tanzania katika ubora wake
 
Tunarudi home maana hawa Guinea tayari Wanaongoza 1,na kwa ukimeo wa timu yetu sidhani kama tunaweza kupata hata sare..........labda kocha abadirike
 
Man of the match ni Collins kombe, nadhani Sasa Simba na yanga wataanza kumsaka Kama kawaida yao.
Ile game ya Taifa Stars na Burundi ambapo yule Mzee Ntibazonkiza kutufunga wale Jamaa wa Jangwani hawakumuacha, na huyu Chabula kufunga bao la pili sidhani kama ataachwa.
 
Kwa jinsi timu inavyocheza, mbinu za kocha wetu jumlisha na uzembe kupitiliza wa wachezaji wetu, nachelea kusema sidhani kama tutapata hata point 1 kwenye group letu.

Soka la Tanzania, bila ya wachezaji wa kigeni ni bure kabisa. Leo Taifa stars wamecheza kama Mbao Fc.

Ni wakati sasa wa kwenda kumuomba msamaha mzee Mwinyi kabla hajatangulia, msemo wa kichwa cha mwendawazimu unaendelea kututesa sana!
Mkuu kauli za wanasiasa na masilahi binafsi ya viongozi wa mpira wa miguu hapa nchini ndio sababu kubwa ya hii team kufanya vibaya.
Kocha anataka kuwaridhisha wana siasa na baadhi ya watu kwa maslahi ya wachezaji wao kwa kutumia kivuli cha kukuza vipaji vipya.

Ukweli ni kwamba sisi Chan mwaka huu hatujapeleka team ya ushindani bali tumepeleka team ya majaribio kwenda kukuza vipaji na matokeo yake ndio haya tunayaona sasa na nakubaliana na wewe kuwa hatutapata hata pont 1 kwenye haya mashindano kamwe.

Huwezi kuacha wacheji wazoefu wote nyumbani na hata hao wachache ulio wachukua bado unawaweka bench kwa makusudi kabisa mfano mabao yote mawili makosa yalianzia katikati pale kwa baraka Majogoro Kisha cross ikapigwa pembeni kushoto kule kwa Manyama inakuja kwenye box Kapombe anajitahidi kuokoa hadi ananawa mpira, Goli la pili napo vile vile ni kule kule kushoto mtu kapiga cross jamaa anaunganisha mpira kambani.

Katikati pamekufa kabisaa ajabu Ndemla yuko bench pale hapewi nafasi, viungo wa Kati wazuri kabisa Kama Mzamiru, Sure boy, Frank Domayo na Mkude wameachwa kwa makusudi kabisa.

Kule mbele ndio kabisaa, yani unamuweka bench Faridi Musa alafu unamuanzisha Mhiru ambae hata ball control nzuri hana, Kama haitoshi tumewaacha mawinga wazuri kabisa huku Nyumbani Kama Iddi Nado na Hassani Dillunga kisa tunataka kukuza vipaji!!!

Nchimbi unamuweka mbele na Lyanga heti ndio wawe wafungaji huku huyu nchimbi hata tu kwenye team yaka hapati nafasi ya kucheza anakaa bench tangu msimu wa ligi imeanza hajafunga goli hata moja alafu eti ndio tunategemea akatupe matokeo CHAN.

Wacha tu tufungwe sababu tupo kwenye majaribio ya kikosi na si kushindana.
 
Back
Top Bottom