CHAN2021: Mchezo umemalizika kwa Taifa Stars kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zambia

Kocha wa stars ni mzuri sana tatizo lipo kwenye ligi ambayo wachezaji wanaocheza ni wageni kutoka nje ya Tanzania sasa unafikiri utapata wachezaji wa aina gani kwenye timu ya taifa?
 
Kocha wa stars ni mzuri sana tatizo lipo kwenye ligi ambayo wachezaji wanaocheza ni wageni kutoka nje ya tanzania sasa unafikiri utapata wachezaji wa aina gani kwenye timu ya taifa?
Uzuri wake ni upi?
kumchukua Baraka Majogoro kama kiungo na kuwaacha MKUDE, MZAMIRU, DOMAYO na SURE BOY
 
Kuna msemo kwamba, kuna watu wakiwa na nyundo, wanafikiri tatizo lolote ni msumari, walimalize kwa kugonga kwa nyundo...
Kutumbua makocha kila siku hakujazifanya simba au Yanga kuwa timu bora kama TP Maembe au AS Vita. Hivyo ni muhimu jiwe aelewe kwamba kutumbua tumbua watendaji wake ni mbwembwe tu na haiongezi ufanisi wa serikali
 
Wakati mpira wa Zambia vs Tanzania unaendelea nikasikia commentary anasema "Baada ya Micho kuita kikosi chake Cha CHAN wadau wengi wa soka Zambia walimkosoa kwa kuacha baadhi ya wachezaji, kitendo ambacho kilipelekea Micho awambie wadau wa soka Zambia waite kikosi chao wao ili ipigwe friendly match na kikosi chake, baada ya hiyo mechi Micho aliwaongeza wachezaji wa 5 kwenye kikosi chake kutoka kikosi hicho cha wadau wa soka"....
Jamani Ndariyigije sio mjinga......nchi hii tunatekekeza amri ya mtu mmoja tu....kwani mmesahau alisema Nini kuhusu Timu ya Taifa majuzi!?
 
katika suala la mchezo wa mpira wa miguu Tanzania bado tunatatizo ambalo halijatatuliwa, kila nikiangalia mechi za kimataifa tunapwaya kabisa.

hivi bado hatuna academy.....??, wachezaji wetu wengi wanacho kikosa ni "skills, miaka mingi sasa imepita sijui kuna mikakati gani ya kuwa na timu ya taifa yenye ubora wa viwango vya kimataifa.

inasikitisha hata mimi nisiye jua mpira naona madhaifu ya timu yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutumbua makocha kila siku hakujazifanya simba au Yanga kuwa timu bora kama TP Maembe au AS Vita. Hivyo ni muhimu jiwe aelewe kwamba kutumbua tumbua watendaji wake ni mbwembwe tu na haiongezi ufanisi wa serikali
JPM yeye kila kitu anajua... kuna watu walipongeza madudu aliyoongea kuhusu timu ya Taifa.
 
Jamani Ndariyigije sio mjinga......nchi hii tunatekekeza amri ya mtu mmoja tu....kwani mmesahau alisema Nini kuhusu Timu ya Taifa majuzi!?
Ettiene akirudi asepe tu.. analeta uoga kwenye kazi kisa Rais kasema
 
Kwa jinsi timu inavyocheza, mbinu za kocha wetu jumlisha na uzembe kupitiliza wa wachezaji wetu, nachelea kusema sidhani kama tutapata hata point 1 kwenye group letu....
Point moja kuipata labda kwa sare ya bilabila, tumuombe mungu atusaidie kwa kweli
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom