Chama Kipya cha Siasa Kusajiliwa

Chama Kipya cha Siasa Kusajiliwa

jnuswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,270
Reaction score
549
Mh. Dr. Slaa katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwa Iringa amesema wamebariki madiwani 2 walioomba kujiuzulu Shinyanga, hiyo ndiyo Demokrasia ya kweli, madiwani hao moja ya sababu kubwa ya kujiuzulu ni kwamba wanamuunga mkono Mh. Zitto , Mh. Dr. Slaa amesema kuna taarifa pia kuwa chama cha ACT kiko mbioni kusajiliwa na baadhi ya wale waliovuliwa uanachama CHADEMA.

Kama ni kweli chama hicho kitasajiliwa na viongozi wake ni miongoni mwa waliovuliwa uanachama CHADEMA, basi Dr. Kitila Mkumbo atakuwa ni mtu wa kuogopwa kama UGONJWA WA KUFISHA, ataogopwa na kizazi kilichoshuhudia usaliti wake na kizazi kitakacho kuja kuzaliwa na kusimuliwa kisa hiki.

Kama watafanya kosa hilo la kusajili chama hicho , natabiri wakiweza kupata wanachama hata elfu kumi kwa nchi nzima basi ntajua watanzania wengi hatunazo akili. Dr. Kitila amekuwa akinukuliwa na magazeti baada ya usaliti wake kukwama na kuvuliwa uanachama akisema tunahitaji chama mbadala cha upizani zaidi ya CHADEMA kumbe malengo yake yalikuwa ni hayo. Huyu mtu ni msomi mzuri lakini nashawishika kusema siasa sio mahali pake alikosea njia, na kama ni mahali pake basi anauchu mbaya sana na tamaa ya madaraka.

Tunahitaji kuikomboa Tanzania kwa kuiondoa CCM madarakani
 
kwani aliyeonewa ni kitila peke yake hadi umlaani hivi? kwani ukombozi utaletwa na chagadema peke yake? wakati chagadema yenyewe inakandamiza demokrasia kwa kuendekeza uhafidhina?
 
ullichokiandika hakiendani kabisa na kichwa cha habari. inaonekana wazi kabisa kwamba umevurugwa.
 
Mkuu mbona kama habari yako ni TETESI tu, halafu habari yako haijabeba vizuri KICHWA CHA HABARI.
Ni kweli ni tetesi lakini naamini taarifa inayotolewa kwenye vyombo vya habari ambavyo vina wataalam zinakuwa na ukweli, hiyo nimeisoma kwenye gazeti la leo
 
Badala ya kufungua makampuni ya kuwekeza hasa kwenye KILIMO na UFUGAJI, watu kila siku na madegree yao ni kufikiri kufungua vyama vya siasa tu -- KUNA BIASHARA GANI HUKO????

ruzuku, huoni slaa na mbowe wanavyopiga?
 
Tumefikaje hapa?
Nchi hiii inahitaji mjeshi mmoja aje akae magogoni walau kwa miaka 2 tujifunze kidogo. Hii democracy ni kansa inayokula akili za watu. Badala ya kufanya kazi wanasubiri kunyoshewa vidole then waanze kufaidi.
 
Ni kweli ni tetesi lakini naamini taarifa inayotolewa kwenye vyombo vya habari ambavyo vina wataalam zinakuwa na ukweli, hiyo nimeisoma kwenye gazeti la leo

gazeti la udaku la tanzania daima la mbowe?
 
ullichokiandika hakiendani kabisa na kichwa cha habari. inaonekana wazi kabisa kwamba umevurugwa.
ugonjwa wetu mkubwa watanzania ni uvivu wa kusoma tunapenda kusoma neno moja tukijitahidi sana mstari mmoja
 
slaa amechuja, amebaki kuweweseka tu. chama kinamfia amebaki na matamko yasiyo na tija. hadi mwaka huu uishe atakuwa amebaki yeye na mbowe peke yao.
 
ugonjwa wetu mkubwa watanzania ni uvivu wa kusoma tunapenda kusoma neno moja tukijitahidi sana mstari mmoja

huo ni ugonjwa wako usiwatupie watu wengine. halafu ww sio msemaji wa watanzania
 
ni kweli hicho chama kipo na bwana kabwe ndio muasisi wake, kinaitwa Alliance for Change and Transparence. nimeiona kadi yao ya uanachama in rangi ya zambarao kama jezi za mbeya city. juzi juzi tu hapa kigoma uliwaka moto baada ya wafuasi wa chama hicho kutaka kupandisha bendera yao kwenye tawi la chadema la urusi (kwa wanaoijua kigoma watakuwa wanakijua kijiwe cha chadema cha urusi) ndipo wanaharakati wa chadema walipozuia upuuzi huo mpaka polisi waliingilia kati
 
basi niseme ni ugojwa wako wewe , mbona heading na contents vinaendana, na wenzako wameelewa kilicho andikwa au ndo zile shule zetu za Kata ?
 
Mh. Dr. Slaa katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwa Iringa amesema wamebariki madiwani 2 walioomba kujiuzulu Shinyanga, hiyo ndiyo Demokrasia ya kweli, madiwani hao moja ya sababu kubwa ya kujiuzulu ni kwamba wanamuunga mkono Mh. Zitto , Mh. Dr. Slaa amesema kuna taarifa pia kuwa chama cha ACT kiko mbioni kusajiliwa na baadhi ya wale waliovuliwa uanachama CHADEMA.

Kama ni kweli chama hicho kitasajiliwa na viongozi wake ni miongoni mwa waliovuliwa uanachama CHADEMA, basi Dr. Kitila Mkumbo atakuwa ni mtu wa kuogopwa kama UGONJWA WA KUFISHA, ataogopwa na kizazi kilichoshuhudia usaliti wake na kizazi kitakacho kuja kuzaliwa na kusimuliwa kisa hiki.

Kama watafanya kosa hilo la kusajili chama hicho , natabiri wakiweza kupata wanachama hata elfu kumi kwa nchi nzima basi ntajua watanzania wengi hatunazo akili. Dr. Kitila amekuwa akinukuliwa na magazeti baada ya usaliti wake kukwama na kuvuliwa uanachama akisema tunahitaji chama mbadala cha upizani zaidi ya CHADEMA kumbe malengo yake yalikuwa ni hayo. Huyu mtu ni msomi mzuri lakini nashawishika kusema siasa sio mahali pake alikosea njia, na kama ni mahali pake basi anauchu mbaya sana na tamaa ya madaraka.

Tunahitaji kuikomboa Tanzania kwa kuiondoa CCM madarakani

1. mnahitaji kuikomboa tanzania
2. mnahitaji kuiondoa ccm madarakani.........................
tafsiri ya sentensi hizo ni kwamba

1. mnawalaghai watanzania kuwa nyie ni wakombozi kumbe mna uchu wa madaraka hata kwa kumwaga damu
2. lengo lenu ni kuiondoa ccm, kipenzi cha watanzania, sio kuikomboa nchi ambayo imekombolewa mwaka 1961
3. rejea maneno ya kitila kuwa ni heri mkoloni mweusi (ccm) kuliko mkoloni mwekundu (chadema).
NB MALENGO YENU BATILI HAYATAFANIKIWA KAMWE.
 
Zitto kaponza vijana wengi sana huku yeye akiendelea kupeta kaua ndoto za vijana kisiasa

Mtaishia kumlaumu mkombozi kwa kuwatetea wahafidhina. wenye akili timamu wamejitambua wakatumia akili zao kufanya maamuzi mmebaki misukule wachache mki brush viatu vya wahafidhina.
 
basi niseme ni ugojwa wako wewe , mbona heading na contents vinaendana, na wenzako wameelewa kilicho andikwa au ndo zile shule zetu za Kata ?

mimi nakushauri uache kutumia kichwa kufugia nywele peke yake. utakosa mengi. ndio nyie mnaokaa vijiweni mkisubiri maisha bora yawafuate hapo mlipo.
 
ni kweli hicho chama kipo na bwana kabwe ndio muasisi wake, kinaitwa Alliance for Change and Transparence. nimeiona kadi yao ya uanachama in rangi ya zambarao kama jezi za mbeya city. juzi juzi tu hapa kigoma uliwaka moto baada ya wafuasi wa chama hicho kutaka kupandisha bendera yao kwenye tawi la chadema la urusi (kwa wanaoijua kigoma watakuwa wanakijua kijiwe cha chadema cha urusi) ndipo wanaharakati wa chadema walipozuia upuuzi huo mpaka polisi waliingilia kati

zitto ni ngumi jiwe. lazima wahafidhina wampigie saluti halafu wakae chini
 
Back
Top Bottom