Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

kama kweli kuna vigogo wapo behind hiki chama, basi wamefanya hivyo kwasababu za kupigana mkwara tu baada ya kuona maslahi yao yanatishiwa au ni njia ya kijitengenezea ajira zao.
Wakikutana kwenye vikao vya faragha na kuahidiwa unaibu kwenye next baraza, CCM hatoki mtu. Kama wanania ya kweli na siwaoga kwani wasijitokeze? hiki ni kipimo ya maamuzi magumu...otherwise kama alivyo sema mjumbe mmoja kuwa wana test zari.

Hakuna matumaini yoyote kwa upande wa walalahoi ama wananchi wa kawaida, kwani CCM si mara ya kwanza kumeguka. Zeji, CCM ilimeguka na kuunda CUF.( it is just a political game)

ukomo wa uwezo na akili za wanasiasa wetu (include mawaziri na wabunge) huishia kwenye kutunga sera. Sera za vyama vyetu ni TAMU ajabu, ukisoma ama kuzisikia zina CCmua, nzuri kuliko hata za wajapan na wamarekani ( si unajua jinsi wa africa tunavyojua kutunga nyimbo/kuimba?).

Sasa twende kwenye utekelezaji utakoma. Hapo ndipo unaona kuwa wanasiasa wetu ni mkusanyiko wa vilaza, mataperi, waongo n.k. Wanajifikiria wao kwanza na familia zao, wananchi wanakumbukwa wakati wa kura tu.

Inchi imepata uhuru miaka karibu 50 sasa, lakini hakuna hata sehemu ya miundombinu iliyo kamilika....miradi mingi tunayo iona imejengwa na wafadhiri, harafu tunapigwa changa la macho kuwa umetokana na utekelezaji wa sera zao.

Inaelekea hawa vigogo wanaposikia tunawalalamikia lakini bado tunapanga foleni kuwapigia kura, wakikutana kwenye vikao vyao vya Lager huwa watuponda na kunyanyua lile dole la kati la mkono juu kabisa....kidumu.
 
Ha ha ha ha, yale yale ya mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya, not so!!!!
 
Kongamano kupinga ufisadi lahusishwa na chama kipya
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd January 2010

Waandaaji wa kongamano hilo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya Serikali ya Aford, Julius Miselya ‘Seneta', alisema jana kuwa kongamano hilo la siku mbili litafanyika kuanzia Februari 13 mwaka huu katika ukumbi wa Karimjee.

Tangazo la kufanyika kwa kongamano hilo, limekuja zikiwa ni siku chache tu baada ya maombi ya kusajiliwa chama kipya cha siasa cha CCJ kuwasilishwa ofisini kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Miselya alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo ambalo litahudhuriwa na wasomi, wanafunzi, wanasiasa na watu wa rika zote.

"Sisi kongamano hili tumeliandaa ili kuipa fursa serikali iseme namna inavyowashughulikia mafisadi, tunaamini wananchi wataelewa kwa kina mambo yanayofanywa na serikali yao," alisema Miselya.

Wakati Miselya anasema hivyo, habari zimedai kuwa nia ya kongamano hilo ni kufikisha kilichoitwa ujumbe kwa wananchi wa namna Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyochukia na kupambana kikamilifu na ufisadi.

"Hatimaye ni wananchi hao kuwa waangalifu na makini katika uchaguzi mkuu ujao wasiwachague viongozi mafisadi," kilisema chanzo chetu cha habari kilicho karibu na kamati ya maandalizi ya kongamano hilo.

Miselya alisema watoa mada kwenye kongamano hilo watakuwa ni wanataaluma kutoka vyuo vikuu nchini ambao alidai wana weledi wa hali ya juu katika kueleza mambo yanayohusu utawala bora.

"Hatutaki wawe wanasiasa, wanaweza kuligeuza kongamano hilo kama jukwaa la wanasiasa," alisema Miselya ingawa kuna taarifa kuwa miongoni mwa watoa mada ni mtu mwenye wadhifa bungeni na mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam.

"Hawa wamekuwa mstari wa mbele na watu makini waliojitolea kikamilifu kupambana na ufisadi … wengine watakuwa wachangiaji tu, " kilisema chanzo chetu cha habari. Miselya, ambaye ni mmoja wa waasisi wa NDC hakutaka kabisa kuwataja watoa mada hao akisema "bado tunawasiliana nao … siwezi kuwataja".

Alipoulizwa kwa nini wamemwalika Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi, Miselya alisema awali walizungumza na Mzee Rashidi Kawawa kabla hajafikwa na mauti.

"Sasa tumemwomba Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi, lakini awali pia tulimtaka Rais Jakaya Kikwete, lakini tumeshauriwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi, itakuwa ni vigumu.

"Huyu kwa sasa tunaona anafaa awe mgeni rasmi hasa kwa hatua yake ya kutangaza mali na kuwatimua maofisa wa halmashauri ya Bagamoyo, anaonesha anachukizwa na vitendo vya ufisadi," alisema.

Alipotakiwa kusema kama kongamano hilo lina uhusiano wowote na kuanzishwa CCJ, alisema halina kabisa.
Habari zilisema kongamano hili halitakuwa na tofauti na lililofanyika hivi karibuni Karimjee chini ya ufadhili wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, kwani washiriki wengi watakuwa ni wale wale.

Ilielezwa pia kuwa washiriki hao miongoni mwao ndio wako nyuma ya uanzishwaji wa CCJ, chama ambacho kiliwasilisha maombi yake ya usajili kupitia kwa Mwenyekiti wa muda, Richard Kiyabo na Katibu wa muda, Renatus Mubhi.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, Mubhi aliwahi kuwa mwanajeshi mwenye cheo cha ukoplo, ambaye inadaiwa anahamasisha wanajeshi wastaafu kudai mafao yao kama ushawishi wa kuwataka wajiunge CCJ.

Inadaiwa Mubhi, ana undugu na Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe, ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa wabunge wanaotarajiwa kujiunga na chama hicho na kwamba ndiye mratibu mkuu wa shughuli za chama.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano huo, Mubhi alisema hana uhusiano na Mbunge huyo na wala hamfahamu na kuhusu madai kuwa anahamasisha wanajeshi wastaafu kudai haki zao ili wajiunge CCJ, alisema hizo ni chuki za wasiompenda wanaotaka kumchafulia jina.

"Hao wanataka kunichafulia jina, hata hivyo chama chetu hakina lengo baya, na CCM ina hofu dhidi yetu … sasa hivi hatutasema mengi tusubiri usajili wa muda kwanza ndipo tutazungumza," alisema.

Kuhusu madai kuwa alitoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) makao makuu akiwa Koplo baada ya kuhamishiwa Arusha, alisema si kweli na aliacha kazi kwa hiari yake na kujiunga na siasa.

Naye Mpendazoe alipoulizwa kuhusu uratibu huo na uhusiano na Mubhi, alisema yeye bado ni mwana CCM na ni mwakilishi wa watu na wanaomhusisha na CCJ wanaweza kuwa na nia yao.

"Siwezi kuzungumzia mambo ya CCJ kwa sababu mimi ni CCM na huyo Mubhi si ndugu yangu na nasikia anatoka mkoa wa Mara … hata angekuwa ndugu yangu kuna tatizo? Mbona Slaa (Wilbrod) yuko Chadema na mkewe CCM na wanaishi pamoja? Kila mtu ni mtu mzima," alisema.

Maandalizi ya kongamano hilo ambalo awali lilikuwa lifanyike Diamond Jubilee, yanaendelea na waalikwa watatakiwa kununua fulana na kofia maalumu zenye picha ya Mwalimu Nyerere na maandishi ya kuhamasisha mapambano dhidi ya ufisadi.

"Fulana na kofia hizo zitauzwa kati ya Sh 20,000 na Sh 7,000 kila moja ili kuchangia gharama za kongamano hilo ambazo ni karibu Sh milioni 10 kwa ajili ya vinywaji, chakula na ukumbi," kilisema chanzo chetu.

Kilisema hadi sasa fulana 5,000 zimetengenezwa kwa gharama ya Sh 12,000 kwa kila moja katika kampuni moja Dar es Salaam na zinaandaliwa zingine milioni moja.

Habari zaidi zilisema waandaaji wanawasiliana na kituo kimoja cha televisheni ambacho kitarusha kongamano hilo moja kwa moja kwa kati ya saa mbili na tatu kwa malipo ya Sh milioni nane.

Alipoulizwa kama wana kibali cha kufanya kongamano hilo, Miselya alisema kwa kuwa ni mkutano wa ndani, hawahitaji kuomba kibali na kuhusu usajili wa Aford, alisema ilisajiliwa mwaka 1997 na iliyokuwa Ofisi ya Kabidhi Wasii wa Serikali, ambayo sasa ni RITA (Ofisi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini).

CCJ ni chama ambacho kinadaiwa kuanzishwa na baadhi ya wanaCCM ambao wanapambana na ufisadi, pamoja na baadhi ya walioshindwa katika kinyang'anyiro cha urais mwaka 2005 kwa tiketi ya CCM na inadaiwa kaulimbiu yao inatokana na jina la chama – ‘Sisi Je (CCJ)?'
 
ndoto yangu sasa inakaribia kutimia kwani hapo awali niliisha andika thread kuwa ''NAOTA CHAMA KIPYA'' wengi walichangia na kuniunga mkono japo wapo pia waliobeza maana niliiamini hakuna chama chochote kati ya vilivyopo kinachoweza kuiteka jamii kiukweli inatakiwa upinzani halisi utoke ndani ya ccm kwani watakao toka humo wanajua madudu yote yanayofanywa na vigogo na staili inayotumika kulindana..................japo bado haijathibitika km kweli vigogo kutoka ccm ndio qwaratibyu wa mchakato mzima wa uanzishwa wa ccj lakini naamini katika lisemwalo lipo..................''TUMECHOKA KUSUBIRI,MABADILIKO NDIYO YATAKAYO TUBADILISHA''.
 
Kwa mawazo yangu, chama hiki cha CCJ ni pimajoto. Mwitikio na msisimko uliopo mtaani kwa kujua kwamba CCM inakaribia kugawanyika unatoa picha ya wazi kabisa kwamba kweli wananchi wamechoka na hali halisi iliyopo ndani ya CCM kama sio ndani ya nchi kwa ujumla.

CCJ kinaweza kuwa si lolote si chochote lakini kutangazwa kwa ujio wake kumedhihirisha kwamba wananchi wana kiu ya kutaka yawepo mabadiliko na kwamba CCM kimeishajipotezea sifa nzuri na umaarufu wake.
 
Kama Katiba yao ndivyo ilivyo, I can say with absolute confidence; CCJ is nothing but a disappointment in the making.

Mimi naona hivi:

Uchaguzi wa 2010

CCM: 70%
CCJ: 10%
CUF&CHADEMA 8%
NCCR&UDP&MAKINI&Others: 2%

Baada ya Uchaguzi Viongozi wa CCJ watagundua CCM ni chama makini kinachowatumikia wananchi, kwa hiyo watarejea CCM, watapewa nafasi za Kuteuliwa, mission inakuwa Successfull

Tusije tukawa tunalifurahia Zimwi lililotumwa kufunika Kombe Mwanaharamu 2010 Apite!

Na kwasababu watagawana Kura na Vyama vingine kama CUF, CHADEMA basi bunge litakuwa la CCM na kidogo CCJ
 
Kwenu wataalam wa sheria ndani ya JF,naomba kujuzwa katika hili.

Kuna thread iliwekwa hapa mwana JF anataka kuanzisha chama cha siasa kwa jina la TANU(Tanzania African National Unit) akajibiwa kuwa hakitoruhusiwa kusajiliwa kwani kina landana na TANU ya Nyerere mzazi wa CCM.
Sasa Hiki cha CCJ nacho na ambacho kinahusishwa na vigogo wengi toka CCM hakiwezi leta mlingano huo?
 

nadhani hawa kundi la wana ccm wanaotaka kumeguka ....wanataka kucheza karata vema.....wanaogopa kuingia vyama vilivyo tayari kwa kuogopa yaliyomkuta mrema na vyama vya kukaribishwa....wenye vyama wakipewa fungu basi wanakuambia ondoka na umaarufu wako ..tuachie chama!!

lakini vile vile kuna risk za kuanza chama especially mwaka wa uchaguzi ..watakosa muda wa kutosha wa kujiandaa.....tatizo hilo!!..matokeo ni wazi ni kushindwa.....

kwa ccm litakuwa pigo na zaidi kwa kikwete ....kwani CHAMA KITAKUWA KIMEVUNJIKIA MIKONONI MWAKE....HISTORIA ITAMKUMBUKA KWA HILO......NADHANI WANA CCM HAWATAWEZA KUMSAMEHE KWA HILO....NA ATAKUWA NA WAKATI MGUMU!!!....NA MSISHANGAE KAMA ATAKUBALI HILI LITOKEE MIKONONI MWAKE ..HATA AKISHINDA UCHAGUZI ..WENZAKE WANAWEZA KUMUONDOA KWA JUMBE AU MBEKI STYLE!!!...

JK KAZI UNAYO NDUGU YANGU!!!!!!!!!!!!!
 

ni kweli

CCM si wajinga kama tunavyofikiri
 
Binafsi ningemshauri mtu yeyote anayetaka kujiunga na CCJ kufikiria kwanza.
Kama wana option, lakini vipi kama hawana?

So far vyama vya upinzani vilivyopo bara bado havina uwezo ata kupata wabunge 10 wa majimbo, hivyo kama CCJ itasaidia kuongeza idadi ya wabunge,naiunga mkono.

Katika siasa hakuna adui wa kudumu!!!
 

CCM iwatume CCJ waanzishe chama ili kugawa kura za wapinzani?kwa hofu gani waliyonayo kwa upinzani huu tulionao??

Tusijifariji, bado hatuna upinzani wa kuitia pressure CCM kwenye uchaguzi.
 

This is a very stupid analysis ambayo sijawahi kuiona.Kweli wewe unaongozwa na hisia zaidi kuliko kufanya uchambuzi wa kina.CCJ hata kama kitakuwa na nguvu vipi hakitaweza kupata Wabunge kwahizo asilimia ulizoziweka,kwani sio rahisi kama unavyodhani....kutangaza chama cha siasa sio kazi rahisi....inahitaji angalau miaka 3 ili kujitambulisha vya kutosha kwa watanzania...kumbuka hapa ni Tanzania na sio nchi Marekani wala Uingereza...Hata hao wabunge watakaokianzisha wengi wao watapoteza ubunge wao wakigombea kupitia CCJ....
 

Kama nimesema uongo nihukumu kwa Uongo wangu lakini kama nimesema kweli yanini kunitukana, kama wautendea mti mkavu hivi je iyakuwaje kwa mti mbichi?

Ukirudi ukasoma na KUELEWA nilichomaanisha naamini utarejea na Kuondoa hilo tusi lako
 
Kama nimesema uongo nihukumu kwa Uongo wangu lakini kama nimesema kweli yanini kunitukana, kama wautendea mti mkavu hivi je iyakuwaje kwa mti mbichi?

Ukirudi ukasoma na KUELEWA nilichomaanisha naamini utarejea na Kuondoa hilo tusi lako

Ndege ya Uchumi
Sijakutusi ila ni mtazamo wangu kwamba uchambuzi ulioufanya sio sahihi.Nimekusoma kwa makini na nimekuelwa vizuri sana.Rejea tena uchambuzi wako halafu tafakari kwa kina utagundua kwamba umekosea.Umekipa CCJ 10% halafu ukavipa CUF na CHADEMA 8% kitu amabcho sio sahihi.Umekaa kishabiki zaidi.
 
[SIZE=3 said:
Mzee Mwanakijiji;757892]Binafsi ningemshauri mtu yeyote anayetaka kujiunga na CCJ kufikiria kwanza[/SIZE].

1. Mpambanaji yeyote hana haja ya kuangalia mambo mengi saanaa mbele yake cha kuangalia tu ni asiangukie mikononi mwa adui Zake kirahisi akisha jiridhidhisha angalau kidogo akapima yaliyoko nyuma yake(adui alionao kwa sasa alipo) huamua kusonga mbele.

2. HILA PIA INAWEZEKANA CCJ UKAWA ndoano iliyowekwa na MAFISADI kuwaondoa watu CCM hili Mafiisadi waweze kupumua
 


nothing new....watafulia tu kama wenzao wa South Africa
 

matumaini yanayofifia......kweli WaTz tumechoka jamani!!
 


Nafikiri ungekuwa unafikiri kabla ya kuandika jambo, hivi kweli CCM ni makini kwa kuwatumikia wananchi kwa yepi au makini kwa kushinda uchaguzi, tofautisha kushinda uchaguzi na utekelezaji wa ilani yake.

Umeandika kwa ushabiki zaidi ya mantiki yenyewe labda ungesema CCM huwa makini linapokuja suala la chaguzi inaweza ikapata hizo 70% lakini si kwa kuwatumikia wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…