Akiongea katika tuongee asubuhi kupitia Star Tv,yule msomi wetu wa Redet Dr Bana amesema yeye mpaka sasa ajaona chama mbadala cha kuongoza nchi zaidi ya CCM,nadhani hizi ni dalili mbaya kwa wasomi wetu.Badala ya kuwasaidia watanzania kujua haki zao za msingi yeye anasema hakuna wa kuiongoza hii nchi..
Siwezi kumshangaa huyo DR,watanzania wengi wana inferiority complex, they fear their nature,huyu DR naye yumo katika hilo kundi mazungumzo yake huwa nayasikiliza sana,ukimuangalia sana huwa comments zake anaangalia mambo yamekaaje kwa wakati huo(anafuata upepo).sote tunajua watu wa aina hii ndio washauri wa serikali yetu katika mambo mengi ya maendeleo Dr Bana kwa upande wangu huwa simtofautishi na mwanasheria mkuu wa serikali ,kwa ajili ya kuhangaikia mkate wa siku hiyo iliyopambazuka na kesho atajua kesho kukicha watachangaje karata wapate mkate mzuri wenye siagi ya brueband toka Kenya badala ya Tanbond ya Tanzania.
Ni aina ya watu wanajitahidi kuakikisha wanaitetea CCM na Serikali yake hata kwa makosa ilimuradi wafanikiwe kuchumia tumbo.
Sasa hivi dunia imebadilika sana kwenye secta ya siasa na uongozi,nchi yetu bado haijabadilika kwasababu kuna udicteta na ufalme wa chini chini ,tena ufalme huu ni mbaya sana kwa sababu ni ufalme wa viongozi kutaka famili zao kuwa viongozi pia hata kama hawawezi muda wao wa kupumzika ukifika.
Nchi hii wapo wenye uwezo wa kuwa viongozi wazuri kinachowashinda ni masharti ya kuingia katika hako kakundi ka sasa maana wanajitahidi kadiri iwezekanavyo kulinda na kuhalalisha maovu wao hiyo sio sera yao katika maisha wanayoamini wao.
Tanzania ya leo haikupaswa kuwa hivi, ni matatizo ya uongozi ndio yametufikisha hapa,hili DR Bana asibishe na wasababishaji ndio hao hao anao wapigia debe leo kwa nguvu zake zote,hivyo DR Bana ajue kuwa kwakuendelea kuwa na mtiririko wa hao viongozi tutazidi kutiririka kwenye maangamizi ya uchumi wetu na maisha ya watanzania kwa ujumla wake.
Kinachotakiwa sasa kwa hali yoyote ile mabadiliko ya uongozi(mfumo mzima)ni lazima ili turudi kwenye msitari.
Tuliweka matumaini sana kwa JK lakini mwishoe hakuna tulichopata zaidi ya kuendelea kuanguka kutokana na matokeo ya sasa wale wote wanaojitayarisha kumrithi siwaamini hata kidogo lazima watanzania tu wa suspect kama ni failure tayari kabla hata hawajaingia madarakani.
CCM ikitoka madarakani ndio utakuwa mwanzo wa kuwepo mfumo mpya wa uongozi amini usiamini uongozi mzima wa CCM utabadilika na ndio uwazi utakuwapo na ulinzi wa mali yetu utakuwapo pia mfumo wa siasa utabadilika kwa 100%. Kwa watanzania wenzangu ambao tunaweza kupamabanua mambo kwa ukweli na si kwa unafiki tuendelee kufanya hivyo kwa jia yoyote ile iwe kwa mahojiano na vyombo vya habari au kwa mitandao kama JF. JF ni chuo cha maendeleo ya kweli.