Chama cha kutetea haki za wahasibu

Aug 10, 2011
35
13
Hivi jamani hapa Tanzania kuna chama cha kutetea masilahi ya wahasibu ? Kama kipo mbona hatukisikii ?
Kwa tafiti nilizozifanya inaonesha watu wanaofanya kazi za uhasibu kwa hapa Tanzania wanalipwa pesa kidogo sana ukilinganisha na unyeti wa kazi wanayoifanya.

Jamani chama cha kutetea haki za wahasibu hapa Tanzania kipo au hakipo ?
 
Wahasibu wanalipwa kidogo ukilinganishwa na watu wa taaluma ipi. Katika nyanja zipi, Serikalini au sekta binafsi. Wenye CPA au kwa ujumla. Nitarudi baadaye
 
Tanzania Association of Accountants ni cha kazi gani? Na hiyo NBAA kazi yake ni nini? Hivyo si ndio vyama vya wahasibu hapa Tanzania au mimi sielewi?

Mkuu tatizo wahasibu wengi wevi ndio maana wanaridhika na mishahara unayosema midogo. Wanajua jinsi ya kuziba mashimo!
 
Fanya tafiti kwanza kabra ya kuropoka ndg. labda mhasibu wa ofisi yako ndo mnalipa pesa ndogo. Na pia tofautisha kati ya Makarani wa Uhasibu na Whasibu waliothibitishwa na bodi ya Uhasibu.

Fanya utafiti kwanza Humu pia kuna wahasibu.
 
Mtu anashikilia kasiki la kampuni, wizara, halmashauri, taasisi n.k. kwanini aanzishe chama!
 
Tanzania Association of Accountants ni cha kazi gani? Na hiyo NBAA kazi yake ni nini? Hivyo si ndio vyama vya wahasibu hapa Tanzania au mimi sielewi?

Mkuu tatizo wahasibu wengi wevi ndio maana wanaridhika na mishahara unayosema midogo. Wanajua jinsi ya kuziba mashimo!

Yaani hicho chama ni kama hakipo kabisa kwa maana sijakisikia kabisa !
kuna Dada mmoja ana degree ya Uhasibu yupo kwenye benki moja binafsi kama mhasibu , eti take home ni laki nne tu ! Hivi hiki kiasi cha pesa kinalingana kweli na majukumu yake ? Halafu muda wa kuingia kazini ni kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni !

Hapa unasemaje kuhusu huu mshahara ? Hawa si ndio wanaosababisha wahasibu waonekane wezi kwa kuwapa mshahara mdogo ?
 
kwa mshahara wa kihasibu lazma ufanye creative accounting ,hapo ni windowdressing kwa kwenda mbele,yan mtu unakusanya milioni mianane kwa siku alaf unalipwa shlak4,5 mpaka7, makusanyo kwa mwaka inafika bilion40+ alaf par annun unakula mil8 huu ni utapeli. pia mabenk yote yamekaa kinyonyaji tu,ukiijua mishahara ya benki na muda wa kazi kwa siku utadata!
 
Fanya tafiti kwanza kabra ya kuropoka ndg. labda mhasibu wa ofisi yako ndo mnalipa pesa ndogo. Na pia tofautisha kati ya Makarani wa Uhasibu na Whasibu waliothibitishwa na bodi ya Uhasibu.

Fanya utafiti kwanza Humu pia kuna wahasibu.

we unalipwa sh ngapi?
 
Sasa wewe ndo mhasibu halisi si utakuwa na majibu?

Haha ha ..! Yaani mimi naipenda sana hii fani kwa kuwa ipo kwenye damu haswaa lakini kwa hapa Tanzania naona kama hailipi kabisa, kinachotumika hapa TZ ni ubabe ubabe tu. Siasa imeshika hatamu. Kila sehemu inatumika siasa. Ndo maana wizi hauishi hapa TZ.

Ikiwa madaktari wanalipwa mpaka laki tisa(9) kwa mwezi lakini wanagoma, iweje mhasibu anaelipwa laki nne(4) kwa mwezi , yaani yupo kazini tu , anaendelea na kazi ? Halafu mbaya zaidi, pesa zinazoingia na kutoka zote anaziona ! Mimi hii Tanzania Association of Accountants hata siioni kazi yake. Labda inafanya kazi kwenye makaratasi tu , kama ilivyo RUBADA.

Hivi wahasibu wenzangu mnasemaje ? Kwanini tusipindue tu huu uongozi wa Tanzania Association of Accountants uliopo madarakani kwa sasa , kwa maana hakuna unachofanya kutetea masilahi ya wahasibu ! Imefikia mahala mtu ukishamwambia tu kwamba taaluma yangu ni mhasibu, picha ya kwanza inayojengeka kichwani mwake ni kuwa wewe mhasibu lazima utakuwa unaiba fedha !
 
Back
Top Bottom