ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,690
- Thread starter
-
- #201
Mkuu bado hujanifungua macho, what is the way forward? Umeelezea matatizo ya CHADEMA, fine, mbona hutaki kutuambia tufanyeje baada ya hapo. Tupe fikra mbadala basi!!
Mkuu mbona unataka kulinyima jukwaa fursa ya kujadili mambo? Yaani ulitaka ZeMarcopolo aende kuwatafuta wanachama wa CHADEMA mitaani na kuwaambia hayo? Nadhani hapa kuna wana CHADEMA ambao wanaweza kutusaidia kujibu huu "upuuzi" wa mtoa hoja.
Jelyfish hapo ndiyo uwezo wako wa uchambuzi wa thread ulipoishia kweli ? Mimi siamini bhana ! Una uwezo zaidi ya huo , hebu rudi tena kwenye huu uzi bhana , Zemarcopollo anasema kwamba Kisandu (aliyehamia NCCR mAGeuzi ) kaondoka Cdm kwa ajili ya Tamaa ya Madaraka, bali Mwampamba (aliyehamia CCM ) kaondoka cdm baada ya kuona Madudu , kweli ndivyo ilivyokuwa ? Siyo thread bora bhana ! Mwandishi amesukumwa na ama Posho au Maslahi ya kisiasa .
unapaswa kujiongeza sio kila jambo utafuniwe. Inshort, amejaribu kuonesha mapungufu hayapatikani ccm tu hata vyama vingne km cdm. Pia uone kwmba cdm ni chama chenye maslahi ya watu wachache na muelekeo wake ni wakibinafsi zaidi wanapaswa kubadilika km wanahitaji dola. Lkn mpk sshv dola kwao itabaki ndoto,hawana mkakati wa kuwafikia mwananchi wameanzisha uongozi wa kanda ambao bado ni centralizatn,ccm wamedecentralize mpk kwa balozi wht do u espect?
Ndugu umetoa maelezo mengi ambayo sio mageni sana kwetu ebu naomba nifafanulie yafuatayo
1.Kuna kundi umesema linataka kupanda haraka kisiasa na hapo hapo umesema ni chama cha Kilaghai inakuwaje mtu atake kupanda kisiasa kwenye chama cha kilaghai ambacho kwa mtazamo wako akina mvuto wala mwelekeo?
Mkuu Ze macropolo naona umeamua kumwaga vitu jamvini.
Chama chenye ulaghai kiko huku.....Mengine yote ni political diversions za kusahaulisha wa-Tanzania kuhusu ahadi zao.
Tembelea
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-za-jk-nape-tuambie-zimetekelezwa-ngapi.html
ZeMarcopolo njoo ujibu hoja za 'ulaghai' huku.
Copy:
Kimbunga
ErythrocyteUmekosea sana kwamba kilichomtoa kisandu ni tamaa ya vyeo bali kilichomtoa Mwampamba ni kujitambua ! Very poor analysis !
ZeMarcopolo..umeiweka vizuri sana.tunaweza kua tumeichoka CCM na ufisadi na udhaufu mwingine wa kiuongozi, lakini CDM siyo mbadala wa CCM kwa kutuonyesha madudu hayo ndani ya uchanga wao kama chama cha kitaifa.
washabiki au dillusional supporters of CHADEMA, I should correctly put it that way wanaamini CDM itamaliza matatizo yote ya Tz-elimu, umaskini, afya, ufisadi, maji safi, miundombinu wengi wamezibwa akili na fikra na chuki za watawala waliopo wanashindwa kuuliza CDM na kuangalia udhaifu mkubwa huu wa CDM ikiwemo mambo ya demokrasia ya ndani na ufisadi wao, kutokua wawazi katika maamuzi yao na mengineo uliyoyaonyesha kwenye thread.
Hawa vipofu wanashindwa kujiuliza Je CDM watahitaji kukuza pato la taifa kwa asilimia ngapi na ndani ya muda gani na kwa njia zipi haswa(kwa sababu ukisema tu tukusanye zaidi kodi ndani ya uchumi mwembamba kama wetu haitotosha, ukisema uongeze kodi kwa wawekjezaji haitotosha, ukisema kuokoa tu hela kutokana namatumizi ya v8 na ukubwa wa serikali na yenyewe haitotosha kupata fungu la kufanya yote wanayoamini hawa blind followers wa CDM na hapo unaitaji kukuza uchumi na hii inachukua muda na mikakati mahsusi ambayo sijawahi isikia kwa CDM).
Je hawa CDM wenyewe ni wanasiasa wanaotumia siasa au wanaharakati wanaotumia siasa na baada yha hapo hawataitaji siasa na (mabaya yote yanayoambatana na siasa ikiwemo rushwa) kung'ang;ania madaraka na kujiongezea nguvu huku wakijenga gap kati yao na wananchi? kwanza sijasikia wakisema watawachukulia hatua gani mafisadi wakubwa walioharibu hili taifa na kuna dalili zote wana dine and wine na mafisadi hawa nyuma ya pazia. huu ni uvugu vugu na siyo mapinduzi kama ambavyo sisi wengi tunavyotaka. na historia ya vyama vya upinzani Afrika ni hii hii ya kufeli kuleta mabadiliko, wapinzani wakiingia wanakua mabwana wakubwa wapya na kazi imeisha.
CDM wangekubali kama wenyewe ni wansiasa tu wanaotaka kujaribu uongozi na kuongoza nchi kutokana na dira yao, ambayo haiko tofauti na ya CCM anyway. lakini huku kujifanya na kuwaaminisha wafuasi wao kua wenyewe ni political saints bent on delevering salvation to the long suffering tanzanias ni uongo nisioweza kuuamini mtu kama mimi mwenye akili kidogo za kufikiria.
JJBndio maana watu wengi wa pwani hawajaendelea
halafu mnajiona wajanjaa! kumbe walalahoi tu. lakini acha mbaki jinsi mlivyo ili kwenye jamii makundi ya kiuchumi yazidi kuwepo ili mkome vizuri
Aaah Mkuu Molemo huwezi kujibu hoja hizo kwa jinsi hii. Nadhani una cha kuchangia hapa kuliko hiki ulichokiandika!
Ni kweli kabisa mkuu,Kaka,
Ni katika kutekeleza majukumu yetu kwa jamii. Tanzania itajengwa na mtanzania.
Tuendelee kuwa Pamoja...