mimi nashangaa aina ya watu kama wewe, na mada dhaifu mnazozipost humu.
vyama vya upinzani na wanaharakati wanakisakama chama cha mapinduzi na serikali yake kwa kuwa ndo chama tawala, chenye dola na kinashindwa kuongoza nchi ili wakiangushe wakae wao madarakani, na wakosoaji wanajipambanua dhahiri kwa misimamo na malengo yao
ni vema basi unapoandika tuweke wazi wewe ni nani, je ni mtanzania mzalendo, ni mwanaCCM,masalia PM7, mwanaCHADEMA, au mwanaharakati???, na je katika maandiko yako, unakejeli??,unaponda?? unakebehi??,unashutumu??, unatoa ushauri, angalizo, ili tuweweze kujadili
kwa mfano rahisi ukisema mimi ni Mwanchama wa Chadema, ninakerwa na mfumu huu wa uongozi wa chama. wasomaji tutajadili kwa mtazamo huo
au ukisema mimi ni mwana CCM, napingana na itakadi na sera za CHADEMA, tutakupa jibu stahiki
sasa unataka tujadili nini??? tuseme ndiyo au hapana??? au unatoa taarifa tu??? kama ni taarifa ili iweje?? na nini kifanyike.
vinginevyo unatupotezea muda kuna issues za msingi za kujadili,
- nchi haina umeme wa uhakika,
- huku ubungo hatuna maji,
- wadogo zetu 95% wamefeli,
- kuna chuo cha ugaidi ukerewe
- kuna vikundi vya uharamia vinavyofadhiliwa na ikulu kudhuru wapinzani