Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,789
- 1,732
Unaposema kuna ambao wamedanganyika na kuhadaika na propaganda, bila shaka unalenga kutuambia kuwa kuna walaghai fulani walifanikiwa kufanya kazi ya kulaghai, na wadanganyifu fulani waliofanikiwa kudanganya.1. Wale ambao ni bendera fuata upepo. Katika kundi hili kuna watu wa aina tatu:
i) Wale ambao wamedanganyika na propaganda kuwa chadema ni chama cha kikabila au cha kikanda na kwa vile wao wanatoka kwenye kanda hizo basi wanajisikia ukaribu zaidi na chadema. Hapa utaona kuwa propaganda za kukichafua chama kuwa ni cha kikabila au cha kikanda kimeweza kuwaongezea chadema nguvu katika maeneo inayoshutumiwa kuyapendelea.
ii)Wale ambao wamelaghaika na propaganda za kuwa chadema ni chama cha udini. Kuna waumini wengi wameviunga mkono vyama vya chadema na CUF kwa sababu tu wamekuwa wakisikia kuwa vyama hivyo vinashabiiana na dini zao. Hawa ni bendera fuata upepo ambao hawachuji ukweli wa taarifa na hawajiulizi chama kinaweza kuwanufaishi vipi kama waumini wa dini husika.
Hao walaghai na wadanganyifu ni akina nani?
Kama wameweza kulaghai Watanzania kuwa Chadema ni chama cha kidini, na kudanganya watanzania kuwa Chadema ni chama cha kikabila, na wewe kila siku unaonekana kuwaunga mkono hao wadanganyifu na walaghai, ni nini kitatufanya tukuamini hata haya unayoandika kama si UDANGANYIFU na ULAGHAI?
Umevutwa nini kuwa upande wa wadanganyifu na walaghai?