Chama cha Kilaghai Tanzania...

Chama cha Kilaghai Tanzania...

what about Mwigulu, anafaa hata kuwa balozi wa nyumba 10?
Nape hata uongozi wa familia ni zero,
Yule mzee wenu aliyeharibika nusu ya ubongo wake (wassira) yule hata ukimpatia umonitor wa darasa atashindwa kuliongoza. hao ni wachache tu kumention, wapo wengi sana humko ccm ambao hawana sifa hata moja ya uongozi lakini ndo wamewekwa kwenye nafasi nzito za maamuzi. NYANI HAONI KUNDULE

1. Huna sababu ya kumtukana Wassira kuwasilisha hoja yako.
2. Sijui kama tatizo lako ni uwezo wa kielimu au uwezo wa kuelewa lugha ya kigeni. Kwa sababu nimeelezea nepotism na nikataja cronyism. Ingawa hii cronyism sikuielezea kwa undani. Kama ungekuwa unaelewa maana yake, basi majibu ya maswali uliyoniuliza ungeshayapata katika maelezo niliyoyaandika hapo awali.

Tafuta dictionary nzuri inayoweza kukueleza maana ya Cronyism kisha utapata majibu ya maswali yako.
 
Swala hapa nafikiri siyo kwamba CCM ni bora au siyo bora, bali pamoja na matatizo yote yanayoendana na uongozi wa CCM, Je kuna Chama mbadala, nikiamaanisha kwamba ni Chama gani ambacho utakiangalia na kusema hawa watakuwa bora au watakuwa tofauti? Hilo ndilo swali la msingi!

Ngoja nikupe mfano mdogo sana, baadhi yetu tunaamini kwamba CHADEMA ndio mkombozi na wako tofauti na CCM, lkn ukiingalia sana CHADEMA hawana tofauti kubwa na CCM kwa mfano, Wabunge wengi wa CHADEMA wanaishi Dar kama vile Bw. Mbowe anaishi Mikocheni, Bw. Lisu anaishi Tegeta, Bw Zito Kabwe Dar, Bw. Sugu n.k sasa hawa pia kama Wabunge wa CCM wanafuja mali ya Umma kwa maana Wabunge wote wana Ofisi Majimboni kwao, na wanalipwa fedha na Serikali kuziendesha hizo Ofisi, hivyo ili kutumia pesa za Watz vizuri walipaswa kila siku wawe ofisini kwao ilikusikiliza Wananchi wao waliowachagua, sasa wewe niambie tofauti hapo iko wapi kati ya Wapinzania na CCM?

Ukiangalia siku ambazo Bw. Mbowe yuko Hai ofisini kwake kwa mwaka hata miwezi 2 haifiki, sasa wanatumia kigezo gani kusema CCM wanafuja fedha zetu?
Kama unaniambia fulani ni mbaya basi wewe lazima uonyeshe mfano kwa kuwa tofauti, lkn ukifanya yale yale, basi ni bora nibaki na yule mbaya lkn namjua kwa muda mrefu, hiyo ndio hoja hapa!

Weka CV yako kwanza.
 
Njaa mbaya sana,povu lote hili mtu anapata hela ya kula mchana tu.
 
Swala hapa nafikiri siyo kwamba CCM ni bora au siyo bora, bali pamoja na matatizo yote yanayoendana na uongozi wa CCM, Je kuna Chama mbadala, nikiamaanisha kwamba ni Chama gani ambacho utakiangalia na kusema hawa watakuwa bora au watakuwa tofauti? Hilo ndilo swali la msingi!

Ngoja nikupe mfano mdogo sana, baadhi yetu tunaamini kwamba CHADEMA ndio mkombozi na wako tofauti na CCM, lkn ukiingalia sana CHADEMA hawana tofauti kubwa na CCM kwa mfano, Wabunge wengi wa CHADEMA wanaishi Dar kama vile Bw. Mbowe anaishi Mikocheni, Bw. Lisu anaishi Tegeta, Bw Zito Kabwe Dar, Bw. Sugu n.k sasa hawa pia kama Wabunge wa CCM wanafuja mali ya Umma kwa maana Wabunge wote wana Ofisi Majimboni kwao, na wanalipwa fedha na Serikali kuziendesha hizo Ofisi, hivyo ili kutumia pesa za Watz vizuri walipaswa kila siku wawe ofisini kwao ilikusikiliza Wananchi wao waliowachagua, sasa wewe niambie tofauti hapo iko wapi kati ya Wapinzania na CCM?

Ukiangalia siku ambazo Bw. Mbowe yuko Hai ofisini kwake kwa mwaka hata miwezi 2 haifiki, sasa wanatumia kigezo gani kusema CCM wanafuja fedha zetu?
Kama unaniambia fulani ni mbaya basi wewe lazima uonyeshe mfano kwa kuwa tofauti, lkn ukifanya yale yale, basi ni bora nibaki na yule mbaya lkn namjua kwa muda mrefu, hiyo ndio hoja hapa!
Mkuu Kijakazi nimekupata, hapa nilipo kuna ulaghai wa TANESCO.

Kuhusu wabunge kukaa Dar hili linatokana na mfumo wa kiutendaji, kila mbunge anayefuatilia huduma za jimboni kwake lazima mda mwingi awe Dar.
Suluhisho la hilo ni kutegemeza wananchi katika maeneo yao (MAJIMBO) na CDM hilo wameishaliona wanalitangaza.
 
Last edited by a moderator:
Tunataka tujue kama wewe ndiyo walewale ambao "wanaopata" -A- masomo tisa form four lakini hawawezi kupata C masomo matatu form six.

"Tunataka tujue" wewe nani mwingine? Isitoshe hata kama sijaenda Shule kabisa, lkn sishindwi kujua kwamba Mbunge anatakiwa awe ofisini kwake kila siku, kwa maana amechaguliwa na wananchi ambao wanamuhitaji jimboni, na si vinginevyo!
 
Mtundiko (thread hii) huu utafungwa haraka sana na aliyeutundika hapa atapigwa "ban" asionekane tena jamii forums. Mimi binafsi nimeshipigwa ban mara kadhaa humu, tena ban la kudumu, lakini bado nimo tuu humu. Kuna wimbo mmoja wa Bob Marley unaitwa "Bad Card". Katika bad card kuna mstari Bob Marley anasema "You a-go tired fe see me face, Can't get me out of the race, Oh, man you said I'm in your place, And then you draw bad cyard, A-make you draw bad cyard, And then you draw bad cyard"

Hiyo ndiyo Jamii Forums, usipokubaliana na uchadema, wanaona "you are in their place".

Kama alivyosema mtoa mada, ndani ya CHADEMA, "nepotism" ndiyo uendeshaji wa chama. Hata CCM nao pia ndiyo hivyo hivyo, ingawa wao kidogo wanachanganya nepotism na "cronyism".

Neno nepotism linatokana na neno la ki-Italiano "nipote". Neno nipote kwa kiingereza linakuwa "nephew". Sasa neno nepotism limeanza kutumika kutokana na tabia ya "papa" wa kanisa katoliki kuwapendelea watoto wao wa kuwazaa wenyewe na kuja kuwa ma-kardinali; na baadaye ma-kardinali hao huwa papa. Lakini kutokana na kwamba "papa" au "pope" hatakiwi kuwa na mtoto, basi watoto wa papa, (popes) walikuwa wakiitwa "nephews" au "nipote" badala ya "sons". Kwa mfano; Pope Callixtus III alimchagua "nephew" Rodrigo kuwa Kardinali. Baadaye Kardinali Rodrigo akaja kuwa papa Alexander VI. Mfumo huu ulishamiri sana ndani ya kanisa katoliki kwa miaka mia kadhaa mpaka alipokuja papa Innocent XII, akakataza tabia ya watu kuwachagua "nephews" kuwa kardinali kuanzia mwaka 1692.

Sasa Chadema kinachofanywa na CHADEMA siyo kitu kipya. CCM nao wanafanya hivyo hivyo. Ingawa kutokana na historia na uzee wa CCM, hakuna mkoa au kanda inayoweza kusema kwamba CCM ni mali yao.
Kuhusu CHADEMA,..... well, waingereza wanasema "the proof is in the pudding"- Godbless Lema. Godbless Lema hana hata sifa ya kuwa "class-monitor" wa darasa la nne wa shule ya msingi. Lakini yupo katika kitovu cha nguvu na utawala wa CHADEMA. Kwanini? kwa sababu - "one of the nephews".

Du!! Watu muna mang'ana!!!! Ngoja nkae pembeni nisijepigwa tena ban with no reason.
 
umesahahu kuweka kundi la walala hoi nao wanaunga mkono chadema,ujakosea, kwa kuwa ccm na chama cha wenye fedha(mafisadi) tutashindana kwenye kura tuone watashinda mafisadi au hayo makundi uliyoyataja. mtaangaika sana lakini mwisho wenu ni 2015 na lazima tutawawajibisheni kwa kututia umasikini kwa miaka yote mliokuwa madarakani,hatutawaacha hivihivi, kama ni mali mtarudisha na jela mtaenda.tuna usongo sana na nyinyi,kadri mnavyozidi kutudharau ndivyo tunavyozidi kuwa na hazira dhidi yenu,na kama wanaosema hayo wanasema kwa kujipendekeza kwa mafisadi basi wanawaaribia nyie mafisadi, maana lazima mrudishe kila mlichofisadi na muingie jela.
 
Watu tuna kila haki ya kuamini kuwa una chuki kwa kunyimwa nafasi na kufukuzwa CDM zaidi ya dhamira ya kuwafanya watanzania kuchagua chama bora. Pamoja na kupiga tararira zote hizi haujatueleza watanzania, hasa sisi vijana wasomi, tusio wanasiasa lakini tunahitaji future nzuri ya watoto zetu, chama mbadala ni kipi?? Yes umeeleza mapungufu ya CHADEMA kwa mujibu wa fikra zako ambazo kimsingi hakuna jipya hapo, ni mambo ambayo tumekuwa tukiyasikia kila siku kutoka kwa watu walewale ambao either ni maccm au wanasiasa njaa waliofukuzwa CDM, je nini chama mbadala kama CDM haifai kwa mujibu wa hoja zako?? Turudi kuiunga mkono CCM?? Twende NCCR?? Twende CUF? Au tuiache nchi yetu ikiendelea KUANGAMIA KWA UFISADI NA UMASKINI?
Naomba nimkumbushe mleta uzi.Mwampamba Mtella,hakuchukizwa na mwenendo mbaya wa cdm,hapo ni kuchanganya mambo,huyu sehemu ya vijana walioombwa kwa fedha ninyi na ccm,zoezi likiratibiwa na nape,mwigulu na mzee wasira,sikatai kutokuwepo mapungufu ndani ya cdm,la hasha na kama yapo basi ni kawaida sana katika uendeshaji wa chama,kinachokuwa kwa kasi kubwa kama cdm,vipandikizi za hoja zenye hujuma za kulazima kama unavyotaka kuwaaminisha watu kwamba ni chama cha kikanda,kikabila.hizo ni propaganda zilizozoeleka kusikika japo katika uhalisia sio kweli,na mleta uzi huu ni sehemu ya watu wanakereka sana kuiona cdm inavyozidi kukua,na sio kweli kwamba eti umekuja na uzi huu ili cdm ijirekebishe,dhima yako ni kuichonganisha kwa mambo ya uongo yasiyokuwepo,na kama ni hivyo si bora uache ili chama kife chenyewe ili ccm,i takeoff kama ulivyoshauri kwamba ni bora kuendelea na ccm,kuliko vyama vingine kama cdm,
 
1. Huna sababu ya kumtukana Wassira kuwasilisha hoja yako.
2. Sijui kama tatizo lako ni uwezo wa kielimu au uwezo wa kuelewa lugha ya kigeni. Kwa sababu nimeelezea nepotism na nikataja cronyism. Ingawa hii cronyism sikuielezea kwa undani. Kama ungekuwa unaelewa maana yake, basi majibu ya maswali uliyoniuliza ungeshayapata katika maelezo niliyoyaandika hapo awali.

Tafuta dictionary nzuri inayoweza kukueleza maana ya Cronyism kisha utapata majibu ya maswali yako.

one of the JF's great thinkers, humu ndani watu aina yako wamekuwa nadra sana,au kama wapo basi hawashiriki kwenye mijadala kama huko zamani, akili na uelewa wako wa mambo ni wajuu zaidi, kwa maana hiyo inawapa watu wengi humu tabu ya kuchambua na kuelewa maoni yako, ila tufanyeje na JF imeingiliwa?

MSAFARA WA MAMBA KENGE HAWAKOSEKANI.
 
Mkuu Kijakazi nimekupata, hapa nilipo kuna ulaghai wa TANESCO.

Kuhusu wabunge kukaa Dar hili linatokana na mfumo wa kiutendaji, kila mbunge anayefuatilia huduma za jimboni kwake lazima mda mwingi awe Dar.
Suluhisho la hilo ni kutegemeza wananchi katika maeneo yao (MAJIMBO) na CDM hilo wameishaliona wanalitangaza.

Hata hiyo bado sio ishu, ishu ni kwamba kama wao wanataka kuwa tofauti na wa CCM wangetuambia kwamba hizi pesa wanazozilipwa za jimbo SIYO halali yao kwa maana wanalipwa ili wawe Ofisini karibu na Wananchi wao Jimboni, na ndio maana ya Mbunge kuwa na Ofisi na sio vinginevyo, sasa Wabunge wa CCM wamekuwa wakitudhulumu miaka yote, wengine miaka 5 hawajawahi kukanyaga Jimboni, na Wapinzani nao hivyo siku ukimuona basi labda Raisi anakuja Jimboni kwake sasa tofauti iko wapi?

Pili kulibadilisha hilo hauhitaji sijui kusubiri sera mpya ya CHADEMA ya Majimbo, ni swala la uamuzi tu, ambao unaweza kufanyika hata leo wakiamua, kwani hata ukiweka Majimbo bado Magavana watakuwa wanaishi Sinza au Kinyerezi, lkn ofisi zao ziko Majimboni.

Tatu hata kama hata kama inabidi waje Dar kushughulikia mambo fulani inaeleweka lkn sio ktk siku 365 ni siku 30 tu ndio wako Ofisini, hilo halina utetezi!

Mwisho mimi sio mwanachama wa Chama chochote bado, ninatoa maoni tu kulingana najinsi ninavyoona!
 
Anakupotezea muda?. KWELI?
Kama angekuwa kweli kweli anakupotezea muda wako wenye gharama kubwa usingepoteza muda mwingi kuandika kwa kirefu namna hii wakati kuna issues za msingi zinahitaji sana mjadala na uchangiaji wako. Vinginevyo, kwa maandishi haya, wewe unakuwa ndiyo siyo mtunza muda mzuri.

Ni angalizo tu.

Nawe pia ni gamba?
 
ila mbona una harufu ya masalia?
umeplay very low kutuambia Z'bar pana demokrasia!
hawa wazenji wamejgawa kimakund,mweus vs mwarab,muumguja vs mpemba na uktaka kuprove ilo angalia matokeo ya pemba na cuf ssm na unguja.
CDM ishaingia zenj subr ukuaj wake ..
 
Lakini pia ukiangalia kwa makini, utabaini kuwa CDM wanategeamea watu yaani wanafanya siasa za watu kwanza, sera baadaye. Hii ndo inafanya watu kama Slaa kujiona kuwa wao ni zaidi ya Chadema na anafanya atakavyo kwa sababu tu bila yeye hakuna Chama. Kimsingi huu ni udhaifu uliopitiliza.

Pia hivi sasa let's say kwamba Wachaga waache au wasiendelee kuwa na matumaini na Chadema, itakuwa na hali gani? Au wakatoriki wanaomchukulia Slaa kama tumaini lao, wakiacha kuamini hivyo, Chadema itakuwa na hali gani?
 
Mkuu vichanzi usemayo ni kweli,
Kama hajapigwa ban basi hii thread itafagiliwa chini ya kapeti haraka sana
 
Last edited by a moderator:
Usiiidanganye akili yako ukatumia macho kufikiri.[QUO

1. wale ambao ni bendera fuata upepo.
2. wale wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za
kisiasa za kitaifa.

Nitayachambua makundi haya mawili kama ifuatavyo:

1. Wale ambao ni bendera fuata upepo. Katika kundi hili kuna watu wa
aina tatu:

i) Wale ambao wamedanganyika na propaganda kuwa chadema ni chama cha
kikabila au cha kikanda na kwa vile wao wanatoka kwenye kanda hizo basi
wanajisikia ukaribu zaidi na chadema. Hapa utaona kuwa propaganda za
kukichafua chama kuwa ni cha kikabila au cha kikanda kimeweza
kuwaongezea chadema nguvu katika maeneo inayoshutumiwa kuyapendelea.

ii)Wale ambao wamelaghaika na propaganda za kuwa chadema ni chama cha
udini. Kuna waumini wengi wameviunga mkono vyama vya chadema na CUF kwa
sababu tu wamekuwa wakisikia kuwa vyama hivyo vinashabiiana na dini zao.
Hawa ni bendera fuata upepo ambao hawachuji ukweli wa taarifa na
hawajiulizi chama kinaweza kuwanufaishi vipi kama waumini wa dini
husika.

iii)Kundi la tatu katika bendera fuata upepo ni vijana ambao wanaona
kuwa chadema ni kama fashion. Ukikaa nao chini vijana hawa kuwauliza
kwanini wanaiunga mkono chadema hawana lolote la kuongea. Mfano wa watu
waliomo kwenye kundi hili ni members wa jamiiforums ambao hurusha matusi
kwa kila mtu anayehoji jambo juu ya chadema.

Makundi haya matatu ya bendera fuata upepo huwa ni rahisi sana kuvunjwa
moyo na kukikimbia chama mara tu upepo utakapoelekea upande tofauti. Kwa
mfano, iwapo chadema itafanya jitihada za kuhakikisha jamii inajua
ukweli kuwa siyo chama cha ukanda wala ukabila, basi makundi haya mawili
i) na ii) yatatoweka.
Vilevile iwapo chadema itasambaza elimu ya uraia na kuwawezesha wananchi
kuchagua vyama vyama vya kuviunga mkono kwa hoja, basi makundi yote
iii),ii) na i) itayapoteza.
Hizi ni changamoto zinazohitaji political calculations kudeal nazo.

2. Wale wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za
kisiasa za kitaifa:
Katika kundi hili wamo wanasiasa kama Dr. Wilbroad Slaa na Shibuda.
Misingi ya wanasiasa wa aina hii kuhama kutoka kwenye chama kimoja mpaka
kingine ni kuhakikisha tu kuwa wanaendelea kuwepo kwenye shughuli za
kisiasa katika nafasi za uongozi. Hawana ugomvi wa kiitikadi na CCM.

Kimsingi hawa ni watu ambao iwapo leo hii CCM itawahakikishia kuwa
watapata fursa ya kuwa viongozi wa juu, basi wako tayari kujiunga nayo.
Wamejitoa CCM kwa sababu tu walinyimwa fursa ya kuwa viongozi katika
ngazi walizogombea. Iwapo chadema itawanyima fursa ya kuwa viongozi,
wataikimbia pia.
Mfano mzuri umeonekana hivi karibuni Lushoto ambaye kijana mpya katika
siasa
Deogratius
Kisandu
aliikimbia chadema kwa kukosa fursa za uongozi ambapo
kimsingi alijiunga chadema kwa kuamini kuwa fursa hizo atazipata kwa
urahisi zaidi ndani ya chama hicho.

CHADEMA imekosa uungwaji mkono katika misingi ya itikadi. Hii
imesababishwa na ukweli kwamba cHADEMA imechukua itikadi zilezile za
CCM, TANU na ASP na kushindwa kuwapa wananchi chaguo jipya. Zaidi ya
hayo, hata kwenye ilani za uchaguzi za chadema hakuna offer tofauti na
zile ambazo wananchi wanapewa na CCM. Kuthibitisha hili, chadema imepata
wakati mgumu sana kupokelewa katika maeneo ambayo kuna chama kingine
cha upinzani kilichojijenga kama Zanzibar. Iwapo chadema wangekuwa na
itikadi au sera mpya ambazo utekelezaji wake unaelezeka, isingekuwa
vigumu kupata wafuasi katika maeneo hayo.

Kwa vile CCM imeshapewa fursa ya kutawala, mapungufu yake yameonekana.
Jukumu la chadema kwenye hili linatakiwa ni kuja na mkakati unaoelezea
kwa undani ni vipi watafanya tofauti na CCM. Badala yake, kazi pekee
inayofanywa na chadema ni kuainisha matatizo na kuyahubiri majukwaani
bila kuelezea iwapo wana mkakati wowote mpya ili wananchi waupime. Hii
inasababisha hata wasomi wanapovifananisha hivi vyama wanakosa zile
tofauti za kuzijadili na mwishowe hujadili tabia za viongozi vya vyama
na utendaji wao badala ya kujadili sera zake na itikadi.


Ulaghai wa CHADEMA ni sababu nyingine iliyofanya chama hiki kupoteza
wafuasi makini. Mtu yeyote atakayejaribu kuichunguza chadema kidogo tu
atagundua kuna mambo mengi yasiyofaa yanayofanywa na viongozi wake.
Viongozi hawa hufanya hivi kujinufaisha wao wenyewe na familia zao. Kwa
vile umaarufu wa chadema umetokana na uhubiri wa ufisadi, uwepo wa
ufisadi ndani ya chadema umewavunja sana moyo wananchi walioamini kuwa
wamepata tumaini jipya. Wale wanaoishabikia chadema kwa kufuata upepo
wanapojua ulaghai huu, huvunjwa moyo na kuikimbia. Mfano wa hili ni
kijana Mtela
Mwampamba
ambaye aliamini kuwa chadema ni tumaini jipya mpaka
pale alipojionea mw
 
Ze Marcopollo , Kwani wewe ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CDM ? HOJA zako ni ndefu sana lakini hazina uzito wowote ! Ni muendelezo wa zile siasa zenu za maji taka , umejidhihirisha namna ulivyojaa dharau , kwa kuwaita baadhi kwa jina la WAFUATA UPEPO Maana hawajitambui siyo ! Kwa sisi wengine tunaoifahamu kidogo afya ya binadamu tunaamini kwamba , yeyote anayedhani anafahamu mambo fulani zaidi kuliko wengine basi bila shaka ana matatizo ya akili ! Umekosea sana kwamba kilichomtoa kisandu ni tamaa ya vyeo bali kilichomtoa Mwampamba ni kujitambua ! Very poor analysis !
 
Back
Top Bottom