Chama cha Kilaghai Tanzania...

Chama cha Kilaghai Tanzania...

ZeMarcopolo..umeiweka vizuri sana.tunaweza kua tumeichoka CCM na ufisadi na udhaufu mwingine wa kiuongozi, lakini CDM siyo mbadala wa CCM kwa kutuonyesha madudu hayo ndani ya uchanga wao kama chama cha kitaifa.

washabiki au dillusional supporters of CHADEMA, I should correctly put it that way wanaamini CDM itamaliza matatizo yote ya Tz-elimu, umaskini, afya, ufisadi, maji safi, miundombinu wengi wamezibwa akili na fikra na chuki za watawala waliopo wanashindwa kuuliza CDM na kuangalia udhaifu mkubwa huu wa CDM ikiwemo mambo ya demokrasia ya ndani na ufisadi wao, kutokua wawazi katika maamuzi yao na mengineo uliyoyaonyesha kwenye thread.

Hawa vipofu wanashindwa kujiuliza Je CDM watahitaji kukuza pato la taifa kwa asilimia ngapi na ndani ya muda gani na kwa njia zipi haswa(kwa sababu ukisema tu tukusanye zaidi kodi ndani ya uchumi mwembamba kama wetu haitotosha, ukisema uongeze kodi kwa wawekjezaji haitotosha, ukisema kuokoa tu hela kutokana namatumizi ya v8 na ukubwa wa serikali na yenyewe haitotosha kupata fungu la kufanya yote wanayoamini hawa blind followers wa CDM na hapo unaitaji kukuza uchumi na hii inachukua muda na mikakati mahsusi ambayo sijawahi isikia kwa CDM).

Je hawa CDM wenyewe ni wanasiasa wanaotumia siasa au wanaharakati wanaotumia siasa na baada yha hapo hawataitaji siasa na (mabaya yote yanayoambatana na siasa ikiwemo rushwa) kung'ang;ania madaraka na kujiongezea nguvu huku wakijenga gap kati yao na wananchi? kwanza sijasikia wakisema watawachukulia hatua gani mafisadi wakubwa walioharibu hili taifa na kuna dalili zote wana dine and wine na mafisadi hawa nyuma ya pazia. huu ni uvugu vugu na siyo mapinduzi kama ambavyo sisi wengi tunavyotaka. na historia ya vyama vya upinzani Afrika ni hii hii ya kufeli kuleta mabadiliko, wapinzani wakiingia wanakua mabwana wakubwa wapya na kazi imeisha.

CDM wangekubali kama wenyewe ni wansiasa tu wanaotaka kujaribu uongozi na kuongoza nchi kutokana na dira yao, ambayo haiko tofauti na ya CCM anyway. lakini huku kujifanya na kuwaaminisha wafuasi wao kua wenyewe ni political saints bent on delevering salvation to the long suffering tanzanias ni uongo nisioweza kuuamini mtu kama mimi mwenye akili kidogo za kufikiria.
 
Thats exactly my point. Chadema hawana offer mpya kwa wananchi ndio maana makundi wanayoyavuta ni hayo niliyoyasema.

Kuhusu thread kufungwa usiwe na shaka mkuu. Thread hii HAITAFUNGWA na wala mleta thread HATAPIGWA BAN.
Umefanya vizuri kumjibu Vichazi, kuna watu ni wanafiki sana na wanatia kichefuchefu
 
Baati mzuri chama hicho ( CDM ) kwetu wana pwani tumekidharau. Tunakiona sio mkombozi wetu, ajenda yao ni ileile "zidumu fikra za mwelimu" wakitaka waamini ninacho kisema waangalie mahudhurio ya mikutano yao katika mikoa yote ya pwani na kusini.

ndio maana watu wengi wa pwani hawajaendelea
halafu mnajiona wajanjaa! kumbe walalahoi tu. lakini acha mbaki jinsi mlivyo ili kwenye jamii makundi ya kiuchumi yazidi kuwepo ili mkome vizuri
 
Ze Marcopollo , Kwani wewe ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CDM ? HOJA zako ni ndefu sana lakini hazina uzito wowote ! Ni muendelezo wa zile siasa zenu za maji taka , umejidhihirisha namna ulivyojaa dharau , kwa kuwaita baadhi kwa jina la WAFUATA UPEPO Maana hawajitambui siyo ! Kwa sisi wengine tunaoifahamu kidogo afya ya binadamu tunaamini kwamba , yeyote anayedhani anafahamu mambo fulani zaidi kuliko wengine basi bila shaka ana matatizo ya akili ! Umekosea sana kwamba kilichomtoa kisandu ni tamaa ya vyeo bali kilichomtoa Mwampamba ni kujitambua ! Very poor analysis !
Iko siku mtajua ukweli na itakuwa too late kwani mtakuwa mmeishachangishwa sana kwenye M4C
 
Mkuu ZeMarcopolo naona umetiririka. Sasa tuone hoja kinzani na siyo vioja. Hivi mtu unakuja na hoja kama hii badala ya watu kutoa hoja kinzani mtu anaishia kusema umelipwa kiasi gani! Mtu kama huyui kama hana utapia hoja ni nini?

Uchambuzi huu wa Marcopolo unatakiwa ujibiwe kwa hoja si vioja. Hizi ni chambuzi fikirizi.

Hakuna kufikiri hapo. Aliyosema hapo yameshaongelewa hadi yamechacha. Kwani ya ccm yalishaongelewa yakaisha? Kuna hili jipya la Kibanda na matamshi tata ya mtoto wa Rais. Ni wehu kudhani kuwa hii ni hoja
 
Last edited by a moderator:
Siasa siku hizi imekuwa ni sehemu mojawapo ya ajira kwa vijana,wazee na kinamama na inalipa zaidi uchaguzi ukikaribia.

Kusema chama fulani ni cha kilaghai inaweza kuwa kweli kwa upande fulani na upande fulani ikawa si kweli.

Kwa maoni yangu; Si chadema tu,bali ni vyama vyote nchini vipo kiutapelitapeli,nasema hivi kwa mantiki moja tu ya

kwanini vyama hivi sasa zaidi ya miaka 21 badala ya kujiunga kuwa chama kimoja vyenyewe bado vinaendelea

kung'ang'ania bendera zao na katiba zao ambazo haziwasaidii wananchi.

Kama kweli vyama vya siasa ndio suluhisho la matatizo ya mtanzania hivi ni lini hasa vyama hivi vitajiunga na kuachana na ubinafsi wa vyeo na idadi ya wanachama walionao,kama havitajiunga mapinduzi yanayoongelewa kila siku yatabaki kuwa ni ya chama tawala kuendelea kutawala.

Ukweli ni kwamba kinachoiweka madarakani serikali ya CCM ni udhaifu uliopo katika vyama vya siasa nchini.
 
mkuu nimekusoma vizuri sana,lakini pamoja na kujitahidi kote ulikojitahidi kuunda hoja,hujanishawishi hata kidogo,kwa vigezo vifuatavyo, Mosi, maelezo yako yako kikada zaidi yaani namaanisha yako kiccm zaidi,kwani katika maelezo yako kuna uchungu ndani ya moyo wako kuwa CHADEMA inaungwa mkono sana na vijana hivyo basi kutoa fursa kwa chama hiki kuchukua nchi 2015,hiyo inakuuma sana,pili,umeonesha wivu wa hali ya juu na ummediriki kutumia muda mwingi sana kuelezea yaleyale ambayo mengi yameshatolewa majibu yake na unajitahidi kuyarudiarudia ili kuaminisha watu kuwa hajatekelezwa,tatu,kwa muonekano wa harakaharaka wewe ni mmoja wa masalia waliotimuliwa kwenye chama kwa usaliti ,hivyo unakesha humu kupiga majungu,

Siku zote mfa maji haachi kutapatapa,Tunaomba muda uliotumia kuandika upuuzi huu,uutumie kutueleza sababu za watoto wetu kufeli kwa asilimia 90%,msuli uliotunisha hapa utunishe pia kutueleza ile slogan ya maisha bora kwa kila mtanzania imetekelezwa kwa kiasi gani hapa Tanzania,pia jaribu kutunisha msuli hivyohivyo kutufafanulia mapesa yaliyofichwa uswis ni ya nani na mmechukua hatua gani kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani,

nimekufatilia sana tread zako unazotoa hapa ni za unafiki mkubwa kwani unajua mambo yanavyoendelea hapa nchini na jinsi maisha yalivyo magumu,lakini unataka tukiunge mkono chama chenu kilichosheheni majambazi yanayoua Tembo wetu,yanayotorosha Twiga na wanyama wetu kwenda kutengeneza zoo huko ulaya,na sasa hivi Jambazi mmoja yuko china kujaribu kuokoa shehena ya pembe za ndovu iliyokamatwa huko,haiingii akilini mtu mzima unashindwa kwenda kutafuta mahitaji ya familia yako unakesha humu kupiga majungu na hutoi mstakabali wa hao wanaoiunga mkono CHADEMA wafanye nini,na waunge mkono chama gani ili tuondokane na UJINGA HUU UNAOFANYWA NA MAGAMBA,umekalia kutugredi huyu yuko kundi hili na huyu kundi hili ili uepuke fedheha na matusi nenda kajipange ndio uje kukishawishi kizazi hiki cha DOTCOM Lakini kwa upuuzi huu hutoweza kunishawishi niunge mkono majambazi.
 
bravo mku,umenena mambo ya msingi sana,tunahitaji watu kama nyie kipind hiki cha ulaghai wa kisiasa
 
Ndugu wanaforum Great thinkers; Magamba yanazani yanaweza kutumia propaganda kuinusuru CCM, hayo ni mawazo ambayo ni sawa na mfamaji hakosi kutapatapa. Kwanza kabisa nataka nimJulishe mtoa mada kuwa Chadema siyo chama cha mbumbu ni cha watanzania wote, wakiwemo na wasomi na siyo washenzi waliokwenda shuleni.

Baada ya maneno hayo ya utangulizi naomba nirudi kwenye mada:
unasema chadema ni chama cha kilaghai! unajua nini maana ya Laghai? Laghai anasifa zipi? usitake kutumia Ambiguous and immotional words kuwafanya watanzaia waamini kwamba wewe ni momi, kumbe ni mshenzi aliyekwenda shule. Nani laghai kama CCM walilaghai watanzania kuwa mtaongeza ufaulu zaidi ya 94% wana sifuri na four mbaya sana, mlisema mtaboresha afya zinazidi kuwa hovyo hayo ni machache tu. Badala ya kujukita kwenye kero za wananchi unapoteza muda kuandika "fallacies" Hatudanganyiki!
Pili, chadema siyo chama cha makundi mawili kama unavyotaka kuwaaminisha watanzaia waamini hoja zisizokuwa na supporting evidence.Chadema ni chama cha watanzania wote bilakujali Kabila, dini ,rangi, jinsia, umri na elimu zao ni chama chaukombozi kutoka kwenye mkoloni mweusi CCM. Kudhihilisha hayo, chadema ina wabunge kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania; Unajaribu kuwatoa watanzania kwenye hoja za msingi za maisha yao ya kila siku lakini nakwambia giza haiwe kushindana na nuru mara zote penye nuru giza hupotea;

1.Hoja ya kwanza, wanachama ni bendera hufuata upepo.
CCM imetumia propaganda za udini na ukabila sasa mmeona zinagongamwamba mnaanza kutapatapa, mara wanachama wa dinin fulani , mara wanachama wa kabila fulani No evidence this is called slippery slope fallacy. Unasupport premises na wrong evidences, therefore your conclusions are incorrect, kama unajua nini maana ya deductive reasoning.

Eti watu wanajiunga kamafashion, nini maana ya fashion ? kwa nini hawajiungi na CCM kama ni fashion?Unajaribu kutumia immotional words, no one is going to appeal to immotions. Kiufupi, umetumia appeal to immotional fallacy. Unajaribu kuwadanganya watu kuwa ukiongea na vijana wa chadema, ukiwauliza kwanini uko chadema eti hawana la kusema, ume kaa na nani? wapi? anauwezo gani wa kuchambua mambo? au umekaa na gamba mwenzako mkadanganyana?

Kwa bahati mbaya zaidi, masomo ya sayansi yalikushinda lakini pia inaonekana Historia nayo ulipata 0, Unasema Dr.Slaa likuwa CCM , kwahiyo hawezi kuwa Chadema! huu ni upuuzi kabisa. Umeshindwa hata kukumbuka kuwa enzi za mwalimu kulikuwa na chama kimoja? That is rediculous! na mwaka 2015 atawatoa makamasi naona manatetemeka sana mkisikia jina la Dr.Slaa.

Kwahiyo, ushauriwangu ambao nataka kukupa ni kwamba,be honest, mche Mungu. Watanzania wana matatizo mengi sana, maisha magumu, mafisadi wanazidi kuharibu nchi, Elimu mbovu, afya mbovu, maji shida, umeme shida, mambo mengi sana hata siwezi kuyamaliza.Kwanini usijadili jinsi ya kujikwamua kwenye hizi shida? don't you feel bad? Hii nchi inahitaju umbozi na siyo vinginevyo.
 
CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa misingi ya ulaghai.
10. Wadau wanajiuliza chama hicho cha siasa kinataka nini Tanzania mpaka kikipinge chama kilichoasisiwa na wapigania Uhuru na kutaka chadema iingie madarakani? Ikumbukwe kuwa muasisi wa CHADEMA Mzee Mtei, alikataa kushiriki harakati za kupigania uhuru na pia alikataa kujitolea kuijenga nchi baada ya Uhuru.
11. Hesabu za pesa zinazochangwa na walalahoi kwa ajili ya M4C imekuwa ni jambo la siri kubwa ndani ya CHADEMA.
  • JAMANI ZeMarcopolo nyie miliokuwa huko jikoni au mliotutangulia mngetuwekea Historia vizuri huyu Mzee Mtei baada ya kuanza kazi huko Naoirbi Kenya na kuja kuwa Gavana wa kwanza BOT, akaenda kuwa Katibu EAC na kuja kuwa Waziri wa fedha baada ya kutofautiana na kifimbo na kwenda IMF kumbe alikuwa anatoroka kazi za kupigania UHURU wa Tanganyika au UKOMBOZI kusini mwa Afrika? au nimekuelewa visivyo?



sio Halali kwa kila anayeipinga CHADEMA kuitwa MAGAMBA nyie Mapro kubalini ukweli na muwe mnajibu kwa Hoja sio matusi mtasababisha uzi kufungwa bila kujua nini kisa kumbe mbinu
 
Hayo ni mawazo yako tunayakubali lakini si kwamba ulichoandika ni sahihi ila ni hoja ambayo wenye busara wataisoma na kupima mawazo yako kama wataona yanaegemea upande fulani watajua lakini kama yapo sahihi watakupa grade. pamoja na yote huwezi badilisha wana CCM waliofaidika na CCM kuwa CHADEMA vivyohivyo CDM. kama ukabila undugu na kurithishana ebu jaribu kutafiti tene utaona ukweli upo wapi kwa umri wa wapinzani na CCM utajua wapi wanarithishana na kuanadaana utajua kuna mifumo mingi ktkt chama ambayo huaandana kuchukua madaraka pia vyama vyote vina mifumo ya kupata viongozi na wawakilishi wao pia katiba nayo ina vigezo vyake pia. mfano hapa ruvuma wabunge wa kuteuliwa woote ni wa ccm kwakuwa CCM imechukua majimbo yote ya uchaguzi wa wabunge sasa ukabila unakujaje mkuu tafiti tena kidogo utupe vitu makini
 
Ahadi zisizotekelezeka si ni uongo ambao unaitwa ulaghai? Kwenye sera za uchaguzi mnajua nani waliokuwa na sera nyingi ambazo nyingi hazikutekelezeka hivyo WAONGO ZAIDI
 
Udini na ukanda!? hizi ni propaganda UCHWARA ambazo ccm wanatumia dhidi ya upinzani na tayari zinaigharim Nchi...ccm wanapingwa nchi nzima sasa, kwa kushindwa kucheza turufu yao muhimu 2012, wangefukuza mafisadi hata kiuwongo uwongo(kama kawa) tu ingetosha wao kupumua na kujipanga...hatari tunaelekea 2015 ccm hawana hoja za kueleweka zenye mashiko...hala hala Baba Wa Taifa anaweza akapewa jina jipya la NABII yulee..
 
Hata hiyo bado sio ishu, ishu ni kwamba kama wao wanataka kuwa tofauti na wa CCM wangetuambia kwamba hizi pesa wanazozilipwa za jimbo SIYO halali yao kwa maana wanalipwa ili wawe Ofisini karibu na Wananchi wao Jimboni, na ndio maana ya Mbunge kuwa na Ofisi na sio vinginevyo, sasa Wabunge wa CCM wamekuwa wakitudhulumu miaka yote, wengine miaka 5 hawajawahi kukanyaga Jimboni, na Wapinzani nao hivyo siku ukimuona basi labda Raisi anakuja Jimboni kwake sasa tofauti iko wapi?

Pili kulibadilisha hilo hauhitaji sijui kusubiri sera mpya ya CHADEMA ya Majimbo, ni swala la uamuzi tu, ambao unaweza kufanyika hata leo wakiamua, kwani hata ukiweka Majimbo bado Magavana watakuwa wanaishi Sinza au Kinyerezi, lkn ofisi zao ziko Majimboni.

Tatu hata kama hata kama inabidi waje Dar kushughulikia mambo fulani inaeleweka lkn sio ktk siku 365 ni siku 30 tu ndio wako Ofisini, hilo halina utetezi!

Mwisho mimi sio mwanachama wa Chama chochote bado, ninatoa maoni tu kulingana najinsi ninavyoona!
Ukiangalia takwimu ulizoziweka hapo juu kwenye nyekundu ni sawa na 8+% ya siku zote kwa mwaka.

Sasa kulingana na mazingira ya kiutendaji serikali kuu ni nyingi mno kama zinakuwa za kiutendaji. Hii ni kama takwimu zako ziko sawa.

Kwa lugha nyingine wanakwenda majimboni mwao walau mara mbili kwa mwezi!.

Ukumbuke kuwa hawa wanafanya siasa kuhamasisha na kuimarisha chama maeneo mengine tofauti na majimboni kwao.
Wanahudhuria vikao vya Bunge na Kamati na kufanya kazi za kamati pia lakini walau 30 kuliko wasiokwenda hata mara 10 kwa miaka mitano.

Kuhusu sera ya majimbo usiwahukumu Magavana hewa maana hawa hawatakuwa sawa na wakuu wa mikoa na wilaya wanaosubiriri sherehe na matukio tu ndio wanajulikana kuwa wapo.

Wewe sio mwachama wa chama chochote lakini una ukereketwa, Shutuma nyingi dhidi ya vyama vya upinzani huwa ni Propaganda lakini hakuna wa kuthibitisha.
 
Mimi naona chama 'laghai' ni kile kinachoahidi ahadi nyingi na kushindwa kutekeleza.
Chama fulani kiliahidi 'maisha bora kwa kila Mtanzania'.
Mpaka leo hakuna dalili zozote za kutekelezwa kwa anadi hiyo !!
Hapo ndio unaweza kukiita chama hicho kuwa ni 'laghai'.
Ni maoni yangu tu, msije mkaniteka nyara bure.
 
ZeMarcopolo..umeiweka vizuri sana.tunaweza kua tumeichoka CCM na ufisadi na udhaufu mwingine wa kiuongozi, lakini CDM siyo mbadala wa CCM kwa kutuonyesha madudu hayo ndani ya uchanga wao kama chama cha kitaifa.

washabiki au dillusional supporters of CHADEMA, I should correctly put it that way wanaamini CDM itamaliza matatizo yote ya Tz-elimu, umaskini, afya, ufisadi, maji safi, miundombinu wengi wamezibwa akili na fikra na chuki za watawala waliopo wanashindwa kuuliza CDM na kuangalia udhaifu mkubwa huu wa CDM ikiwemo mambo ya demokrasia ya ndani na ufisadi wao, kutokua wawazi katika maamuzi yao na mengineo uliyoyaonyesha kwenye thread.

Hawa vipofu wanashindwa kujiuliza Je CDM watahitaji kukuza pato la taifa kwa asilimia ngapi na ndani ya muda gani na kwa njia zipi haswa(kwa sababu ukisema tu tukusanye zaidi kodi ndani ya uchumi mwembamba kama wetu haitotosha, ukisema uongeze kodi kwa wawekjezaji haitotosha, ukisema kuokoa tu hela kutokana namatumizi ya v8 na ukubwa wa serikali na yenyewe haitotosha kupata fungu la kufanya yote wanayoamini hawa blind followers wa CDM na hapo unaitaji kukuza uchumi na hii inachukua muda na mikakati mahsusi ambayo sijawahi isikia kwa CDM).

Je hawa CDM wenyewe ni wanasiasa wanaotumia siasa au wanaharakati wanaotumia siasa na baada yha hapo hawataitaji siasa na (mabaya yote yanayoambatana na siasa ikiwemo rushwa) kung'ang;ania madaraka na kujiongezea nguvu huku wakijenga gap kati yao na wananchi? kwanza sijasikia wakisema watawachukulia hatua gani mafisadi wakubwa walioharibu hili taifa na kuna dalili zote wana dine and wine na mafisadi hawa nyuma ya pazia. huu ni uvugu vugu na siyo mapinduzi kama ambavyo sisi wengi tunavyotaka. na historia ya vyama vya upinzani Afrika ni hii hii ya kufeli kuleta mabadiliko, wapinzani wakiingia wanakua mabwana wakubwa wapya na kazi imeisha.

CDM wangekubali kama wenyewe ni wansiasa tu wanaotaka kujaribu uongozi na kuongoza nchi kutokana na dira yao, ambayo haiko tofauti na ya CCM anyway. lakini huku kujifanya na kuwaaminisha wafuasi wao kua wenyewe ni political saints bent on delevering salvation to the long suffering tanzanias ni uongo nisioweza kuuamini mtu kama mimi mwenye akili kidogo za kufikiria.

Dah!! Sred inajivuta taratiib kama vile haiwahusu CDM. Maana kwa uzoefu uliopo, mada yoyote inayotoa challenge kwa CDM, hupokewa kwa kejeli na matusi yasiyotamalika.

Lakini leo naona kiwango cha matusi si kivile nadhani ni sababu zifuatazo:

Kwanza; Mada ni mahsusi kwa wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo kitu ambacho wengi wa wafuata upepo, hawana ubavu.

Pili; Mada ni ndefu kiasi ambacho wafuata upepo hawana ubavu wa kuisoma soma yote Kwa sababu haiko kimipasho na kimatusi ambayo ndo fani ya wafuata upepo wengi.

Na tatu ni kwa kuwa mada inahitaji uwe na uwezo mkubwa wa kiakili na sio kukariri na hivyo kuwashinda wafuata upepo wengi.

Ni hayo tu.
 
Mkuu ZeMarcopolo,

Pilipili iko Shamba wewe inakuwashia Nini.

Laknin Hebu tugeuke upande wa Pili.

Aina za Supporters wa CCM

1. Watu wasio na Elimu ya Kutosha e.g Wale Wa Mama na wazee wanaodanganyika kwa Kanga, Pila, Vitumbua n.k

Reffer uchaguzi mdogo wa Igunga na Uchaguzi Mkuu 2005 na 2010.

2. Ukiwa CCM lazima uwe Muongo na Mnafiki

Reffer ahadi ya Mahakama ya Kadhi, huu ulikuwa ni Uongo Mtakatifu
Reffer Kauli ya Mwenyekiti wenu, "Nawajua wauza Madawa ya Kulevya" Lakini hadi leo Kimyaa na Wadogo zetu Mateja wanazidi kuongezeka Mitaani.
Kuna mengi tu hapa nadhani kuna watu watakua ku add

3. Ukiwa CCM Adabu inaondoka na unakuwa mtu wa Hovyo sana, hii ni Credit ya ku Prosper ndani ya CCM

Reffer Mwigulu na Matusi yake, Reffer Jerry Silaa na Matusi yake Nape Nnauye etc etc.

4. Ukiwa CCM unakuwa Kipofu Kabisa na kushindwa Kung'amua na kusoma alama za Nyakati

Reffer wewe Mwenyewe jinsi ulivyo.
5. Ni Wachumia tumbo na Wa Ganga Njaa tu ndo waliobakia na Mapenzi ya Dhati kwa CCM

Mwisho Kabisa, Mtakesha kila siku Kukipaka Matope CHADEMA, Kwa taarifa yako watu tuna Support CDM simply because kinaongea Lugha ya Wa Tanzania.
Watu wanataka watu wawajibishwe kwa Kusafirisha Twiga, Biashara ya Meno ya Tembo.
Wa Tanzania wanataka wezi wa EPA wajibishwe, DeepGreen Finance, Richmond, na Mikashfa Kibao tu.
CCM iko Kimyaaa, Mtanzania gani gani mwenye akili Timamu ataendelea ku support CCM, lazima atakuwa na Sababu inayo fall kwenye Categories nilizoeleza.
Kile wanachosema CDM ndo kipo katika Mahitaji Muhimu ya Wa Tanzania, We kaa Piga Domo hapa CDM Kitaendelea kuwa Moto wa Kuotea Masafa Marefu.
Tunajikita Vijijini Kujenga Chama, Kelele zenu wala haziturudishi Nyuma, Response ya Umma ndo Ngao na Muongozo wetu.
Machapisho ya Waganga Njaa na Wachumia Tumbo kama wewe wala hayatutishi na Kutustua.

PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS
 
Hata mfanye nini chadema haiwezi kufa. Tafuteni ajenda nyingine. Hapo mmeshindwa. Tena sehemu yenyewe JF, nani anaweza kusikiliza habari za majungu.
 
Back
Top Bottom