Chama cha Kilaghai Tanzania...

Chama cha Kilaghai Tanzania...

Mkuu bado hujanifungua macho, what is the way forward? Umeelezea matatizo ya CHADEMA, fine, mbona hutaki kutuambia tufanyeje baada ya hapo. Tupe fikra mbadala basi!!

Swali zuri.
Swali hilo litajibiwa katika thread nyingine ambayo Mungu akipenda italetwa hapa JF mwezi wa sita mwaka huu.
Utafiti wake bado unaendelea.
 
Mkuu mbona unataka kulinyima jukwaa fursa ya kujadili mambo? Yaani ulitaka ZeMarcopolo aende kuwatafuta wanachama wa CHADEMA mitaani na kuwaambia hayo? Nadhani hapa kuna wana CHADEMA ambao wanaweza kutusaidia kujibu huu "upuuzi" wa mtoa hoja.

Labda wewe na ZeMarcopolo lenu moja, ni mwana Chadema wa ajabu sana atayejihusisha na hoja za mtu anayejulikana kuwatetea wahujumu Chadema
 
Jelyfish hapo ndiyo uwezo wako wa uchambuzi wa thread ulipoishia kweli ? Mimi siamini bhana ! Una uwezo zaidi ya huo , hebu rudi tena kwenye huu uzi bhana , Zemarcopollo anasema kwamba Kisandu (aliyehamia NCCR mAGeuzi ) kaondoka Cdm kwa ajili ya Tamaa ya Madaraka, bali Mwampamba (aliyehamia CCM ) kaondoka cdm baada ya kuona Madudu , kweli ndivyo ilivyokuwa ? Siyo thread bora bhana ! Mwandishi amesukumwa na ama Posho au Maslahi ya kisiasa .

Huo ndio ukweli, ila wanapofushwa ufisadi, rushwa, undugu kwa maana ndugu zao kufanya kazi ndani ya ccm tena kwa kupewa upendeleo. But all in all what we are discussing is not the solution for the problems facing our Nation. We are wasting our time in useless issues like this.
 
unapaswa kujiongeza sio kila jambo utafuniwe. Inshort, amejaribu kuonesha mapungufu hayapatikani ccm tu hata vyama vingne km cdm. Pia uone kwmba cdm ni chama chenye maslahi ya watu wachache na muelekeo wake ni wakibinafsi zaidi wanapaswa kubadilika km wanahitaji dola. Lkn mpk sshv dola kwao itabaki ndoto,hawana mkakati wa kuwafikia mwananchi wameanzisha uongozi wa kanda ambao bado ni centralizatn,ccm wamedecentralize mpk kwa balozi wht do u espect?

Asante mwalimu kwa kusaidia ufafanuzi...
 
Zemarcopolo!Asalaam aleykum!
Nimejaribu kuupitia uzi wako bi maana ya hoja zako hakika nathubutu kusema kwamba kuna utovu mkubwa wa mashiko katika hoja zako.

Awali ya yote umetanabahisha kuwa CDM kinaendeshwa kwa misingi ya ulaghai, je ni nani anafanya ulaghai and to what end?
Je tunaifahamu tafsiri ya chama kiasi kwamba endapo one individual akitenda kosa basi huo ni utakuwa utendaji wa chama husika?.
je una imply ya kwamba chadema ni chama kinachomilikiwa na watu wachache na wanakatiba na malengo yao ya siri ambapo the rest of sympathizer wake hawatakiwi kuyajua?
Hakika hapo umefanya al-jumala ya tukio moja na kulazimisha kuwa hiyo ndiyo sura halisi ya CDM.

Umejiaminisha kuwa CDM inaungwa mkono na makundi mawili,kundi bendera na kundi vyeo.

Kundi bendera-wakabila,

Unataka kutuambia ya kwamba CDM inawachama ,wafuasi,wapenzi kutoka sehemu moja tu ya tanzania? Na tunaposema propaganda za kukichafua,nani anafanya hizo propaganda? Hutokubaliana na mimi kuwa chama kitakachokuwa kina
fanya propaganda za kuichafua CDM kikabila na kidini kuwa hicho ndicho chama chenye udini na ukabila pia kilaghai?

katikavuguvugu la kisiasa ,hasa mageuzi ya kisiasa kuna sehemu zinakuwa na mwamko mkubwa,hakuna chama kinachoweza kuachia sehemu zenye majority ya suppoter wake bila kuwapa special attention.

Na umenichosha zaidi katika uanisho wako wa kundi la vijana,kwamba wanafikiri chadema ni fashion,hivi kweli wewe unafikiria vijana wa chadema sawa na CCM kuwa watavaa sare za chama,watapiga picha na nape,watacheza kwaya ya captein Lulu.tena unatumia kigezo cha majibu chukizi uyapatayo kutoka kwa member wa JF ambao kiukweli si wasemaje au wawakilishi wa vijana wote wa chadema (idadi ya vijana wa chadema haiwezi kuwakilishwa na mawazo huru ya JFmembers 100000).

Katika hitimisho lako ni kwamba umeliweka kanakwamba members wote wa CDM wanajua kuwa chama chao ni cha kilaghai,cha kidini,cha kikabila na kwamba siku wakijua kupitia juhudi ya chama chenyewe kuwa si kama wanavyofikiri basi watakikimbia !wewe wa ukweli wewe?yaani watanzania wanataka chama cha udini,ulaghai ukabila na members wote wa chadema lazima wawe na nafasi za utawala!mlinganyo kama huo una exist wapi duniani ?
unatuaminisha kuwa watu wako CDM kwa kuwa tu ni mbumbumbu wa elimu ya uraia ?

Kwenye kundi la madaraka naomba niipinge hoja yako kwa swali moja tu.

Hivi unajua kwamba watu walijitoa ,japokuwa wenyewe mnaita mliwafukuza ccm kabla hata kuingia mfumo wa vyama vingi tena wapo mliowafunga na wengine vizuzini na baadhi kuwafanya wakimbizi.

In short watu walitaka mabadiliko tokea enzi ya mfumo wa cham kimoja.
Chadema haijakusa uungwaji mkono Zenji,tupo wenyewena sijuiunaongea nini inaelekea hujui chochote kuhusiana na siasaa za zenji ,hilo darsa lingine panapo majaaliwa.

Na kuhusu offer tofauti mi naamini mahitaji ya nchi na wananchi hayatobadilika kwa kigezo cha itikadi ,ugomvi ni utekelezaji ya majukumu ya ki nchi na huo ndio ugomvi wetu kwani nyie mmeshindwa hata kama ilani yenu na itikadi yenu ni njema-tatizo inaishia kwenye makaratasi na majukwaa ya siasa or TBC CDM imelenga ku deliver kile wananchi wanachokitaka na serikaki yao ya CDM imewaahidi.

Mifano yako ya ulaghai ime base katika isolated cases na umetaja majinaya wahusika hapo siwezi kujengea mfumo mzima wa chama kwa case za baadhi ya watu fulani ambao kwa namna moja au nyingine hawajaridhia na ni haki yao kuhama lakini hao hawawakilishi kundi kubwa la wanachama ,si kweli kila mtu anataka kuongoza!

Nawasilisha.
 
Ndugu umetoa maelezo mengi ambayo sio mageni sana kwetu ebu naomba nifafanulie yafuatayo

1.Kuna kundi umesema linataka kupanda haraka kisiasa na hapo hapo umesema ni chama cha Kilaghai inakuwaje mtu atake kupanda kisiasa kwenye chama cha kilaghai ambacho kwa mtazamo wako akina mvuto wala mwelekeo?

Chama hicho cha kilaghai kinamlipa katibu wake mkuu mamilioni ya shilingi kila mwezi.
Hujasoma thread za misuguano ya ndani ya chadema ya kugombania kushirikishwa kwenye safari za M4C? Hizi ndio sababu zinazowafanya hao wanasiasa kutaka kupanda kisiasa.
 
Chama chenye ulaghai kiko huku.....Mengine yote ni political diversions za kusahaulisha wa-Tanzania kuhusu ahadi zao.
Tembelea
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-za-jk-nape-tuambie-zimetekelezwa-ngapi.html

ZeMarcopolo njoo ujibu hoja za 'ulaghai' huku.

Copy:
Kimbunga

1 Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga � Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani � Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma � Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma � Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng�ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha � Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti � Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) � Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania � Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda � Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Hizo kwenye red naona zimetekelezwa! Kumbe JK ametekeleza nyingi na anaendelea kutekeleza wakati anakombelezea urais wake.
 
Umekosea sana kwamba kilichomtoa kisandu ni tamaa ya vyeo bali kilichomtoa Mwampamba ni kujitambua ! Very poor analysis !
Erythrocyte
Kilichomtoa Kisandu alikisema yeye mwenye sio mimi na Mwampamba sasa hivi anazunguka nchi nzima kuelezea alivyokuwa disappointed.
Kwahiyo hapo sio kwamba mimi nina poor analysis kama ulivyosema ila wewe huna taarifa za kutosha. Jaribu kusoma thread zinazohusu watu hao wawili kwanza kabla hujalikosoa chapisho la leo.
isome pia ile thread aliyoanzisha Kisandu baada ya kupewa cheo NCCR.
 
Last edited by a moderator:
ZeMarcopolo wewe ndie una dalili zote za kuumwa ugonjwa wa kufuata upepo, kipindupindu cha uongo na uzandiki dhidi ya CDM na Kichocho cha hofu juu ya nini atakachowafanya kiongozi wa CDM akiingia madarakani!!

Mbinu hizi za kufarijiana haziwasaidii, mie mtumishi wa umma niko kijijini, hapa kijijini sie watumishi wa umma wote tunaiunga mkono CDM wanakijiji ndio usiseme! unaongea nini wewe mtu mdogo!
 
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
 
ZeMarcopolo..umeiweka vizuri sana.tunaweza kua tumeichoka CCM na ufisadi na udhaufu mwingine wa kiuongozi, lakini CDM siyo mbadala wa CCM kwa kutuonyesha madudu hayo ndani ya uchanga wao kama chama cha kitaifa.

washabiki au dillusional supporters of CHADEMA, I should correctly put it that way wanaamini CDM itamaliza matatizo yote ya Tz-elimu, umaskini, afya, ufisadi, maji safi, miundombinu wengi wamezibwa akili na fikra na chuki za watawala waliopo wanashindwa kuuliza CDM na kuangalia udhaifu mkubwa huu wa CDM ikiwemo mambo ya demokrasia ya ndani na ufisadi wao, kutokua wawazi katika maamuzi yao na mengineo uliyoyaonyesha kwenye thread.

Hawa vipofu wanashindwa kujiuliza Je CDM watahitaji kukuza pato la taifa kwa asilimia ngapi na ndani ya muda gani na kwa njia zipi haswa(kwa sababu ukisema tu tukusanye zaidi kodi ndani ya uchumi mwembamba kama wetu haitotosha, ukisema uongeze kodi kwa wawekjezaji haitotosha, ukisema kuokoa tu hela kutokana namatumizi ya v8 na ukubwa wa serikali na yenyewe haitotosha kupata fungu la kufanya yote wanayoamini hawa blind followers wa CDM na hapo unaitaji kukuza uchumi na hii inachukua muda na mikakati mahsusi ambayo sijawahi isikia kwa CDM).

Je hawa CDM wenyewe ni wanasiasa wanaotumia siasa au wanaharakati wanaotumia siasa na baada yha hapo hawataitaji siasa na (mabaya yote yanayoambatana na siasa ikiwemo rushwa) kung'ang;ania madaraka na kujiongezea nguvu huku wakijenga gap kati yao na wananchi? kwanza sijasikia wakisema watawachukulia hatua gani mafisadi wakubwa walioharibu hili taifa na kuna dalili zote wana dine and wine na mafisadi hawa nyuma ya pazia. huu ni uvugu vugu na siyo mapinduzi kama ambavyo sisi wengi tunavyotaka. na historia ya vyama vya upinzani Afrika ni hii hii ya kufeli kuleta mabadiliko, wapinzani wakiingia wanakua mabwana wakubwa wapya na kazi imeisha.

CDM wangekubali kama wenyewe ni wansiasa tu wanaotaka kujaribu uongozi na kuongoza nchi kutokana na dira yao, ambayo haiko tofauti na ya CCM anyway. lakini huku kujifanya na kuwaaminisha wafuasi wao kua wenyewe ni political saints bent on delevering salvation to the long suffering tanzanias ni uongo nisioweza kuuamini mtu kama mimi mwenye akili kidogo za kufikiria.

Yote uliyosema ni sahihi:
1. Umenikumbisha bajeti ya chadema ya upinzani bungeni iliyokuwa na matumizi lakini haina vyanzo vya mapato. Baadae walisema wamesahau. Can you imagine mtu anatengeneza bajeti bila vyanzi vya mapato!!!

2. To wine and dine na "mafisadi" umenikumbusha Mabere Marando wa chadema ambaye akipanda jukwaani anawasimanga mafisadi lakini akienda mahakamani yuko mstari wa mbele kuwatetea. Marando anakesha akibuni mbinu mbalibali za kuhakikisha "mafisadi" wanashinda kesi.
 
ndio maana watu wengi wa pwani hawajaendelea
halafu mnajiona wajanjaa! kumbe walalahoi tu. lakini acha mbaki jinsi mlivyo ili kwenye jamii makundi ya kiuchumi yazidi kuwepo ili mkome vizuri
JJB
Unaposema watu wa Pwani wengi hawajaendelea inamaana kuna watu wa sehemu nyingine wameendelea. Je, maendeleo ya hao watu wasio wa Pwani yana uhusiano wowote na jitihada za serikali?
I will appreciate an example of such places.
Regards...
 
Last edited by a moderator:
Aaah Mkuu Molemo huwezi kujibu hoja hizo kwa jinsi hii. Nadhani una cha kuchangia hapa kuliko hiki ulichokiandika!

Kaka Kimbunga
Hata Edwin Mtei yupo hapa anafuatilia, lakini hawezi kuwa na la kujibu.
Kwenye ukweli, uongo hujitenga. Aje aseme kama hakukataa kushiriki katika harakati za kupigania Uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Humu mbona mashabiki wamo wengi sana awajui a wala b wanafata mkumbo tu haya acha tuone...yani wao matusi tu jamani tuwasamee tu ni ndugu zetu tusiwatenge tuwabebe hvyo hvyo
 
Mtoa mada unaonekana kuiandama CHADEMA kwa hoja ambazo hazina tija kwa mtanzania wa sasa.1992 watanzania tulikubaliana kuingia katika mfumo wa vyama vingi na kwamba chama kitacho shinda uchaguzi kitaongoza nchi na vyama vingine vitakuwa vya upinzani.
Sina hakika kama unaelewa majukuu sahihi ya vyama vya upinzani,na demokrasia kwa ujumla.NAomba urejee somo la uraia upanue uelewa wako kwenye maeneo hayo uache kuja na porojo ambazo hazina tija kwa mtanzania wa sasa.
Jaribu kujikita kuelezea mafanikio ya chama tawala na changamoto,pia jinsi ya kukabiliana na vikwazo vinavyojitokeza.
Mtakuwa mnatupotosha kuifanya CHADEMA kuwa kikwazo; mtakuwa mnatupotezea mda watanzania kwa maana tunamahitaji mengi ya msingi ambayo hayana majibu then mnapambana na CDM!"Shame on you" kutupotosha kuwa wanachama wa CDM wana aina mbili kama ulivyo categorize,Wa CCM wapo wa aina ngapi?
Tuje na hoja zitakazo ikwamua Tanzania katika kadhia tulionayo sasa baada ya miaka 51 ya uhuru na si kuidhoofisha upinzani.
Naomba kuwasilisha.
 
Huu uzi umejaa hoja za msingi ambazo zinaitaji majibu ya kisomi kuliko porojo.
 
Back
Top Bottom