mshikachuma
JF-Expert Member
- Dec 2, 2010
- 2,853
- 638
Wa Tanzania kwa Sasa hawahitaji Mipasho.Dah!! Sred inajivuta taratiib kama vile haiwahusu CDM. Maana kwa uzoefu uliopo, mada yoyote inayotoa challenge kwa CDM, hupokewa kwa kejeli na matusi yasiyotamalika.
Lakini leo naona kiwango cha matusi si kivile nadhani ni sababu zifuatazo:
Kwanza; Mada ni mahsusi kwa wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo kitu ambacho wengi wa wafuata upepo, hawana ubavu.
Pili; Mada ni ndefu kiasi ambacho wafuata upepo hawana ubavu wa kuisoma soma yote Kwa sababu haiko kimipasho na kimatusi ambayo ndo fani ya wafuata upepo wengi.
Na tatu ni kwa kuwa mada inahitaji uwe na uwezo mkubwa wa kiakili na sio kukariri na hivyo kuwashinda wafuata upepo wengi.
Ni hayo tu.
Ulichoandika hapo ni mtazamo wako ambao hata sisi tunaoiamini CDM tunaweza tukaandika mtizamo wetu kuhusu CCM na ndio maana ukiwauliza vijana wengi wa CCM ni kwa nini wanaipenda CCM hutopata majibu au utapata majibu ya kuchekesha. Mimi ninaiamini CDM na sitaacha kuiamini kwa sababu sioni namna ambapo CCM inaweza kututoa hapa tulipo na kutupeleka kule tunakotarajia. Hizo ni propaganda za kijinga ambazo hazina uhakika zenye lengo la kuwaondoa wasio na akili ya kufikiri ili wakiweza waendelee kushabikia upuuzi wa CCM.
Watu wengi wanaojitambua iwe ni serikalini au nje ya serikali wanajua mapungufu ya CCM na wanaamini kama ninavyoamini mimi kuwa CCM imeishiwa uwezo wa kuongoza nchi hii. Wasomi wengi hata kama hawasemi wazi lakini wanatambua hilo kuwa CCM si lolote na si chochote katika kutuletea maendeleo.
Ushahidi upo mwingi kuwa CCM haiwezi tena, angalia katika sekta zote kama kuna maendeleo ya wazi yanayoletwa. Angalia sekta ya elimu, angalia sekta ya afya, angalia kilimo, n.k huwez kuona maendeleo yanayotuwezesha kujisifu. Angalia asilimia kubwa ya wabunge wa CCM wakiwa bungeni, kazi yao ni kuitetea serikali katika kila jambo na si kuwatetea wananchi. Hiyo ndio sababu kubwa ya kuichukia CCM na mambo yake na sio propaganda unazojaribu kuwaaminisha watu.
Lakini pia ukiangalia kwa makini, utabaini kuwa CDM wanategeamea watu yaani wanafanya siasa za watu r, sera baadaye. Hii ndo inafanya watu kama Slaa kujiona kuwa wao ni zaidi ya Chadema na anafanya atakavyo kwa sababu tu bila yeye hakuna Chama. Kimsingi huu ni udhaifu uliopitiliza.
Pia hivi sasa let's say kwamba Wachaga waache au wasiendelee kuwa na matumaini na Chadema, itakuwa na hali gani? Au wakatoriki wanaomchukulia Slaa kama tumaini lao, wakiacha kuamini hivyo, Chadema itakuwa na hali gani?
Wa Tanzania kwa Sasa hawahitaji Mipasho.
.
Wa Tanzania wanataka Kujua nini Hatma ya Waliotorosha Wanyama Mchana kweupeee
Wa Tanzania wanataka kujua nini hatma ya Wale walio fuja Kodi zao kwa Kuingia Mikataba ya Kipuuzi kama Richmond.
Wa Tanzania wanataka watu (CCM) wawajibishwe kwenye Kashfa za Meremeta, Deep Green Finance, EPA etc etc.
Wa Tanzania wanataka watu (CCM) wawajibishwe kwa kucheza na Elimu yetu na kusababisha tuwe na Taifa la Wajinag Kabisa.
Haya yote yamefanywa na CCM, badala ya Kuhoji haya, WAPUUZ.I wanakuja na Thread kama hizi.
ZeMarcopolo kwa sisi tunaomfahamu tokea Ilboru hadi MUCHS wala hatushangai kuona kila siku anapoteza Muda ku i atack CDM ilhali CDM haijawahi kuongoza Nchi.
Anajaribu kuzuia Upepo kwa Mikono
Ukiangalia takwimu ulizoziweka hapo juu kwenye nyekundu ni sawa na 8+% ya siku zote kwa mwaka.
Sasa kulingana na mazingira ya kiutendaji serikali kuu ni nyingi mno kama zinakuwa za kiutendaji. Hii ni kama takwimu zako ziko sawa.
Kwa lugha nyingine wanakwenda majimboni mwao walau mara mbili kwa mwezi!.
Ukumbuke kuwa hawa wanafanya siasa kuhamasisha na kuimarisha chama maeneo mengine tofauti na majimboni kwao.
Wanahudhuria vikao vya Bunge na Kamati na kufanya kazi za kamati pia lakini walau 30 kuliko wasiokwenda hata mara 10 kwa miaka mitano.
Kuhusu sera ya majimbo usiwahukumu Magavana hewa maana hawa hawatakuwa sawa na wakuu wa mikoa na wilaya wanaosubiriri sherehe na matukio tu ndio wanajulikana kuwa wapo.
Wewe sio mwachama wa chama chochote lakini una ukereketwa, Shutuma nyingi dhidi ya vyama vya upinzani huwa ni Propaganda lakini hakuna wa kuthibitisha.
hizo hoja zenu tutazijibu after 2015 baada ya ww na kamanda ZeMarcopolo kuwa kuwa uhamishoni Msumbiji kwenye hifadhi ya muda.
Kwangu mimi hii thread ndio bora kabisa katika zote nilizowahi kuzisoma JF. Mwandishi amechambua kisayansi na nirahisi kujua ukweli huo. Utatukanwa lkn ukweli utabaki palepale. Hata Mhe. Mbowe alikiri kuwa staili wanayotumia kwenye siasa inaleta picha mbaya kwenye jamii. Kukumbatia ukanda, ukabila na udini ni suluhisho la kushindwa katika siasa.
hata chadema ingekuwa inalaghai vp , ukweli ni kwama ndio chama mbadala ambacho kinaweza kukabidiwa nchi. CCM hata kama kingekuwa kina mazuri ya namna gani , ukweli ni kuwa kimeisha chokwa na watu wengi . kimekaa madarakani kwa muda mrefu watu wamekichoka haijalishi kinafanya mazuri namna gani , huu ni mtazamo wa fikr za kawaida kwa mwanadamu inafika pahala watu wanakuchoka tu , CCM pisha kidogo mfano tumeuona kenya , majina makubwa ya miaka nenda miaka rudi watu huyachoka
emarcopolo
Lini CDM waliunda serikali na kukusanya kodi ni inakuwaje unawapima na magamba waliokusanya kodi na kutumia rasilimali kwa miaka 50 bila maendeleo stahiki kuonekana.
Mkuu bado hujanifungua macho, what is the way forward? Umeelezea matatizo ya CHADEMA, fine, mbona hutaki kutuambia tufanyeje baada ya hapo. Tupe fikra mbadala basi!!