Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,464
Miaka 20 sasa tangia chama cha siasa CHADEMA kupata usajili wa kudumu. Chama hiki kimepitia mikiki mingi sana ya kisiasa. Siku za mwanzo wengi waliogopa hata kuitwa wapinzani kwa hofu ya kupoteza kazi, biashara, au hata kupata mikopo ya shule, huduma za jamii kama hospitali na haki za kisheria. Leo hii tunashuhudia kukomaa na kukua kwa chama na tunawashukuru wananchi wote waliojitoa muhanga kukiunga mkono kwa siri na kwa uwazi uliotukuka. Hongera viongozi shupavu na mashujaa waliokubali kupitia, mateso, majaribu na mahangaiko yote.
Chama hiki kikiamini katika demokrasia ya kweli, uwazi na utawala wa kufuata sheria, haki na usawa kwa jamii, kinajipambanua wazi kwa kuzifuata na kuzisimamia sheria za chama na kanuni. Chama hiki kinachojiandaa kuchukua dola ni lazima kijidhihirishe kwa wananchi kuwa kinauwezo wa kusimamia sheria za ndani za chama chake na kanuni kabla hakijapewa dola.
Swala la kugombea udiwani, ubunge, Uraisi umeanishwa ndani ya katiba ya chama na ni haki ya kila mwanachama hai kuchukua form na kugombea chochote kwa kufuata sheria kanuni na taratibu za chama. Hakuna anayebaguliwa wala anayeandaliwa, kwani chama ni mimi na wewe na wapiga kura ni mimi na wewe.
Ikumbukwe tu kwa kila jambo kuna wakati wa kupanda, kupalilia na kuvuna. Ni vyema kila mmoja akajua vipindi hivi kwani sio jambo jema kuanza kutaka kuvuna mbegu. Wakati wengine wako shambani kulima na kupanda na kupalilia wengine wanafikiria kuvuna bila kujua huwezi vuna bila kupanda. Chama kwa sasa kipo kwenye mikakati ya kujenga chama, kufungua mashina na kutangaza sera zake kwa wananchi hasa sehemu ambazo chama bado ni kichanga.
Chama hakina matatizo na yeyote mwenye nia njema ya kugombea nafasi yeyote ndani ya chama, hasa mwenye nia safi na dhahiri ya kukikuza kukienzi na kuthamini utu wa mtanzania asiye na tamaa wala ubaguzi, ghiliba, na mgombanishi, ila ikumbukwe sio wote wasemao bwana bwana wana mpenda Mungu. Chama hakiko tayari kuvurugwa wala kujiingiza kwenye malumbano na mtu yeyote yule mwenye nia ya kututoa kwenye mwelekeo wa kujenga chama. Mwaka 2015 si mbali na wakati ukifika milango itakuwa wazi kwa yeyote yule kuchukua form aipendayo.
Kwa sasa kama kweli wewe ni mwana-Chadema wa kweli na kiongozi, diwani, Mbunge wa kweli wa CDM ni wakati wa kujenga chama sio kuanzisha malumbano yasiyo na tija wala mwelekeo, nani atashinda bila wanachama hai na wapenzi wa ukweli? Bila kufungua matawi na ngazi ya awali ya chama. Tuache wafu wazike wafu wao. siasa za maji taka na kujibizana na wanaotakia mabaya chama hakutajenga chama.
chief Mkwawa Wa Kalenga