Chama cha demokrasia na maendeleo-cdm-na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha demokrasia na maendeleo-cdm-na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, May 20, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Miaka 20 sasa tangia chama cha siasa CHADEMA kupata usajili wa kudumu. Chama hiki kimepitia mikiki mingi sana ya kisiasa. Siku za mwanzo wengi waliogopa hata kuitwa wapinzani kwa hofu ya kupoteza kazi, biashara, au hata kupata mikopo ya shule, huduma za jamii kama hospitali na haki za kisheria. Leo hii tunashuhudia kukomaa na kukua kwa chama na tunawashukuru wananchi wote waliojitoa muhanga kukiunga mkono kwa siri na kwa uwazi uliotukuka. Hongera viongozi shupavu na mashujaa waliokubali kupitia, mateso, majaribu na mahangaiko yote.

  Chama hiki kikiamini katika demokrasia ya kweli, uwazi na utawala wa kufuata sheria, haki na usawa kwa jamii, kinajipambanua wazi kwa kuzifuata na kuzisimamia sheria za chama na kanuni. Chama hiki kinachojiandaa kuchukua dola ni lazima kijidhihirishe kwa wananchi kuwa kinauwezo wa kusimamia sheria za ndani za chama chake na kanuni kabla hakijapewa dola.

  Swala la kugombea udiwani, ubunge, Uraisi umeanishwa ndani ya katiba ya chama na ni haki ya kila mwanachama hai kuchukua form na kugombea chochote kwa kufuata sheria kanuni na taratibu za chama. Hakuna anayebaguliwa wala anayeandaliwa, kwani chama ni mimi na wewe na wapiga kura ni mimi na wewe.

  Ikumbukwe tu kwa kila jambo kuna wakati wa kupanda, kupalilia na kuvuna. Ni vyema kila mmoja akajua vipindi hivi kwani sio jambo jema kuanza kutaka kuvuna mbegu. Wakati wengine wako shambani kulima na kupanda na kupalilia wengine wanafikiria kuvuna bila kujua huwezi vuna bila kupanda. Chama kwa sasa kipo kwenye mikakati ya kujenga chama, kufungua mashina na kutangaza sera zake kwa wananchi hasa sehemu ambazo chama bado ni kichanga.

  Chama hakina matatizo na yeyote mwenye nia njema ya kugombea nafasi yeyote ndani ya chama, hasa mwenye nia safi na dhahiri ya kukikuza kukienzi na kuthamini utu wa mtanzania asiye na tamaa wala ubaguzi, ghiliba, na mgombanishi, ila ikumbukwe sio wote wasemao bwana bwana wana mpenda Mungu. Chama hakiko tayari kuvurugwa wala kujiingiza kwenye malumbano na mtu yeyote yule mwenye nia ya kututoa kwenye mwelekeo wa kujenga chama. Mwaka 2015 si mbali na wakati ukifika milango itakuwa wazi kwa yeyote yule kuchukua form aipendayo.

  Kwa sasa kama kweli wewe ni mwana-Chadema wa kweli na kiongozi, diwani, Mbunge wa kweli wa CDM ni wakati wa kujenga chama sio kuanzisha malumbano yasiyo na tija wala mwelekeo, nani atashinda bila wanachama hai na wapenzi wa ukweli? Bila kufungua matawi na ngazi ya awali ya chama. Tuache wafu wazike wafu wao. siasa za maji taka na kujibizana na wanaotakia mabaya chama hakutajenga chama.

  chief Mkwawa Wa Kalenga
   
 2. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hoja imekubalika,kila jambo linautaratibu na wakati wake.
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  "Kukaa kimya ni jawabu tosha kwa mjinga."
  Ninawapongeza wale wote wnaokaa kimya kujibu hoja
  na viroja vinavyokuzwa na wasioitakia mema CDM.
  Ni bora haya ya kulumbana muwaachie walumbanaji.
  Wengine wakilumbana, CDM wajenge chama,
  siku waki(onekana ku)patana, CDM ichukue
  "visanduku" wakavune.
   
 4. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,715
  Likes Received: 17,763
  Trophy Points: 280
  Mi bana nitakufa na CDM, embu ona makamanda wake walivyo na mawazo chanya, heshima mbele Chief Mkwawa,najivunia kuwa na watu kama wewe humu JF. Ngoja niifowadi hii kwnye e-mail ya Shibuda
   
 5. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimeupenda saaana mtazamo wako kwani hata mimi ndio mtazamo niliokuwa nao akilini. Big up!!!!!!
   
 6. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Napenda sana mawazo ya wanaCDM,hakika haya mawazo ya chief Mkwavinyika ni darasa tosha kwa wanachadema,kwamba uwajibikaji wa wanachama ni mpango mzima wa CDM kuchukua dola 2015 huku kikiwa chama madhubuti chenye sura ya kitaifa na kimataifa.
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  bravo chadema.
   
 8. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,672
  Likes Received: 2,207
  Trophy Points: 280
  big up men!
  Huo ni mtizamo wa kiongozi !
  Ww hata kama c kiongoz kitaifa ni kiongoz katka jamii .
  Big up men
   
 9. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kama lengo ni kukuza demokrasia zitto mlitumia mizee yenu kumuomba asigombee uenyekiti taifa kipindi kile cha uchaguzi?
   
 10. Ciphertext

  Ciphertext Senior Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umefikiri sahihi na ukaandika vizuri. Mungu akuzidishie ufahamu wa mambo kwa usahihi.
   
 11. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Mleta thread una akili sana so inabid nifunge maombi ya mnyororo kukuombea kwani unafaa na nina iman utakuja kuwa kiongozi mzuri sana kwani una mawazo yenye kujenga na kutuliza hasa ktk hiki kipindi ambacho wavuta bangi kama shibuda wanapofanya mambo ya kibangibangi juu ya chama.

  Ubarikiwe san mleta thread na Mungu wangu wa israel akuinue kutoka hapo ulipo mpaka mahali unapohitaji ufikie.Amen
   
Loading...