Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,801
- 24,433
Iwapo mashoga watatambuliwa kisheria wakati wewe siyo siyo shoga na hulazimishwi kuwa shoga; je utapungukiwa na nini? Mambo ya mtu binafsi kutumia mwili wake apendavyo siyo mambo ya kitaifa; hiyo inatakiwa iwe ni ruksa mara moja katika jamii tuliyo nayo leo. Ukizuia mashoga utakuwa unaweka mianya ya kuanza kuingia maisha ya watu binafsi ikiwamo hata kuwapangia wawe wanapandana na wenzi wao wa ndoa mara ngapi kwa wiki. Kama serikali haimpi mtu chakula na wala haimlipii kodi yake ya nyumba, ni lazima imwachie mtu huyo kutumia mwili wake katika kujipatia rizki yake. Ni kweli kuna mambo mengine hayana radha nzuri katika utamaduni wetu wa zamani, lakini kulingana na mfumo wa maisha tuliyo nao leo, mambo hayo bado hayavunji sheria kuu ya nchi.