Chama cha conservative cha Cameroon na CHADEMA

Cameroon aliongea hapa mbele ya JK na wala hakuongea haya mbele CDM, hivyo urafiki wa CDM haupo ktk ushoga kama mkutano wa huo aliohudhuria JK, IKUMBUKWE cdm ina urafiki na vyama vingi barani Africa na ulaya na hata AUSTRALIA
 
Kuna mambo yameshaanza kuumiza vichwa vya serikali ya kikwete, wanakuja na utetezi dhaifu kwamba hawakubali misaada ya UK kwa hoja ya ushaga.
Je UK ingekuja na hoja ya kutupa maiti barabarani huko North Mara kitu ambacho ni moja ya kukosa haki za binadamu serikali hii hii ingekuja na utetezi gani kama si kujitetea kwa kusema kuingilia mambo ya ndani ya nchi?
 
Viongozi wa chadema huwa wa kwanza kuwasemea wananchi mbona katika hili wapo kimya ?au ndio ajenda waliyokua nayo chini ya kapeti wakichukua hatamu?dili limeshabumbuluka.
 
Umezungumza mambo mengi mazuri na yenye mashiko lakini ni vyema tukakubaliana kuwa CDM na CONSERVATIVES ni marafiki, na katika urafiki huo CDM huwa anafadhiliwa na CONSERVATIVES katika kuendesha harakati za kisiasa hapa nchini. Kama huo ndio ukweli CONSERVATIVES kupitia serikali yake imeweka wazi kuwa bila Nchi zetu kukubali haki za binadamu kwa kujumuisha USHOGA kuwa ni sehemu ya haki za binadamu hivyo itambuliwe kisheria ktk nchi zetu wao kama serikali ya Uingereza hawatotoa ufadhili kwa nchi zetu. Kumbuka uhusiano wa CDM na CONSERVATIVE si wa Cameron na Freeman au na Dk Slaa bali ni uhusiano wa vyama hivyo lazma kutakuwa na MOU inayoongoza ushirikiano huo au urafiki huo. Hivyo majibu ya CDM yatatuweka wazi kuhusu kilichomo ktk MOU yao kama inahusisha kutambuliwa kwa USHOGA kama sehemu ya msingi ya haki za binadamu au la. Pili kama ktk MOU hawajazungumzia sera au mambo ya haki za binadamu ni wazi CDM wanapaswa kutueleza nini msimamo wao kuhusu mwenendo wa sasa wa swahiba wao CONSERVATIVES maana kama leo wanazishini kiza nchi kukubali USHOGA ni wazi kesho wataamia kwa vyama wanavyoshirikiana navyo nao watambue ushoga. KUMBUKA kwa sasa hapa DUNIANI hakuna ushirikiano usio na manufaa kwa pande zote mbili. (labda shirikiano zinazoandaliwa na mafisadi wetu wa TZ waitwao na chama chao MAGAMBA) lakini ushirikiano wowote ni lazima unufaishe pande zote kama sio sasa basi baadae, hivyo kama CONSERVATIVES hawanufaiki sasa kwa ushirikiano wao na CDM wanatumaini baadae CDM wakishika DOLA wao lazima watanufaika na opportunity za kiuchumi na kijamii zilizopo TZ hivyo CONSERVATIVES uwasaidia CDM ili wajekushika DOLA ili uhusiano wao ulete faida na kwao pia ktk kushirikishwa ktk shughuli za kiuchumi hapa TZ ambapo watafaidika kutoa ajira kwa wananchi wao, kupata soko la bidhaa zao na kama CDM watakuwa wasaliti kwa nchi yao basi wao CONSERVATIVES wanufaike na Rasilimali zetu.

Hivyo kama ufadhili wao kwa CDM unalengo la kuwasaidia washike DOLA na kwa sasa CDM ni chama MBADALA wa CCM hapa BONGO ni wazi ushirikiano wa CDM na CONSERVATIVES unagusa si maslahi ya wanachama wa CDM bali na WATZ kwa ujumla maana matokeo ya uhusiano wao yakiwa mazuri tutanufaika wote na yakiwa mabaya tutaumia pia bila kujali sisi ni wana CDM au la. Na sharti la kukubali USHOGA lina athiri nchi kwa ujumla si chama pekee hivyo kusema Kuwataka CDM wajibi hatuwatendei haki si kweli. WATOE MAJIBU ILI TUELEWE MSIMAMO WAO JE WANAKUBALI USHOGA AU LA? KAMA WANA UKUBALI KAMA MARAFIKI ZAO CONSERVATIVES WATUAMBIE KAMA HAWAUKUBALI KAMA WATANZANIA WENGI WASIVYO UKUBALI WATUAMBIE. KIUFUPI URAFIKI UNAGHARAMA ZAKE NA UWA HAZIKWEPEKI HIVYO KUTOA MAJIBU NI SEHEMU YA GHARAMA ZA URAFIKI WAO HIVYO NI LAZIMA CDM WALIPE HIYO GHARAMA
Naloli heshima yako Mkuu! Mchango wako umetulia sana sana! Tunataka Michango kama hii hapa JF! Tungechangia hivi bila unazi wa wa Ki-CDM au Ki-CCM JF ingewasaidia Watanzania! You are the Great Thinker of the Year 2011! Hongera sana!
 
Nauliza swali eti ule undugu wa CHADEMA NA CHAMA CHA CONSERVATIVE kinachohimiza tuoane bado upo?na je chadema wanapataje misaada toka chama hichi kama masharti ndo hayo?
Swali hili muulize JK . Mbona unauliza swali la kimasaburi?
 
Kuna mambo yamesha.anza kuumiza vichwa vya serikali ya kikwete, wanakuja na utetezi dhaifu kwamba hawakubali misaada ya UK kwa hoja ya ushaga.
Je UK ingekuja na hoja ya kutupa maiti barabarani huko North Mara kitu ambacho ni moja ya kukosa haki za binadamu serikali hii hii ingekuja na utetezi gani kama si kujitetea kwa kusema
Hii ni hoja ya msingi.. Sana tu! Unafiki unaiponza serikali yetu.
 
Nauliza swali eti ule undugu wa CHADEMA NA CHAMA CHA CONSERVATIVE kinachohimiza tuoane bado upo?na je chadema wanapataje misaada toka chama hichi kama masharti ndo hayo?
Swali hili muulize JK . Mbona unauliza swali la kimasaburi?
 
Nauliza swali eti ule undugu wa CHADEMA NA CHAMA CHA CONSERVATIVE kinachohimiza tuoane bado upo?na je chadema wanapataje misaada toka chama hichi kama masharti ndo hayo?

Kuna thread humu JF ilisema cdm inaundugu na christian democratic party ya ujerumani naona sasa ni conservative party ya uingereza? Kesho itakuwa National Party ya makaburu wa RSA
 
Hizo ni sera za Conservative, chama cha Labour cha kina Tony Blair marufuku mashoga

Na mwenyekiti wenu kuhongwa suti na wanaume wa Kiarabu tuuiteje, Mwenyekekit wenu nae Bwabwa??
 
Kuna thread humu JF ilisema cdm inaundugu na christian democratic party ya ujerumani naona sasa ni conservative party ya uingereza? Kesho itakuwa National Party ya makaburu wa RSA

Kwani uwongo? Usilete porojo kweli Chadema wana mauhusiano na Conservative na CDU..
 
Kwani hakuna mashoga ccm?

Je mnaruhusu ushoga?Kama hamuruhusu,wafukuzeni uanachama halafu muweke wazi kuwa ccm haitaki mwanachama shoga.

Kama mnapinga ushoga,onesheni kwa vitendo msiwe na ule unafiki wa "Dont ask dont tell" waliokuwa nao marekani kwa wanajeshi wao before.

Hapo nawakumbuka MATAKA,MUDHIHIR,MACHENI nk.nk hawa hawajifichi waanze nao
 
Nauliza swali eti ule undugu wa CHADEMA NA CHAMA CHA CONSERVATIVE kinachohimiza tuoane bado upo?na je chadema wanapataje misaada toka chama hichi kama masharti ndo hayo?


Hivi CCM kupitia serikali yake hawajawahi kupata msaada kutoka chama cha CONSERVATIVE?. Nahitaji kuelimishwa kidogo.
 
Mkuu shukran sana kwani watu wanachanganya sana vitu bila kujua..Yaani ni vioja vitupu...
Conservative wanapinga Ushoga siku zote na sehemu zote kwa kufuata maadili yao wakati Liberal ndio walohalalisha Ushoga huko Uingereza na kuifanya kuwa sheria baada ya Bill kupitishwa.. Na imekuwa sheria ya nchi kutokana na wawakilishi wengi wa Liberal kuwezesha kupatikana kwa kura nyingi zaidi na hivyo Cameron hawezi kupinga leo Ushoga wakati sheria ya nchi yake inamlazimisha kuukubali. Na kama sikosei Ushoga wa wanawake haukuwa illegal UK, hivyo hata utunzi wa sheria hii ulihusu zaidi Ushoga wa jinsia moja ya kiume..

Sasa labda niwaulize nyie Liberal na CCM yenu ambao leo mnaupinga Ushoga hali mkiwa Liberal na hao Chadema Conservative wanaupinga imekuwaje?..Membe na CCM mko upande gani maanake mna wabunge zaidi ya 2/3 mnaweza kabisa kuupitisha na kuwa sheria! Lakini badala yake mmekuwa wakali kupita kiasi, ghafla mnageuka na kuwa conservative!

Wanajaribu mno kupotosha umma, shifting the general population's idea kuelekea kwenye mambo yasiyo hitaji mijadala, kila kitu kuchungu hapa bongo, hata chumvi inapaa bei, kashfa za akina Jairo, DOWANS kulipwa, TANAPA- na uuzaji wa wanyama mali ya asili, na nkupa sure mkuu, ipo siku hapa karibuni utasikia mlima Kilimanjaro umeuzwa, na hivi sasa waziri mkuu anatumika kufanya matangazo kampuni binafsi AIRTEL, yote haya wanajaribu kuya-camouflage na upuuzi huu! They better be wary, nchi sasa haitaki kuburuzwa!
 
Kwa hiyo unataka kusema Maswala ya USHOGA tuwaachie Conservative na CHADEMA au kwa maana nyingine unataka kusema hayawahusu watanzania wengine? Chadema ni chama sawa lakini endapo wataunda serikkali si ni wazi wataikubali hii sheria? hapa unatunganya wewe. Nashauri CHADEMA wenyewe watoe tamko si kuwasemea

Hauna hoja ndugu, kama vipi muandamane ili balozi wa Uingereza afukuzwe, sidhani kama anaiwakailisha nchi yake kwa CDM, na Cameron ni Waziri mkuu wa Uingereza, so anawakilisha nchi na siyo chama!!!! magamba mbona ni elimu ndogo sana hii??? au "DR" Kikwete huwa anawakilisha chama kule ankozurura? i mean anakofanya ziara? Halafu conservatives maana yake hata huo ushoga wanapinga mno THEY 'RE THE CONSERVATIVE! Huwezi kujibu hoja hapa wewe just recess!
 
Back
Top Bottom