Wanabodi.
Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kinatakiwa kiweke wazi msamamo kwa watanzania mahusiano yao na chama cha Conservative cha Uingereza..
Conservative ni wadhili wakubwa wa Chadema wanawapa misaada mingi sana Chadema.
Tunakumbuka 2005 na 2010 Chadema walipokea misaada mingi kutoka Conservative, Pikipiki, Magari, Baiskeli, pamoja na pesa..
Waziri mkuu wa Uingereza Davidi Cameron, kutoka chama cha Conservative, alitoa kauli kwenye mkutano wa nchi wanachama wa Jumuia ya Madola (CHOGM) uliofanyika Perth, Australia..
Nchi zinazoomba misaada kwao zitambue haki za mashoga kama moja ya masharti ya kupewa misaada hiyo..
Tunaomba viongozi wa Chadema walitolee maelezo jambo hili sababu kati ya wanaopokea misaada Chadema nao inapokea
ubatili mtupu, kwani ni kwa nini jamii yetu inachukia ushoga?-hata mmi nachukia sana tena sana na nikiona shoga au hata nikisikia uwepo wao napata kichefuchefu.
Lakini huwa najiuliza na naomba wan jf tujiulize, hivi ni nini hasa msingi wa sisi kuuchukia ushoga?
Ni mafundisho ya dini zetu? Ni maagizo ya vitabu vyetu vitakatifu?
Kwamba tunaogopa dhambi?
Tunaogopa kumkosea mungu wetu mkuu?
Na ufisadi je?
Uzinzi je?
Uwongo je?
Wizi je?
Udikteta?
Ubinafsi je?
U sisi tu je?
Yeye aliye msafi na awe wa kwanza kurusha jiwe.
Ushoga si haramu zaidi kuliko hayo mengine,
ccm na serikali yake haina haki ya kupinga ushoga kwa nguvu zake zote.
Ukichukia dhambi moja na ukakumbatia zingine inakuwaje?
Nadhani hizo nchi za magharibi zilijiuliza sana maswali haya kabla ya kutoa huo uhuru wa mashoga.
Naomba nieleweke kwamba mimi siungi mkono na wala sitaunga mkono ushoga.
Hivi kwa mfano shoga akikuuliza swali hili, ipi ni haramu zaidi kwa jamii ushoga na uzinzi utajibu vipi?
Ufisadi na ushoga?
Mbona mafisadi na wazinzi serikali zetu zinawapenda?
Jamii zinawafanyia sherehe mafisadi na akina membe hawasemi?
Serikali na wananchi wengi wayatendayo kila siku hayana tofauti na ushoga.
Kwanini mashoga wanyimwe haki wakati mafisadi wananyenyekew na kuheshimiwa?
Ni ubatili mtupu.