Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Hah! Chadema ni chama Rafiki na conservative ya Uingereza huo ni ukweli.Cameroon alihutubia mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola kama waziri mkuu na mkuu wa serikali ya uingereza.Msimamo alioutoa Cameroon kwenye Commonwealth not necessarily ni backbone ya ideology za chama chake.Kinachounganisha Chadema na Conservative ni mambo ambayo ni deep kabisa katika itikadi.Msingi wa kilichounganisha vyama hivyo utakapotikiswa then Chadema kwa umakini wake na weledi wa kusimamia maslahi ya Taifa ikiwamo utamaduni wa Taifa hili,haki na sheria za nchi zinazokataza ushoga basi naamini chadema haitasita kuchukua hatua
Aidha,kama itatokea masharti hayo ya kipuuzi yakatumika dhidi ya vyama shirika na Conservative naamini Chadema haitaweza ku-compromise values zake na za watanzania kwa kuendeleza ushirikiano wa aina hiyo
Sasa tujadili kwamba sisi kama Taifa tumefikaje hapa?Sera mbovu za CCM na wizi wakutisha na matumizi mabaya ya Raslimali za Taifa hili Tangu tupate uhuru na katika kipindi ambacho chama cha mapinduzi kilipewa,kilinyakua au hata kughilibu dhamana ya kuongoza na kuamua hatma yetu ndicho kilichotufikisha kwenye udhalilishaji huu.Ni dhahiri kwamba kama tungekuwa na mipango thabiti na kutumia dhamana tuliyowapa basi tusingekuwa ombaomba kiasi cha kupewa masharti yenye lengo la kudhalilisha na kuthibitisha kwa jeuri kwamba ukoloni mambo leo ni sehemu ya maisha ya Taifa hili lenye umri wa miaka 50,kimsingi mabeberu wamefanikisha hilo kutokana na usaliti wa tuliowapa dhamana.
Jambo la msingi,kila aliyeguswa na hili na kujisikia kudhalilishwa sasa achukue hatua na kuanza maandalizi ya kuikataa serikali hii ya chama cha mapinduzi ili kuepuka fedheha na balaa zaidi ya hili siku za Usoni