Chalz Baba-"Sina Contact na Twanga"

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,141
13,215
Akihojiwa na Vyombo vya Habari Mwanamuziki Charles Gabriel akisema sina Contact na Twanga (Akimaanisha Contract) ndio maana naamua kuondoKA.......alirudia neneo hilo mara 3 bila kujistukia kwamba anachapia au huenda hajui kabisa
 
Kumbe na wewe ulisikia minilicheka kinoma ii inanikumbusha siku moja shilole akihojiwa kwenye xxl akashema yeye ni celebration badala ya celebrity kweli kazi hipo.
 
hahahahahaha, ya shilole ndo imenimaliza kabisa, kwamba yeye ni 'celebration' bola huyu wa 'contact' huenda alimaanisha mawasiliano na twanga hana, japo na mimi nilimsikiliza alikuwa akimaanisha contract..khe jamani kizungu sio chetu...
 
Jamani Ncha Butu,Wasiwasi,ML chris,Stivie Kabuye,DJ JD ebu ingilieni kati kuwapiga msasa wa ki-english baadhi ya macelebrations(source shilole) wetu,kuna siku nilizisikia kauli kwao

1.Hii dhiara ya uku marekani imetuwezesha kujua jinsi ya kua good leadership----B12(Akimaanisha kua kingozi bora)
2.Haaaa uje mie ni celebrate---Barnaba(Akimaanisha yeye ni celebrity)
3.I was good-Barnaba(vp unajisikaje kwa sasa? Aliulizwa na Arnold)
4.Nitafanya futuring na Ay,pia na Prof jay katika nyimbo yangu itayokuja---Wasanii wengi wanachemka hapa,anamaanisha collabo aka featuring
 
Kati ya wasanii wa movie wanaojua kingeleza Wema namkubali sana kwa ngeli yupo bomba sana katika lugha hiyo
 
kikaza ndo nini?unamcheka nini wakati we mwenyewe kiazi tu

Unamaanisha jamaa ni kiazi anamenywa anawekwa jikoni anapikwa kwa kugeuzwa geuzwa kisha analiwa !? Am anakaangwa na kupasuliwa mayai na kuliwa kama chipsi yai...haa haa haaa
 
Kumbe na wewe ulisikia minilicheka kinoma ii inanikumbusha siku moja shilole akihojiwa kwenye xxl akashema yeye ni celebration badala ya celebrity kweli kazi hipo.

kwenye hizo ''red''....................... nafikiri ilipaswa kuwa ''hii'' ''akasema'' ''kweli kazi ipo''.
 
hahahahahaha, ya shilole ndo imenimaliza kabisa, kwamba yeye ni 'celebration' bola huyu wa 'contact' huenda alimaanisha mawasiliano na twanga hana, japo na mimi nilimsikiliza alikuwa akimaanisha contract..khe jamani kizungu sio chetu...

''ndio''........................................''bora''
 
Hivi kumbe kuna watu mpaka leo wanaamini kutokujua kingereza ni ishara ya ujinga! Kweli safari ni ndefu ,watu wanaongea kiswahili lugha waliyozaliwa nayo wanachapia ndio ije kingereza lugha ya kujifunzia ukubwani.Tuache uvivu wa kufikiri.Chalz Baba kipaji chake na kutokujua lugha ya kingereza vinamahusiano gani? Ama mnataka kutuambia akiwa anajua kingereza ndio atakuwa anaimba zaidi kama kina Kofi Olomide ama R.Kelly!?. Wiki 2 zilizopita nilikuwa naangalia mahojiano ya fally Ipupa -BET.Fally aliongea kingereza kibovu sana ,ila hiyo haimpunguzii kipaji chake sababu anajitambua na kujikubali.Hata washabiki wake wana mkubali kwa hicho kingereza chake kibovu.Hao kina Wema mnaowasifia wanajua kingereza kimewapeleka Holiwood? Ama wamepata tunzo za kimataifa kwenye uigizaji/filamu?. Ushabiki wa kimawazo ni mbaya sana na ndio unatufanya tushindwe kuendelea kwa kuwa hatujitambui na kujikubali .Huwezi kajikubali kama hukubali wenzako kwa machache mazuri wanayofanya.Tufunguke tuache ulimbukeni na ufinyu wa mawazo.
 
english co ishu jaman sema inaboa kuona mtu anajifanya anajua wkt 0..hata kiswahili kinatushinda kuna mtu hapa kaandika bola badala ya bora..
 
nyie si wa kumcheka chalz baba

Hakuna aliyemcheka chalz hapa,hoja ya msingi hapa kuongea vitu ambayo hauvijui,contacts na contracts ni vitu viwili tofauti kabisa,pia kingeleza na kingereza tofauti yake ni nini kimaana? English na Engrish?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom